Wakati wa mimi kusema umefika

Wakati wa mimi kusema umefika

Watu mnamtukana Mama zenu na Dada zenu na wake zenu kwa kudhani kuwa Mnamtukana Deus F Mallya. Poleni sana
Mkuu Wewe Usiogope, kuwa na tabia za kike sio kutukana, wanawake ni mama zetu, dada zetu na wake zetu, kwao hizo tabia za kike ni sifa za mwanamke!, tatizo ni jianadume zima, linapoibuka na tabia za kike kike, kutishia watu nyau, kwa mtindo wa niseme nsiseme!, mwanamume ukiamua kusema, unasema sio umeamua kusema, unasema mtasema na mwisho wa siku hausemi chochote!.

Thanks.

Pascal.
 
Hivi jamani,,ndugu yangu Ben Saanane yuko wapi..,mbona simuoni akitokwa mapovu kwenye thread kama hizi...yaani Mzee wake anakaribia kupelekwa lupango na yeye amekaa kimya kama hayamuhusu..njoo uwaambie umma wa JF kuwa hatuhusiki na atakachosema Mallya ni uzushi.

KUNA HOJA GANI HAPA ? HUYU ALINASWA AKIRUBUNIWA NA DIALLO ( KUMBUKA KWAMBA NI AIBU SANA MTOTO WA KIUME KURUBUNIWA ) ana LIPI ?
 
who was behind the assassination of chacha Wangwe Deus F Mallya ?kuepuka maswali mengi nakuomba ungesimulia ilikuaje siku hiyo ya tukio then baada ya hapo tuanze kuuliza maswali(ushauri tu)
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Arafat, naona umeandika kwa uchungu mkubwa na pole sana kwa hilo.
Hapo kwenye red wengine wanasema ni moshi wa 'kibatari' ndio umeharibu akili za Watz!
 
Tena huu ndio muda muafaka Mkuu,, we sema tuu! Manake Mbowe anahitaji mwenye ubavu wa kupambana nae!!
Tupe sisi hizi taarifa tuone kama atakuwa na jeuri tena.....
 
ukiua usimtazame mhanga machoni, lazima atakuwewesua uanze kuropoka tu.
 
Mkuu Deus Mallya, kwanza asante kwa kuamua kutaka kusema!. Kwenye jamii yetu, tuna watu wa jinsia mbili, ya kiume na ya kike!. Watu wa jinsia hizo wanakuwa na tabia na mienendo inayoendana na tabia zao. Yaani mwanaume anakuwa na tabia za kiume, na mwanamke anakuwa na tabia za kike!. Ila pia hutokea baadhi ya wanaume, kuzaliwa wanaume na maumbile ya kiume lakini wakawa na tabia za kike!, vivyo hivyo kuna wanawake wenye maumbile ya kike na tabia za kiume!.

Moja ya tabia za kiume kwa mwanamume ni kuwa na msimamo thabiti, msimamo imara, akiamua kitu, ameamua na anasimama nacho mpaka mwisho wake, na ikibidi kufa, anakufa na msimamo wake huku akiitwa shujaa!. Sasa wewe kama ni mwanamume na unazo tabia za kiume, ulipoamua kukaa kimya na kunyamaza, ni lazima uendelee kukaa kimya na kunyamaza mpaka mwisho!.

Hili tishio la oh mara ntasema, au wakati wa kusema umefika!, hizi ni tabia za kike!, mwanamume akiamua kusema, hasemi ntasema bali husema!. Mwanamke ndio huamua kutishia aseme au asiseme, na hata akitong..zwa anajijua kabisa amekubali, atajifanya hataki ili uonyeshe kuhangaika kumpata!.

Hii ya wewe kutishia kuwa utasema, its as if ulilipwa kiasi fulani hapo mwanzo ili unyamaze, na ukanyamaza, sasa umeishiwa, unataka kuendelea kulipwa siku zote kwa kukaa kimya!, yaani ukimwa wako ndio ajira yako, ili uendelee kulipwa, unatishia kusema ili watishike na kukulipa tena ili usiseme, ukae kimya!.

Nakushauri, kama umeamua kweli kusema, amua moja na useme sasa!, hukupaswa kusema utasema, ulipaswa useme tuu tujue moja, kitendo cha kutishia nyau kuwa utasema, kinaweza kupelekea wale waliokulipa siku zote kukaa kimya, wakakuona you are not an asset, you are a liability which needs disposal kabla haijawa too risky or threat, hivyo ukanyamazishwa jumla!.

Ni ushauri tuu.

Asante.

Pasco.

Mkuu Pasco kimantic tayari amesha divulge,hofu yangu wasije wakamu eliminate tu,ameshafika kwenye no turning point
,mwisho kabisa nadiliki kusema mtandao wa Zitto kabwe chadema iwapo atafukuzwa rasmi utakitafuna sana chama kumbuka alisema hivi "Chacha died i wont"-The guy(zitto) seems to know the tragedy too
 
Salaam!

Kwa muda Mrefu nimekuwa nikipata msukumo unaonitaka kuzungumzia maneno yaliyosambaa mitandaoni na kwenye vyombo vya habari hivi karibuni kutoka kwa ndugu ma makundi mbali mbali.

Kimsingi sintajibu wanayotaka kwa sababu nimeendelea kupokea jumbe za Matusi na kejeli hata kuvamiwa na wanaodai ni wafuasi wa CHADEMA wakitaka niendelee kuwa Kimya!. Wapo walioamua kujitaja majina yao ili nijue ni kiasi gani wako 'Serious' kwenye kile wasemacho!.

Japo nilishatoa taarifa Polisi, kwa sasa nimechoka kuishi maisha ya kuwindwa ndani ya Nchi yangu. Nimechoka. Nitakachofanya ni KUONGEA na si KUJIBU kilichosemwa na yeyote kuhusu Mimi na 'Ajali ya Pandambili'

Naamini kwa Mungu siku zote
Naamini nikifa ni kwa Mpango wake
Nikifa ukweli Utaishi hadi vizazi vijavyo.

Deus Mallya
Dar es Salaam.

Nilidhani umesema kumbe hata hujasema. Tunasubiri useme

 
Ngedere wa Ufipa miti yote leo inateleza
 
Ben Saanane kuja hapa. kuna mtu anahitaji kulishwa ile sumu ya zitto.
 
Sina imani na Mallya huyu Kama ni Kweli ndo Mallya aliehusika na ajali ile!!
 
Kuna siku nilimshuhudia yule kijana Habib Mchange akifoka kwenye TV kwa kujiamini kweli kweli. Siku hiyo alikuwepo Mnyika na kipindi kikiendeshwa na Mzee Angalieni Mpendu kupitia Star TV. Mchange alinena maneno mazito, nikawa najiuliza huyu mtoto ananena haya ana ushahidi.

Japo sijajua Mallya atasema nini, lakini hili la kugusia kwamba amekuwa akitishwa na kuambiwa akae kimya na watoa vitisho ni wanaosadikiwa kuwa wafuasi wa CHADEMA limenifanya nikumbeke ufokaji wa Mchange.
 
Back
Top Bottom