Waislamu wapigwa marufuku kushiriki pasaka

Waislamu wapigwa marufuku kushiriki pasaka

Status
Not open for further replies.
mimi nachinja mwenyewe na nikiwaalika wanakula bila maswali

Eliza ulipotea wapi? Kesho panda fastjet ya kwanza uje Arusha tule pilau kwa gharma zngu Mambo ya dini tupa kule kwnz zilletwa na wazungu na waarabu
 
Kwani Redio Imani siku hizi ndiyo wasemaji wa Waislamu?

Na sasa hivi kuna Tv Imaan mwaka huu mtafurahi,kusheerekea Pasaka kwa muislamu ni haramu kwasababu mwenyezimungu amesema hawakumuua Wala hawakumsulubu Yesu/Isa.

Kwahiyo kusheerekea Pasaka ni kupingana na maandiko matakatifu Quran tukuftu.
 
ngoja uje utengwe....
heee! nitengwe na nani kwani sasa wananisaidia kwa lipi hao watakaonitenga, naishi maisha yangu aisee! Ingekuwa iraq, pakistan au saudia sawa huko wakikutenga kweli utatengeka maana hadi mfumo utakutenga lakini sio hapa tz.
 
jamani namtafuta sheih HUSIEN CHIFUPA, rafik yangu wa siku nyingi mwambieni kesho akitoka tu kwenye swala ya alfajir aje kwetu anisaidie kumchinja huyu mbuzi kwani kesho nimewaalika marafiki zangu kina HAJI,ABDVL,SHAMSI na dada zangu kina SALMA na ZAKIA.na kwa kuwa sitaki kuwalisha haram chonde chonde mwambieni aje.au kama kuna ustath mwingine plz anPM ili aje nisaidia!
 
Dah! Afazali kuna ukombozi wa kifikra humu ndani kidogo!
 
hivi kula na kuvaa vzr na kutembea ndo umeshiriki pasaka?hii radio cdhan kama ni ya waislam safi...,hii ni ya waiskam makafiri wanaodhani ukiua utaona pepo, boko haramu hawa...Mungu hashindwi kuua hata amkodi mwanadamu
 
Huyo mtoa kauli ya kibaguzi amesomea wapi elimu yake ya kislamu? Pengine kasomea katika nchi za Afghanistan,Pakistan ama Somalia.Kwa maana hiyo lazima awe na msimamo anao Amini yeye.Lakini huyu si wakumpuuza ni wakumfahamisha.
 
Mada hizi zitakuja sana wakati huu ambapo INTERAHAMWE wamesusiwa mjengo...

Kila wakati CCM ikibanwa lazima mada za udini zitamalaki...
 
Wameanza tena hawa jamaa? Kazi kweli kweli, hawana hoja kabisa hawa mburura!!!
 
hivi kula na kuvaa vzr na kutembea ndo umeshiriki pasaka?hii radio cdhan kama ni ya waislam safi...,hii ni ya waiskam makafiri wanaodhani ukiua utaona pepo, boko haramu hawa...Mungu hashindwi kuua hata amkodi mwanadamu

Wewe kiumbe na wenzako wenye mawazo mgando hebu eleweni kuwa Pasaka, christmas n.k ni sherehe zinazoambatana na imani za watu. Tumeambiwa tushirikiane lakini si mpaka katika ibada. Uislamu ndio unakataza na sio radio iman wala shekh flani. Ni Amri ya Allah subhanahu wataala. Pungezeni kelele zenu kwakuwa hazitomzuia tembo kunywa maji. Ngoja waislamu waelimishwa na waijue dini yao waache kufuata mambo yenye kuwatia katika madhambi. Sio Qur-aan, Hadith, wala waja wema wote (Maswahaabah, wafuasi wa maswahaba, wafuasi wa wafuasi wa maswahaba), wala Ma¡¯ulaamaa wa Kiislamu waliohalalisha kujumuika na makafiri kwenye sherehe zao za Kikafiri.
Miongoni mwa sherehe ambazo zinafurahikiwa mno na Waislamu ni Mwaka Mpya wa Kikiristo ingawa haimo sikukuu hiyo katika orodha ya sherehe za Kiislamu. Masuala mengi yanabaki kichwani bila ya majibu: ¡°Ni kwa sababu gani haswa Muislamu ashiriki sherehe hizo? Kwani Mola Mtukufu hakuwatunukia Waislamu siku zao za kusherehekea? Je, Mtume hakujua kwamba kitakuja kizazi ambacho hakitatofautisha Uislamu na Ukafiri?
Kutokana na ujinga wetu Waislamu ndio maana tunarushiwa mabomu kwenye ardhi zetu, tunaendelea kutawaliwa, kuteswa, kunyanyaswa na mengineyo. Hao wanaotutesa ndio tunaoshirikiana nao kwenye tafrija zao za uzushi. Hao wanaotutukana na kutukana dini yetu hata humu ndio eti tunashirikiana nao katika sherehe zao, Yote haya yanatokana na Waislamu kuacha kutambua kwamba Uislamu wao ni kamili, hautaki viraka wala kuengezewa matambara. Allaah (Subhaanahu wa Ta¯ala) Anasema:
{Leo Nimekukamilishieni Diyn yenu, na Nimekutimizieni neema Yangu, na Nimekupendeleeni Uislamu uwe ndiyo Diyn}[Suratul-Maaidah: 3]
Pia Qur-aan imeshakata kauli kwamba makafiri wana dini yao na sisi tuna Uislamu wetu. Yashangaza kuwaona Waislamu wakiwa hawaelewi ama wanajitia upofu wa mafundisho haya:
{{Sema: Enyi makafiri! Siabudu mnachokiabudu. Wala nyinyi hamuabudu ninayemuabudu. Wala sitaabudu mnachoabudu. Wala nyinyi hamuabudu ninayemuabudu. Nyinyi mna dini yenu, nami nina Diyn yangu.}}[Suratul-Kaafiruun: 1-6]
Kwa kuongezea, Mtume (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam) ametubainishia kwamba zama zetu zitakuwa zinachanganya mambo tukashindwa kuchambua baina ya haqq na baatwil. Hizi ndio zama za kukamata vyema Sunnah iliyoachwa na Mtume pamoja na kuachana na mambo yote yenye mashaka matupu:
((Mtafuata Sunnah (nyendo) za watu waliokuwa kabla yenu, kiganja kwa kiganja, mkono kwa mkono, hata wakiingia kwenye shimo la kenge mtawafuata)). Tukasema: Ewe Mjumbe wa Allaah, 'Je, Unamaanisha Mayahudi na Manaswara?' Akasema: ((Kwani nani zaidi ya wao?)).
Kwa upande wa Maswahaabah, tunamkuta Amiyr wa Waumini Sayyidna Umar bin Al-Khatwaab akitwambia:"Jiepusheni na maadui wa Allaah katika sherehe zao"
Ni vyema pia kunukuu maneno ya Mwanachuoni mcha Mungu, Mujaahid Shaykhul Islaam Ibn Taymiyyah:"Sisi Waislamu tusifanye jambo lolote lilokuwa si la kawaida katika siku hizi. Iwe kama siku yoyote nyingine katika maisha yetu bila ya kuwa imekhusishwa na lolotekamamfano wao watu wa Vitabu walivyokuwa hawasherehekei wala kuzifanya siku zetu za 'Iyd kuwa ni khaswa (maalum) kwao."
Ya Allaah tunakuomba kutokana na Nuru ya Wajihi wako, ambayo inaangazia mbingu na inaondoa kiza na kutawala mambo yote ya dunia na Akhera ili hasira Yako isitufikie au ghadhabu Yako isituangukie; utuongoze katika njia iliyonyooka na utusamehe madhambi yetu. Kwa hakika tunakiri kwamba hakuna mamlaka wala nguvu na uwezo ila Wako peke Yako.
 
M MA nyoko hatujitengi ng'o wanangu wakina idd mufti puza shekh abeid hareed wanakuja maana krismas tulipiga msos na kesho ni bia mchana kutwa M Ma make huyo mwana habari Ni mngese
 
Mkuu Chamviga nimekusoma baereze baelewe bamutu ya Tanganyika.
 
Kuna watu wanasema uislamu na dini nyingine ni sawa tu kwahyo twaweza shirikiana hata kwenye mambo ya ibada kama haya ya sikukuu. Basi kwa wale wanaosema kwamba Uislamu upo sawa na dini nyengine, haswa zile zinazosemwa kuwa ni dini za Kitabu, kama vile Uyahudi na Ukristo, hao wamekwenda kombo na wala hawaelewi misingi ya Uislamu. Kwani hata huo Uyahudi na Unaswara unaofuatwa leo, hauna uhusiano sahihi na hivyo Vitabu Alivyovishusha Mola wetu (Subhaanahu wa Ta¡¯ala). Sasa ni wapi tena tunataka kuwabebesha watoto wetu elimu ya Yesu aliyevumbuliwa na Ukristo hali ya kuwa Uislamu unayo mafundisho yake sahihi ya Nabii Iysa bin Maryam (Alayhis Salaam)?
Mola wetu Amesema:
{Bila shaka Diyn (ya haki) mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu. Na waliopewa Kitabu (Mayahudi na Manaswara) hawakukhitalifiana ila baada ya kuwajia ilimu.}[Al-Imraan: 19]
Na Akasema pia:
{{Na anayetaka dini isiyokuwa ya Kiislamu basi haitakubaliwa kwake. Naye Akhera atakuwa katika wenye khasara (kubwa kabisa).} [Al-Imraan: 85]
Kwa hivyo, tuelewe Waislamu kwamba, iwapo tumeukubali Uislamu kuwa ni Diyn yetu, basi hayo hapo juu ndio mafunzo sahihi, wala Mola wetu hajatutaka tuchanganye imani zetu zilizo safi dhidi ya imani za kikafiri. Na kwa hakika Uislamu wetu unatufunza kutochanganya ukafiri na Uislamu:
{{Sema: Enyi makafiri. Siabudu munachoabudu. Wala nyinyi hamuabudu ninayemuabudu. Wala sitaabudu munachoabudu. Wala nyinyi hamutaabudu ninayemuabudu. Nyinyi muna dini yenu nami nina Diyn yangu.}}[Al-Kaafiruun: 1-6]
Yapo mambo ambayo kweli tunaweza kushirikiana na makafiri, kama vile elimu sahihi za dunia kwa mfano utabibu na ufundi; lakini abadan sio ndani ya misingi ya Kiislamu hadi kufikia binti wa Kiislamu kutoona tofauti baina ya kuvaa ama kutovaa hijaab.
Tumche Mola wetu (Subhaanahu wa Ta¡¯ala), na tumuabudu Yeye kama Alivyotuamuru bila ya kumshirikisha. Tunamuomba Mola wetu Atuongoze katika njia sahihi na Atukhitimishe kwa kauli ya haki iliyothibiti.
 
wakristo msianze uchoyo kuwanyima waislamu kuchinja ili muwape shingo za kuku. tuache uchoyo.

ha ha ha umenikumbusha mbali sana nilikuaga napenda kula shingo ya kuku basi nilikua namaind akija kuchinja muislam home maana nilikua najua shingo ya kuku sitokula mimi atapewa mchinjaji.
 
Hii inanikumbusha maneno ya Mwalimu Julius K. Nyerere, tuna maadui watatu Ujinga, Umasikini na maradhi. Kwa hiyo ukiona ukisikia mtu anawagawa watanzania kwa namna yeyote ile bila shaka hayo mambo matatu anahusika nayo.
 
Mkuu Chamviga nimekusoma baereze baelewe bamutu ya Tanganyika.

Hawa jamaa zetu wanadhania wanaweza kutuburuza watakavyo. Nadhani wakati huo umeshapita. Huu ni muda wa kubainisha haki na uovu bila kupepesa macho.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom