Waislamu wapigwa marufuku kushiriki pasaka

Waislamu wapigwa marufuku kushiriki pasaka

Status
Not open for further replies.
Mi mwenyewe jirani yngu muislam na anakuja kunichinjia,redio imani hawawezi kututenganisha wanajisumbua,only majuha ndio watawasikiliza na c wny akili timamu
 
Mungu kasema "Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa" Kwa kweli kuna siku nimeisikiliza hii redio niliishia kushangaa tu jinsi tunavyohamasishwa kugombana wenyewe
 
Yanayoendelea Africa ya Kati yalianza hivi hivi
 
Kama ni kurejea mafundisho ya dini na vitabu vitakatifu yaani biblia hata Wakristi wanaelezwa dini nyingine kama Uislamu ni Ushetani na Ubatili.
Mashirikiano wakati wa sherehe ni mazoea tu baina ya majirani;ndugu,wengine wamechanganyika,marafiki makazini au mashuleni n.k.Si kwamba eti Wakristo wanawahitaji sana Waislamu ili kukamilisha sherehe zao.Huu ni ulimbukeni tu wa watu wasio na hoja.Mbona kauli hii haikutolewa wakati wa sherehe za Idd kuwazuia Waislam wasichanganyike na Wakristo?.
Suala la kupigwa mabomu?.Hivi Iraq washia na Wasunni wanaopigana kuna mkristo?.Somalia vita ilikuwepo dhidi ya Siad Barre bila mkristo kuhusika kabisa.
Watu wanahalalisha kuua wenzao kwa kupandikiza chuki bandia kwa kutumia dini tu!!!
 
Kwani wasiposhiriki wakristu wanapungukiwa nini?
Hizo roho za kimaskini eti msivae vizuri ni juha tu atasikiliza hayo machukizo.

Na hii inaonyesha kwamba Mungu wa watu wote sio mungu wa waaislam

Mungu ni mwenye Upendo si mwenye visazi.

Ukitajiwa dini huwa unakuwa kama immature fulani hivi, jirekebishe!!!!!!!
 
Sina uhakika kama hiyo redio wamesema kama mleta mada anavyodai, labda kweli na pia inawezekana mleta mada kapindisha maneno ili kuleta mfarakano, hasa kwa wale wasiotaka kushughulisha akili zao.

Mimi ni muislamu, kuna jiranizangu wakristu wamenikaribisha j.pili niende kwao. Si mara ya kwanza huwa ni kawaida yetu X.mass, Pasaka mimi huenda kwao tunakula pamoja. Idd nawakaribisha nao wanakuja familia nzima wanakula na kufurahi pamoja na familia yangu.

Bado sijaona aya inayokataza kula chakula kwa mkriso
sijaona aya inayokataza kuwa siku fulani usivae nguo nzuri.

Wanaotaka tusishirikiane katika furaha au misiba washindwe na walaaniwe.
 
Ni vigumu kutengana na jamaa zangu kisa Imani, kwanza Tumetoka mbali halafu Imani haijawai kuwa kikwazo kwetu.

Redio Imaani mtawashawishi hao hao wenye upeo mdogo kama nyie wenyewe.
 
Tuheshimu imani za watu wengine, Mimi mkristo ,siyo tu MkRisto lakini lutherani ,siyo tu Mlutheri lakini Mlokole !!!!!!!!!!!!!?!!!!!!!!!!----!imani yangu ni ;wokovu ulokole' siwezi kuwadharau waalimu wangu wa darasa la kwanza kiroho kwa kuwa
tu leo Mimi nipo chuo kikuu ,Hivyo
Hivyo, kiimani redio Imani iko sahihi lakini kidini hawapo sahihi ,,Tuheshimu imani za watu wengine
Dini yeyOte inaweza kuupuzwa ,lakini siyo IMANl ili mradi haindoi uhai na utu
wako au mwenzako

Bwana Yesu Kristo asifiwe sana!!!!!!!!P
 
Waislamu kote nchini wamepigwa marufuku kushiriki sikukuu za kikristo kwa kuwa ni haramu kwa waislamu. Marufuku hiyo imetolewa leo kupitia Radio Imaan FM inayomilikiwa na kuendeshwa na waislamu. Mambo ambayo wamezuiwa kushiriki ni kula na kuvaa vizuri, kutoka na kujitembeza barabarani au kushiriki mialiko yoyote kutoka kwa wakristo kwani kufanya hivyo watakuwa wanamuudhi Mwenyezi Mungu SAW na ni kwenda kinyume na mafundisho ya kiislamu.

MAONI YANGU:
Siku zote wakristo na waislamu tumekuwa tukishiriki pamoja kusherekea sikukuu za pasaka, krismas, eid el fitr, eid el haj, nk bila ubaguzi wowote. Ni vigumu kuwazuia, hasa watoto, wasivae nguo mpya au kudoea pilau kwa jirani zao wakristu kwani sote tumaishi pamoja kwa upendo bila kubaguana.

Aidha kuna waislamu wengi wengi wamesoma na bado wanaendelea kusoma katika shule za kikristo (seminaries). Je, ina maana hawa nao wanafanya kitendo haramu au uharamu upo kwenye sherehe tu?

Tujadiliane hoja hii bila jazba yoyote ya udini. Mungu wabariki waislamu na wakristo.

hawa jamaa mungu wao ni wa ajabu sana.huwa simuelewi kabisa.
 
Tuheshimu imani xza watu wengine Mimi mkristo lakini lutherani lakini imani yangu ni "wokovu ulokole'"siwezi kuwadharau waalimu wa darasa la kwanza kwa kuwa
tu leo chuo kikuu ,Hivyo 1
Hivyo kiimani ya korani redio iko sahihi la lakini kidini hawapo sahihi ,,Tuheshimu imani za watu wengine
Dini yeyOte inaweza kuupuzwa ,lakini siyo IMANl

Bwana Yesu Kristo asifiwe sana!!!!!!!!

hahaha hii kitu inanifurahisha sana.yaani maisha tunayoishi juku uswahilini cjui tu.mbona hiyo kesho huyo mungu wao atanuna mpaka basi....tunavyojijua sisi mitoto ya uswaz kwenye wali mchafu....hahaha
 
m ma nyoko hatujitengi ng'o wanangu wakina idd mufti puza shekh abeid hareed wanakuja maana krismas tulipiga msos na kesho ni bia mchana kutwa m ma make huyo mwana habari ni mngese

we mpare mbona unatukana sasa?
 
Kuna watu wanasema uislamu na dini nyingine ni sawa tu kwahyo twaweza shirikiana hata kwenye mambo ya ibada kama haya ya sikukuu. Basi kwa wale wanaosema kwamba Uislamu upo sawa na dini nyengine, haswa zile zinazosemwa kuwa ni dini za Kitabu, kama vile Uyahudi na Ukristo, hao wamekwenda kombo na wala hawaelewi misingi ya Uislamu. Kwani hata huo Uyahudi na Unaswara unaofuatwa leo, hauna uhusiano sahihi na hivyo Vitabu Alivyovishusha Mola wetu (Subhaanahu wa Ta¡¯ala). Sasa ni wapi tena tunataka kuwabebesha watoto wetu elimu ya Yesu aliyevumbuliwa na Ukristo hali ya kuwa Uislamu unayo mafundisho yake sahihi ya Nabii Iysa bin Maryam (Alayhis Salaam)?
Mola wetu Amesema:
{Bila shaka Diyn (ya haki) mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu. Na waliopewa Kitabu (Mayahudi na Manaswara) hawakukhitalifiana ila baada ya kuwajia ilimu.}[Al-Imraan: 19]
Na Akasema pia:
{{Na anayetaka dini isiyokuwa ya Kiislamu basi haitakubaliwa kwake. Naye Akhera atakuwa katika wenye khasara (kubwa kabisa).} [Al-Imraan: 85]
Kwa hivyo, tuelewe Waislamu kwamba, iwapo tumeukubali Uislamu kuwa ni Diyn yetu, basi hayo hapo juu ndio mafunzo sahihi, wala Mola wetu hajatutaka tuchanganye imani zetu zilizo safi dhidi ya imani za kikafiri. Na kwa hakika Uislamu wetu unatufunza kutochanganya ukafiri na Uislamu:
{{Sema: Enyi makafiri. Siabudu munachoabudu. Wala nyinyi hamuabudu ninayemuabudu. Wala sitaabudu munachoabudu. Wala nyinyi hamutaabudu ninayemuabudu. Nyinyi muna dini yenu nami nina Diyn yangu.}}[Al-Kaafiruun: 1-6]
Yapo mambo ambayo kweli tunaweza kushirikiana na makafiri, kama vile elimu sahihi za dunia kwa mfano utabibu na ufundi; lakini abadan sio ndani ya misingi ya Kiislamu hadi kufikia binti wa Kiislamu kutoona tofauti baina ya kuvaa ama kutovaa hijaab.
Tumche Mola wetu (Subhaanahu wa Ta¡¯ala), na tumuabudu Yeye kama Alivyotuamuru bila ya kumshirikisha. Tunamuomba Mola wetu Atuongoze katika njia sahihi na Atukhitimishe kwa kauli ya haki iliyothibiti.
sheikh chamviga nataka kurithi mabikira 72 nipe aya..na hamu nao sana
 
Wewe kiumbe na wenzako wenye mawazo mgando hebu eleweni kuwa Pasaka, christmas n.k ni sherehe zinazoambatana na imani za watu. Tumeambiwa tushirikiane lakini si mpaka katika ibada. Uislamu ndio unakataza na sio radio iman wala shekh flani. Ni Amri ya Allah subhanahu wataala. Pungezeni kelele zenu kwakuwa hazitomzuia tembo kunywa maji. Ngoja waislamu waelimishwa na waijue dini yao waache kufuata mambo yenye kuwatia katika madhambi. Sio Qur-aan, Hadith, wala waja wema wote (Maswahaabah, wafuasi wa maswahaba, wafuasi wa wafuasi wa maswahaba), wala Ma¡¯ulaamaa wa Kiislamu waliohalalisha kujumuika na makafiri kwenye sherehe zao za Kikafiri.
Miongoni mwa sherehe ambazo zinafurahikiwa mno na Waislamu ni Mwaka Mpya wa Kikiristo ingawa haimo sikukuu hiyo katika orodha ya sherehe za Kiislamu. Masuala mengi yanabaki kichwani bila ya majibu: ¡°Ni kwa sababu gani haswa Muislamu ashiriki sherehe hizo? Kwani Mola Mtukufu hakuwatunukia Waislamu siku zao za kusherehekea? Je, Mtume hakujua kwamba kitakuja kizazi ambacho hakitatofautisha Uislamu na Ukafiri?
Kutokana na ujinga wetu Waislamu ndio maana tunarushiwa mabomu kwenye ardhi zetu, tunaendelea kutawaliwa, kuteswa, kunyanyaswa na mengineyo. Hao wanaotutesa ndio tunaoshirikiana nao kwenye tafrija zao za uzushi. Hao wanaotutukana na kutukana dini yetu hata humu ndio eti tunashirikiana nao katika sherehe zao, Yote haya yanatokana na Waislamu kuacha kutambua kwamba Uislamu wao ni kamili, hautaki viraka wala kuengezewa matambara. Allaah (Subhaanahu wa Ta¯ala) Anasema:
{Leo Nimekukamilishieni Diyn yenu, na Nimekutimizieni neema Yangu, na Nimekupendeleeni Uislamu uwe ndiyo Diyn}[Suratul-Maaidah: 3]
Pia Qur-aan imeshakata kauli kwamba makafiri wana dini yao na sisi tuna Uislamu wetu. Yashangaza kuwaona Waislamu wakiwa hawaelewi ama wanajitia upofu wa mafundisho haya:
{{Sema: Enyi makafiri! Siabudu mnachokiabudu. Wala nyinyi hamuabudu ninayemuabudu. Wala sitaabudu mnachoabudu. Wala nyinyi hamuabudu ninayemuabudu. Nyinyi mna dini yenu, nami nina Diyn yangu.}}[Suratul-Kaafiruun: 1-6]
Kwa kuongezea, Mtume (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam) ametubainishia kwamba zama zetu zitakuwa zinachanganya mambo tukashindwa kuchambua baina ya haqq na baatwil. Hizi ndio zama za kukamata vyema Sunnah iliyoachwa na Mtume pamoja na kuachana na mambo yote yenye mashaka matupu:
((Mtafuata Sunnah (nyendo) za watu waliokuwa kabla yenu, kiganja kwa kiganja, mkono kwa mkono, hata wakiingia kwenye shimo la kenge mtawafuata)). Tukasema: Ewe Mjumbe wa Allaah, 'Je, Unamaanisha Mayahudi na Manaswara?' Akasema: ((Kwani nani zaidi ya wao?)).
Kwa upande wa Maswahaabah, tunamkuta Amiyr wa Waumini Sayyidna Umar bin Al-Khatwaab akitwambia:"Jiepusheni na maadui wa Allaah katika sherehe zao"
Ni vyema pia kunukuu maneno ya Mwanachuoni mcha Mungu, Mujaahid Shaykhul Islaam Ibn Taymiyyah:"Sisi Waislamu tusifanye jambo lolote lilokuwa si la kawaida katika siku hizi. Iwe kama siku yoyote nyingine katika maisha yetu bila ya kuwa imekhusishwa na lolotekamamfano wao watu wa Vitabu walivyokuwa hawasherehekei wala kuzifanya siku zetu za 'Iyd kuwa ni khaswa (maalum) kwao."
Ya Allaah tunakuomba kutokana na Nuru ya Wajihi wako, ambayo inaangazia mbingu na inaondoa kiza na kutawala mambo yote ya dunia na Akhera ili hasira Yako isitufikie au ghadhabu Yako isituangukie; utuongoze katika njia iliyonyooka na utusamehe madhambi yetu. Kwa hakika tunakiri kwamba hakuna mamlaka wala nguvu na uwezo ila Wako peke Yako.


