Waislamu wapigwa marufuku kushiriki pasaka

Waislamu wapigwa marufuku kushiriki pasaka

Status
Not open for further replies.

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
27,567
Reaction score
28,730
Waislamu kote nchini wamepigwa marufuku kushiriki sikukuu za kikristo kwa kuwa ni haramu kwa waislamu. Marufuku hiyo imetolewa leo kupitia Radio Imaan FM inayomilikiwa na kuendeshwa na waislamu. Mambo ambayo wamezuiwa kushiriki ni kula na kuvaa vizuri, kutoka na kujitembeza barabarani au kushiriki mialiko yoyote kutoka kwa wakristo kwani kufanya hivyo watakuwa wanamuudhi Mwenyezi Mungu SAW na ni kwenda kinyume na mafundisho ya kiislamu.

MAONI YANGU:
Siku zote wakristo na waislamu tumekuwa tukishiriki pamoja kusherekea sikukuu za pasaka, krismas, eid el fitr, eid el haj, nk bila ubaguzi wowote. Ni vigumu kuwazuia, hasa watoto, wasivae nguo mpya au kudoea pilau kwa jirani zao wakristu kwani sote tumaishi pamoja kwa upendo bila kubaguana.

Aidha kuna waislamu wengi wengi wamesoma na bado wanaendelea kusoma katika shule za kikristo (seminaries). Je, ina maana hawa nao wanafanya kitendo haramu au uharamu upo kwenye sherehe tu?

Tujadiliane hoja hii bila jazba yoyote ya udini. Mungu wabariki waislamu na wakristo.
 
Roho mbaya imejaa baadhi ya watu wachache wenye upeo wa kufikiri
 
Hiyo redio Iman sio redio ya waislam bali ni redio ya walioianzisha. Haiwezi kuwa sauti au kauli ya waislam. Wapuuzwe.
 
Kwani wasiposhiriki wakristu wanapungukiwa nini?
Hizo roho za kimaskini eti msivae vizuri ni juha tu atasikiliza hayo machukizo.

Na hii inaonyesha kwamba Mungu wa watu wote sio mungu wa waaislam

Mungu ni mwenye Upendo si mwenye visazi.
 
na hata wakienda sokoni waulize huyo aliyelima nyanya au carots au vitunguu kama alikuwa muislamu ili wasije wakamuudhi mwenyezi mungu, wakimaliza huko, wakitaka kupanda basi kusafir pia waulize, na madukani kabla ya kununua kitu pia waulize!
 
Kuna watu wafukunyuku, huu unaitwa uchochezi, kila mtu na imani yake, sasa usiingilie imani ya wenzio. Wao wakifunga ramadhani unawasaidiaga? Eid unashiriki nao?. Kwani wasiposhiriki pasaka unapungukiwa nini? Acha uchochezi.
 
Na jumatatu ta pasaka isiwe mapumziko kwao.
 
Kwanza nakutoa makosa, inapokuja neno Mwenyezi Mungu huwa (SWT) na sio (SAW).

SWT ni kifupi cha Subhana Wa Taala.

Ama SAW hiyo ni kwa ajili ya Mtume Muhammad tu, na kirefu chake ni Salallahu Aleyhi Wasalm,

Kwa hapo natumai umeelewa.

Ama kuhusu Muisilamu kusherehekea sikukuu za Kikristo au Wakristo kusherehekea za Waisilamu watu hufanya kwa mazowea tu na kama ile sikukuu sio ya dini yake basi huwa ni kama sherehe tu haifanyi kiimani, yaani huwa haimo moyoni mwake. 🍌
 
Kwanza nakutoa makosa, inapokuja neno Mwenyezi Mungu huwa (SWT) na sio (SAW).

SWT ni kifupi cha Subhana Wa Taala.

Ama SAW hiyo ni kwa ajili ya Mtume Muhammad tu, na kirefu chake ni Salallahu Aleyhi Wasalm,

Kwa hapo natumai umeelewa.

Ama kuhusu Muisilamu kusherehekea sikukuu za Kikristo au Wakristo kusherehekea za Waisilamu watu hufanya kwa mazowea tu na kama ile sikukuu sio ya dini yake basi huwa ni kama sherehe tu haifanyi kiimani, yaani huwa haimo moyoni mwake. ?

Swadakta, umenena vema kwa kutoa elimu kwa wasioelewa. Binafsi tayari nimealikwa kesho kwa mnuso na nitawachinjia.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom