Waitara: Wanasiasa wanaokaa chama kimoja muda mrefu ni Manungayembe

Waitara: Wanasiasa wanaokaa chama kimoja muda mrefu ni Manungayembe

Kupitia kipindi cha Jahazi,cha Clouds fm,Mbunge wa zamani wa Ukonga kwa tiketi ya CDM, Mwita Waitara amesema wanasiasa wanaodumu kwa muda mrefu kwenye chama kimoja ni "Manungayembe".

Waitara amesema huwezi kuwa awamu zote we upo upinzani tu lazima ubadilike..."huwezi kuwa miaka yote upo upinzani tu kaja Nyerere we ni mpinzani, kaja Mwinyi we ni mpinzani, kaja Mkapa bado uko upinzani, mzee Kikwete we upo upinzani hadi Magufuli bado unapinga tu we huwezi kuwa mwanasiasa we ni Nungayembe tu" amesema Waitara.

Waitara alijiuzulu nafasi yake ya ubunge na kujivua uanachama wa Chadema na kujiunga na CCM mapema mwezi huu, kwa madai ya kuunga mkono juhudi za rais Magufuli
Viongozi wa CCM wanajua kutukana...
 
Hizi kauli zake zinaweza kusababisha hata wapiga kura wa CCM wasimpigie kura
 
Huyu anatakiwa kunyang’anywa ‘silaha’ yake haraka haraka
 
Kwahyo anatuaminisha na huko alikohamia nako pia atahama...
Malaya mkubwa wa kisiasa
 
Jamaa ameshavutishwa jani la kijani. Anatia huruma kwa kweli.
 
Hapo kuna logic; maana huwezi Ukawa unapingana na kila mtu; hizo ni dalili za kuwa na matatizo
 
Mtu kama huyu anaonesha udhaifu kotekote.

Anaonesha udhaifu huko alikotoka chamani, kwa sababu walimkubali awe kiongozi.

Anaonesha udhaifu huko alikoenda chamani, kwa sababu wamemkubali awe kiongozi.

Anaonesha udhaifu shule zote alizopitia. Hazijaweza kumtayarisha kuwa kiongozi mzuri.

Anaonesha udhaifu bungeni mwetu,hakujaweza kumnoa.

Anaonesha udhaifu kwenye mifumo ya dini zetu, haijaweza kumpa maadili.

Anaonesha udhaifu mpaka kwenye familia, haijaweza kumlea akajisitiri.
 
Pamoja na form four yangu mbovu, sijawahi hangaika maisha kama hawa wasomi wetu. Tena wala mnyenyekea mtu ili nipate mkate wangu wa siku.
 
Anaongeaga kama mlevi fulani.Namuonaga kama mtu aliyepiga vyombo anabwabwaja.

Kungekuwa na Demokrasia ata hile ya kikwete.Huyu ubunge angeusikia kwenye redio.

Chaguzi uchwara za kumfurahisha jiwe ndio zimeleta undondocha huu.
 
Huyu jamaa anakoelekea atavua ngua hadharani

Apewe Msaada wa Kisaikolojia
 
Huyu anawaaibisha sana akina tata mura. Kama kahama wenzie wamekaa kmya mbona kiharage hakiishi kumuwasha??
 
Back
Top Bottom