Maasha Allah,swadakta wajazakallahu khair!
 
Waache uchonganishi sasa..Mimi Fatuma wangu anakuja kesho yupo njiani kuja kula pasaka ya bwana alafu wanaanza matangazo ya ajabu ajabu bwana mambo gani haya..karibuni ndugu zangu waislamu wote tusherekee sikukuu ya bwana!
 
kwa vile umetaka tusitumie Jazba...ni vizuri na wewe ukawa katika hali ya kutofungamana na dini ya upande wowote......Sawa tuendelee.....

Kikawaida kaka yangu katika Uislam kila kitiu ni Ibada....Kula ni Ibada na mtu analipwa(Thawabu) kama atakula chumo lake la halali...akianza kusema Bismilahi Rahmani Rahiim....akila na kunywa kwa mkono wa kulia....na kesema Alhamdulillah baada ya kumaliza kula...

Kumuingilia mkeo katika Uislam pia ni Ibada...kama mtaoga mtatia udhu na mtaanza kupigana miti kwa kupiga Bismilahi..na inakua Vizuri kama utasoma dua hii....."Allahuma Jannibna Mina shaitwaani Wajannibnaa maarazaqtanaaa"....Mola wetu tunajilinda na shetani na pia tunamlinda na shetani mtoto wetu kama utatupa mtoto katika kungiliana kwetu huku....

Hata Kwenda chooni katika Uislam ni Ibada na Allah anatulipa thawabu kama tutaingia Chooni kwa mguu wa kushoto na kutoka kwa kwa mguu wa kulia....pia utalipwa zaidi kama utasoma Dua hii..."Allahuma Aundhu bika mina Khubuth wal-khabaaith" Ewe mola wangu mlezi nnajilinda kwako na Majini Makhabithi ya kiume yanayokaa chooni na majini ya Kike yanayokaa chooni" ukitoka chooni pia kuna dua yake...unaweza kusoma dua Ewe Mola wangu nakushuru kwa kuniondolea yale yaliokua yakinuudhi katika mwili wangu na kunibakishia yanayonifurahisha"....

Kiufupi Uislam ulivvyo ni mfumo mzima wa Maisha ya Bidadamu...Na nafikiri ndio maana walimwengu wanauogopa kufuatwa...

Tuje kwenye madaa kuu....X-mass ni siku kuu inayotoka na kuzaliwa na Mungu wa kikiristo...Yesu...kwetu sisi waislam Yesu si Mungu na wala si mtoto wa Mungu...kwa hio hatuwezi kushereheka kwa misingi hio.....historia pia inasema kua Yesu mwenyewe hakuzaliwa December...ni mambo yalio tengenezwa tu......

Tuje kwenye Pasaka.....Pasaka ni siku kuu ya miungu ya Kisanamu ya Uzazi na Tendo la ndoa ambalo wajanja waliibadilisha ikawa ni kufa na kufufuka kwa Yesu.....https://www.facebook.com/photo.php?...05998019.26164.1765009520&type=1......Wengine wanasema Pasaka ni sherehe inayotokana na wanaoabudia Jua...kwa sababu siku ya Easter Monday ndio siku ambayo Jua huchomoka kwenye uso wa dunia kutoka katikati ya Mashariki(Exactly East)....naifikiri tunaweza kuufanya utafiti huu kesho kutwa Jumaa tatu.....kwa hio Redio Imaan wako sahihi kukataza waislam kuabudia Miungu ya Kishirikina kama hii.....na mambo mengine ya Kipumbavu kama Valentine day....nk.
 
Ji puuze mwenyewe na sio. Redio hatuipuuz hata kidogo nyie mna mungu wenu na sie tuna mungu wetu faten yenu na sie tufate yetu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom