Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 10,129
- 35,153
Sio siri tena tangu Papa na Vatican kutoa miongozo ya kuukumbatia ushoga, kwa sasa wakatoliki wengi wameanza kupoteza furaha, amani, ujasiri na ufahari wa kujivunia ukatoliki.
Papa na Vatican walianza kutoa kauli tata za kuona ushoga (kubadili jinsia nk) sio dhambi ya kukemewa na kanisa (yaani mashoga wavumiliwe na kutambuliwa kama sehemu ya waumini ndani ya kanisa katoliki), baadaye wakaja kutoa ruhusa mashoga kuwa wadhamini wa sacramenti za kikatoliki (Ubatizo, Komunio, ndoa) na sasa ruhusa kwa mashoga kubarikiwa! Mwelekeo unaotabiriwa kufuata ni kanisa katoliki kuanza kufungisha ndoa za mashoga na hitimisho ni kanisa katoliki kuja kuruhusu kuwa na makasisi mashoga.
Wengine walijaribu kutetea Kanisa Katoliki kwa kusema Papa na Vatican wamenukuliwa vibaya, lakini kadri muda ulivyokwenda hali imezidi kuwa wazi na mbaya kiasi cha watetezi wa Katoliki kuanza kusalimu amri.
Kwa sasa ukatoliki umewekwa kapu moja na harakati za kuukuza na kuulinda ushoga duniani.
Mwaka huu huenda ndio mwaka mbaya zaidi kwa waumini wa kikatoliki katika kujivunia imani yao. Upepo bado unavuma, mawimbi bado yanaibuka na chombo kimeanza kuyumba huku safari ikiwa imeshika kasi.