Waislamu wapigwa marufuku kushiriki pasaka

Waislamu wapigwa marufuku kushiriki pasaka

Status
Not open for further replies.
Hakunaaa! Mi mwislam ila nasubili midaa ya kesho nipige kipunga, dini nazo ukiendekeza utakosa mengi,

Karibu jirani tusherehekee pamoja! baba na mama Hassan wanasubiri hiyo kesho kwa hamu! Pia Malik naye amesema atakuwapo!
 
ufinyo wa kufikiri mangapi wanafanya haramu liwe kula pilau kwa wakristo..... naaamini hata waabudu miti wanajua umuhimu wa upendo ..... kukosa hoja za msingi imekuwa tatizo kubwa vichwani mwa watu wengi...... kwa mtazamo wangu naona hii hoja nyepesi sana....
 
hawa viumbe sijui wapewe nini katika dunia hii..

mbona hata wao kwa wao hawaishi kwa usawa basi tuone mifano hai??

let them go, let them go!
 
Yan baada ya kusisitiza umoja na mshikamano,mnataka kutugawa watz.Waambieni walowatuma mtangaze hivo wamefeli.Waislamu wa tz na wakristo tunafahamu athari za ubaguzi wa kidini,mshindwe na mlegee watz tuna macho na masikio ya kuona na kusikia yanaendelea kule afrika ya kati,naigeria,na kwengineko dunian,taifa letu alijajengwa juu ya mising ya uchochez,ningekuwa mkuu wa tume ya wanatoa vibal vya matangazo ya radio,ningedhibitsha kama haya mmetamka kwel endapo ikiwa kwel,NINGEWAMBIA MUWAOMBE RADH WATZ THEN WIK MOJA YA KUTOSIKIKA HEWANI INGEWAHUSU ili iwe fundisho kwa vyombo vyote vya habar visipomima habar zake kabla ya kuzirusha hewani.
 
Kwanza nakutoa makosa, inapokuja neno Mwenyezi Mungu huwa (SWT) na sio (SAW).

SWT ni kifupi cha Subhana Wa Taala.

Ama SAW hiyo ni kwa ajili ya Mtume Muhammad tu, na kirefu chake ni Salallahu Aleyhi Wasalm,

Kwa hapo natumai umeelewa.

Ama kuhusu Muisilamu kusherehekea sikukuu za Kikristo au Wakristo kusherehekea za Waisilamu watu hufanya kwa mazowea tu na kama ile sikukuu sio ya dini yake basi huwa ni kama sherehe tu haifanyi kiimani, yaani huwa haimo moyoni mwake. í-¼í½Œ

sasa anamkasirisha vipi mungu wake wakati kitu chenyewe hakipo moyoni mwake au ikiwa kitu chenyewe hakifanyi kwa imani
 
Mambo ya Lukuvi hayo. Ngoja tumhoji Lukuvi analipi la kusema kuhusu hilo.


Sent from my iPad using JamiiForums
 
magaidi hao huwa hatuwashangai..hicho kituo cha redio ni cha magaidi

Waislamu kote nchini wamepigwa marufuku kushiriki sikukuu za kikristo kwa kuwa ni haramu kwa waislamu. Marufuku hiyo imetolewa leo kupitia Radio Imaan FM inayomilikiwa na kuendeshwa na waislamu. Mambo ambayo wamezuiwa kushiriki ni kula na kuvaa vizuri, kutoka na kujitembeza barabarani au kushiriki mialiko yoyote kutoka kwa wakristo kwani kufanya hivyo watakuwa wanamuudhi Mwenyezi Mungu SAW na ni kwenda kinyume na mafundisho ya kiislamu.

MAONI YANGU:
Siku zote wakristo na waislamu tumekuwa tukishiriki pamoja kusherekea sikukuu za pasaka, krismas, eid el fitr, eid el haj, nk bila ubaguzi wowote. Ni vigumu kuwazuia, hasa watoto, wasivae nguo mpya au kudoea pilau kwa jirani zao wakristu kwani sote tumaishi pamoja kwa upendo bila kubaguana.

Aidha kuna waislamu wengi wengi wamesoma na bado wanaendelea kusoma katika shule za kikristo (seminaries). Je, ina maana hawa nao wanafanya kitendo haramu au uharamu upo kwenye sherehe tu?

Tujadiliane hoja hii bila jazba yoyote ya udini. Mungu wabariki waislamu na wakristo.
 
Mbona binti ISSA kanambia nisipotoka naye out kesho na mba yake nifute na mapenzi yaishe!

Nimekula sana pilau la idd el fitri la washkaji,Kesho nitawaalika na watakuja.
 
Hakunaaa! Mi mwislam ila nasubili midaa ya kesho nipige kipunga, dini nazo ukiendekeza utakosa mengi,

Kweli ni kuupiga mpunga kwa kwenda mbele kwani hapo mwanzo kabla hawajaja hawa wazungu na warabu mungu tulimuomba kwa njia gani? Na baada ya kuja mbona tulikuwa pamoja maitubabaishe hapa. Mnataka kutugombanisha sisi ni ndugu maana ndani ya familia kuna ukristo na uislamu
 
Kweli ni kuupiga mpunga kwa kwenda mbele kwani hapo mwanzo kabla hawajaja hawa wazungu na warabu mungu tulimuomba kwa njia gani? Na baada ya kuja mbona tulikuwa pamoja maitubabaishe hapa. Mnataka kutugombanisha sisi ni ndugu maana ndani ya familia kuna ukristo na uislamu

mtaani kwetu tunaishi kiushirika bhana asikwambie mtu kesho nitakula hata zaid ya wenyewe maana mahotpot huwa yanatua home kutoka kila pande za majirani,
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom