Wake wa Marais wetu na Mambo yao

jamni mmesoma mtanzania leo? aliyemsaidia ana mkapa kudhulumu wafanyakazi wa serikali nyumba hizi, ni mramba wakati akiwa mkuu wa mkoa wa mbeya.
 
mkapa hakuwa na ujanja wowote kwa pesambili mramba kwa sababu hizi
1.0, wakati mkapa akiwa waziri wa mambo ya nje, hakuwa na kibanda zaidi ya nyumba alikokuwa anaishi ambayo serikali ilipangishwa toka national housing, nyumba hii ipo osterbay karibu na agakhan hospital, kwa miaka kadhaa ilikuwa inatumika kama makzi ya waziri wa mambo ya nje

2, mwinyi rais alipofanya mabadiliko ya kwanza ya baraza la mawaziri akamteua diria hassan kwa waziri wa mambo ya nje, mkapa akaundiwa wizara mpya inayoitwa ya habari.
na kama mnakumbuka mramba kiakota akabaki kuwa mwenyekiti wa bodi ya national housing corporation

3. diria hakufanya ajizi akadai apewe ile nyumba. ilibidi mzee mzima aadhirike wakataka kuhamia pagala la mama ana liko kimara, halikuwa limemalizika, hata umeme wala maji hamna.
4. mzee mzima mkapa akamkimbillia mramba amtamfutiie house ya chapu chapu huko NHC, mramba akamwita mwanasheria wa NHC asaidie hili. kumbe serikali ilikuwa kweli imepanga ile nyumba lakini haikuwa inalipa kodi. ikatafutwa lophole, kodi ikalipwa kwa mkupuo kwa jina la mkapa, na NHC, ikatamka kuwa mkapa mdo mpangaji halali wa ile house, mpooo!!!!, yule mwanasheria aliyecheza hiyo simtaji, ila alikuja kuukata sana kwenye utawala wa mkap. mpooo? kwa hiyo mramba akamsadia mzee mzima asidhiriwe na mzanzibar diria

AKUFAAYE WAKATI WA DHIKI?........kama siyo kimbelembele cha mrema kumpaka mramba kule rombo mpaka akashindwa ubunge 1995! mramba angekuwa ndiye waziri mkuu...

YETU MACHOOOOOOOOOOOOOOOOO

huyo mwanasheria ni CHENGE nini
 
jamani hili swala ajibu mzindakaya mwanafamilia wa mr clean!!!!!

mama mkapa mbona ameiba vidogo jamani hao wa epa mbona hamsemi na yeye si binadamu na anatamani mbona mawaziri wengi tu wameiba na wengine wanaua vijana wetu pale magomeni na sinza kwa pesa nyingi tu haramu na kuna nyumba zinajulikana zinatengenneza mizigo kusafirisha nje!!!!wangapi hawawajui wale vijana pale airport wanaosindikiza wauza unga mpaka mlangoni na kuwapokea mpaka kwenye gari!!!!hizi story nimeahakikishiwa na mmoja wa mdogo wangu yuko usalama alikuwa pale wamempeleka moja ya mashirika ya umma ....

mwacheni alichoona kuchukua nae achekue jamani/!!!!!salimu bado uko dar ????????

nao wanaosafirisha watu kubeba unga wana mkosa yao pia ambayo hayahalalishi wizi wa mrs
 
Ufisadi haukutosha kuwapa fedha za kutosha? ni mpaka tena wawanyonye waalimu jamani? Mgodi wa kiwira mbona uanwapa pesa nyingi ? ulafi huu ndio utawaangamiza kabisa .

Hivi ule mfuko wa EOTF ni wa kwake binafsi ama nao kaupora tuu?

Mpaka kieleweke, kama ulikuwa hujui ngoja nikupe ukweli. Mfuko wa EOTF ni mali halali ya mama Anna Mkapa. Hata kama ilianzishwa ikulu na ikapata wafadhili wa ndani na nje kwa msaada wa serikali na bunge lenu la wabunge makanjanja lakini Anna aliianzisha kwa mtaji wake mwenyewe. Kumbuka mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe. Anna aliweka nguvu zake mwenyewe kuipata EOTF.

EOTF ni mali halali ya Anna Mkapa kama ilivyo WAMA ambayo ni mali halali ya mama Salma Kikwete. Nyie mlie tu, hapa hanyang'anywi mtu. Jiandaeni kushuhudia mama Salma Kikwete akiondoka na WAMA yake.
 
Kama mifuko hii ni MALI yao; kwa nini wanasubiri waume zao waingie IKULU yetu ndipo waianzishe?
 
Mkuu,
Kwanza kabisa nitumie fursa hii kukukaribisha hapa kijiweni.Karibu tufanye mageuzi ya kweli kwenye taifa hili lililopoteza dira.wewe una wajibu mkubwa kabisa katika kuwa wakala wa mabadiliko ya kweli.

Btn: mbona hii taasisi alikua anafanya nayo kazi as if ni public institution? Nguvu za kumtetea hapa sijui unazioa wapi mkuu? Labda kuna jipya ambalo hatulijui? Basi hebu rudi basi kwa hisani yako utueleweshe.
 
Kama mifuko hii ni MALI yao; kwa nini wanasubiri waume zao waingie IKULU yetu ndipo waianzishe?

Ikulu ndiko mitaji inakopatikana kwa urahisi. Mbona watu wengi wamepata mitaji kupitia mashirika ya umma lakini hamuwasakami kama mama???? Mama kawatumikia miaka kumi bila mshahara. Sasa kumbe mlitegemea yeye aishije??? Mlitegemea mama akale polisi???
 
Kwani KAACHIKA? Ikulu yenye mitaji ni hii ya Watanzania? Mwalimu asitusikie huko alikotangulia.
 
MRAMBa na mkuu wa wilaya wa wakati huo mbeya, walimlazimisha aliyekuwa municipal director wilson kabwe kutoa letter of offer kwa mama ana mkapa na baadaye kumlikisha eneo lenye nyumba za serikali.

waliouziwa nyumba hizo ni pamoja na mhandisi wa sekretariat ya mkoa. hadi leo wamekwama kupata hati hali wakiwa wamelipa
 
Date::7/23/2008
Walimu wajutia kilichowapeleka kukopa Bayport
Na Tausi Mbowe
Mwananchi

BAADHI ya walimu wamejitokeza hadharani na kudai Kampuni ya Bayport Financial Services, ambayo mke wa Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Anna ana hisa imekuwa ikikata zaidi ya mara tatu mkopo waliyochukua.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Mwalimu wa Shule ya Msingi Hekima zamani Buguruni B, Scolastica Kaduma, alisema kampuni hiyo imekuwa ikiwanyonya bila huruma kutokana na kulipa kiwango kikubwa cha deni halisi ikilinganisha na benki nyingine ambako baadhi yao wamechukua mkopo.

Kaduma alitoa mfano wake kwamba Aprili mwaka jana alikopa Sh470,000 kutoka Bayport, lakini anaendelea kukatwa Sh43,747.75 kila mwezi kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa na bado anadaiwa Sh1.1 milioni.

"Mpaka sasa nimeshalipa zaidi ya Sh437,000 katika kipindi cha mwaka mmoja, lakini bado karatasi yangu ya malipo inaonyesha nina deni la Sh1,049,922," alisema huku akionyesha karatasi hiyo.

Kwa mujibu wa hesabu ambazo Mwananchi ilifanya, zinaonyesha walimu hao wanalipa riba ya asilimi 6.53 kwa mwezi sawa na asilimi 78.36 kwa mwaka.

Hesabu hiyo inafanya walimu hao kulipia zaidi ya mara tatu ya kiwango halisi cha mkopo.

Kwa mujibu wa mchanganuo ambao Mwananchi imefanya, inaonyesha katika mkopo huo mwalimu huyo analipa Sh13,055.55 kama makato ya kila mwezi sanjaro na riba ya Sh30,691.20 kwa mwezi na kufikia Sh43,746.75.

Wakati zikiibuliwa tuhuma hizo dhidi ya Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa na mkewe Anna, bado kuna tuhuma lukuki ambazo hazijatolewa maelezo zinazowahusu kwamba walijihusisha na biashara wakiwa Ikulu.
 
Wana ndugu hili jambo nafikiri inatukumbusha ule uzama wa ufalme hivi sasa kila sehemu ya zanzibar utokosa jina la karume mwishoni...sasa naona na hawa walio uongozini wameamua kula kivyao....pale forodhan tulipokuwa tukiingia na kutafuta samaki wa pweza ukiwa na mkeo...leo hii kumefungwa wanaakarabati na habari za uhakika ni kwamba mke wa RAIS wa ZANZIBAR mama shadya karume katunukiwa kipande ile...kwa hiyo wale ndeugu zzetu waliotoka bara kuja zanzibar kuuza pweza ni wakati wa kurudi kwao mbagala kuangalia kama wnaweza pata mafao ya nyumba zao walizokimbia.....sioni mantiki ya kugawa hizi nchi kwa kisingizio cha me wa rais...jamani mama mkapa bado kidogo atuache UC*** WA MNYAMA KILA SEHEMU YAKE MPAKA MAJUZI KAJIFANYA KUMUUZIA MTU LILE HOTEL LAKE KUBADILI NA JINA KUMBE FIX...MAMA SALMA NAE ALTHOUGH AJATOKA RASMI NATUMAINI NNDANI YA MIAKA 5 NA WAMA YAKE LAZIMA WAMTAMBUE...HAYA WA MADHABAHUNI ALI MADHABAHUNI
 
Jamani wake za marais mtatumaliza watoto wetu watokaje???????????
 
....pale forodhan tulipokuwa tukiingia ...leo hii kumefungwa... ni kwamba mke wa RAIS wa ZANZIBAR mama shadya karume katunukiwa kipande ile...kwa hiyo wale ndeugu zzetu waliotoka bara kuja zanzibar kuuza pweza ni wakati wa kurudi kwao...
Duh! Hivi wauza pweza na ngisi pale forodhani ni wabara... eh!?
 
Viongozi wetu wanapaswa kujua kwamba wakipata public offices siyo sehemu za ku -accumulate wealth na kujipendelea.
Huyu Mama Shadya na kupewa hiyo Forodhani amepewa kwa sababu zipi hasa?kama siyo sababu za kimaendeleo wala kuwanuafaisha watu wa sehemu husika basi it does not justify hicho kitendo chao cha kifisadi!
 
hasara loo mtu mzima kuvamia mambo ya udaku na kuanza kulaumu kwanza fuatilia upashwe na ndio unene sio upayukwe utadhani umepandwa na kibuki

pole mradi
 
Back
Top Bottom