Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 11,866
- 4,252
Ni nani wajumbe hao?
- Ni walioko kwenye Kamati Kuu ya CCM Taifa (National Executive Council – NEC), pamoja na wajumbe maalum wa kutoka mikoa (Wilaya/Mkoa) na vyama vya UWT, UVCCM, Wazazi nk, ambao wako kwenye ngazi za uchaguzi wa ndani.
- CCM imeongeza idadi na nafasi kwa wajumbe kutoka vikao vya mkoa, wilaya na vikundi maalum ili kuwapa sauti kubwa zaidi uchaguzi wa ndani, lakini mgawanyo wa nguvu bado uko mikononi mwa Kamati Kuu
Tunawaomba sana wajumbe, na hata Kamati kuu. Tafadhali sana mtuletee wabunge na madiwani ambao ni watanzania halisi na waio na nasaba na uongozi wa taifa hili. Tuleteeni watu ambao hawana maslahi binafsi na koneksheni zisizo na tija kw amanufaa ya Tanzania.
Nyie wajumbe ni watu na nusu kwetu watanzania. Mtakuwa wajumbe si watu kwao wenye makusudio binafsi. Tunajua mnataka chama chenu kiendelee na hatamu ila basi tuwekeeni watu ambao hawajafungwa mikono na midomo
Mtapatiwa angalau watia nia 6 kila jimbo kwa nafasi ya ubunge, ambapo majimbo ni 272 kote nchini. Ndani ya hiyo idadi kuna watu watakuja kutuuumiza kwa kuwa tayari wana maagano na vifungo kwa watawala. Hawtakuwa na nia njema sana kwa Taifa hili.
Tafadhali washangazeni watanzania kwa kuwapa furaha, shangwe, kicheko na matumaini