Jackwillpower
JF-Expert Member
- Oct 4, 2017
- 2,301
- 3,414
Papa huyu mjesuit anawaumiza sana Wakatoliki waaminifu, hajui tu
Ingawa ndio injili ya wajesuit ya umoja katika tofauti. Mnamo karne ya 17, Wajesuit walifanya maridhiano na Wachina juu ya ibada zao za kuwaomba mababu zao waliokufa kama sehemu ya imani ya Katoliki.
Wajesuit wakakubali na ikawa hivyo, na mfalme wa China akawapenda sana kwa ustadi wao na kuupa utamaduni wa China heshima, kidogo tu abatizwe. Leo China ingekuwa ni taifa la Kikatoliki.
Lakini mvurugano ulitokea kati ya Wadominika na Wafranciskana dhidi ya injili ya Wajesuit ya maridhiano. Kesi ikafika hadi Vatican kwa Papa. Wajesuit wakajenga hoja lakini wakashindwa mbele ya Wadominika na Wafranciskana, ikaamulia injili yao ya maridhiano huko China ikomeshwe.
Mfalme wa China hakupendezwa na mvurugano huo. Papa akamuandikia barua mfalme Kang wa China dhidi ya injili hiyo na akimtaka ajisalimishe kwenye ukatoliki pasee aachane na wazo la Wajesuits. Mfalme alikerwa na barua hiyo na akaichana mbele ya baraza lake.
Maana aliona papa kavuka mpaka kuingilia uhuru wa China. Na toka siku hiyo akapiga marufuku mahubiri ya Wakristo na kuwafukuza Wadominika, Wafranciskana na akaamuru Wachina wasiwe Wakatoliki kwa amri ya kifo.
Wajesuit walipata kibali machoni pake sababu ya aina ya injili yao ya maridhiano, maana walivalia kama makasisi wa Confusian na mfalme aliwachukua kuwa washauri wake na wakaiboresha sayansi ya China. Lakini mnamo 1773 shirika la Jesuits lilivunjwa na papa Clement IV kwa shinikizo la wafalme wa Ulaya, hivyo mission yao ndani ya China ikakoma. Kwanini shirika lao lilivunjwa, hiyo ni mada nyingine....
Walirejeshwa rasmi mnamo 1814 na Papa Pius VII, na leo wanaye papa anayetokana na wao. Inasemekana walirudi Vatican kibabe na sasa ndio wanaoliendesha kanisa. Na mkuu (jenerali wao) amebatizwa jina la Papa mweusi (black pope) kuashiria yupo nyuma ya Papa mweupe (White Pope).
Hivyo tegemea injili ya maridhiano isiyotaka kuudhi watu bali kuridhisha matakwa ya umma. Ingawa kuna vuguvugu la upinzani ndani ya kanisa dhidi ya injili ya Papa huyu.
Hivyo wakatoliki waaminifu wajiandae kwa mambo ya kukera zaidi kutoka kwa Papa huyu.