Jinsi marafiki wa mpenzi wako wanavyoweza kukuharibia mapenzi yako, yamenikuta

george aloyce

JF-Expert Member
Aug 22, 2017
1,177
1,827
"Wakati niko chuo kuna manzi nlikua nae nilimpenda sana na nlkua na mipango nae mizuri tu tukimaliza kusoma tuwe pamoja.

Siku moja nikamkuta yuko na rafiki zake wamekaa nkamwita pembeni nikaongea nae kisha nikaondoka zangu. Baada ya hio siku kila atakapokua na rafiki zake anasema hataki nimfate nkatulia tu nkajua labda wivu.

Tulivomaliza chuo mapenzi yakawa kama ya kufos ivi nisipomtafuta basi hatuongei nkajiongeza nkamove on. Sasa mwaka huu kaja kunitafuta anaomba msamaha turudiane nkamwambia simsamehi hadi atakaponipa sababu kwanini alifanya vile.

Kumbana sana akaja akasema kua rafiki zake walimwambia kua hatuendani yani yeye alkua mnene mie mwembamba ndomana akawa anaona aibu nionekane tena mbele ya rafiki zake.

Cha kushangaza mmoja wa wale rafiki zake sjui alitoa wapi namba yangu akanichek akanitongoza ila sikumwambia yule dem maana sikutaka kuwagombanisha.

Binafsi nimemsamehe ila siwezi kurudiana nae tena maana kwanza saivi nipo mkoa mwingine kikazi na mambo ya long distance relationship sitaki kabisa na pia ili ajifunze tu kwa faida yake.

Nlichogundua bana wanawake wananafkiana sana na hawapendani kama sisi wanaume tunavopendana kiwana.

Share wanawake wajifunze kama wanataka ushauri watafte watu wazima na sio vijana wenzao tena hasa ambao hawajaolewa.
 
Kitu ambacho nakiogopa maishani mwangu ni kuwashirikisha rafiki zangu habari za mahusiano yangu.. bora waendelee kujua niko single sikuzote
Dada yangu tuliwahi kujua mpenzi wake mmoja tu kama ndugu yani kishikaji mana ni watu walioajiriwa serikalin miaka ya kikwete anapoingia madarakani.
Toka na hapo sijui waliachana au bado wapo ila tuna muona yupo single mpk wazazi wameamua kumwambia aolewe mana yupo single mda mrefu.

Usishirikishe furaha yako kwa watu itakuwa huzuni mda mfupi tu.
 
Yeah ni kweli... marafiki zangu hua kila siku wananiuliza una shida gani mbona hatujawahi kuona hata ukizungumzia habari za mapenzi au hata kukuona uko mahali na mpenzi au hata kupost😃😃.,, naishiaga kucheka tu kwasababu naona wao wanavyosumbuka na kuchitiana wenyewe kwa wenyewe, yani full unafki
 
Screenshot_20231211-065858_X.jpg
 
marafiki ndo wanaongoza kusababisha ndoa kuvunjika, hasa marafiki wa mwanamke wa kike, kuna mmoja alisambaratisha ndoa yake kwa vurugu kubwa, hakumsikiliza mama mkwe, baba mkwe, shemeji wala wifi, yaani alikuwa hashauriki, yule mwanamke ilifika mpaka anawaambia wakwe zake, hii familia yenu ina laana, hata hiki kidogo mlichonacho ni baraka zangu tu, ngoja niondoke mfe njaa, baada ya mwaka anakuja kuomba msamaha, kuulizwa kilichomkutaga ni nn anasema ulikuwa ushauri wa marafiki. watu walimjibu kistaarabu tu, nenda ukaolewe na hao marafiki au waambie wakutafutie mume, sisi hatukutaki tena,
 
Walimpa majibu mzuri sana
 
Back
Top Bottom