Waislam nijibuni hili

Waislam nijibuni hili

Labda pengine Gharama za msikiti ni ndogo kuliko za shule. Msikiti unajengwa Kama hall tu, tofauti na madarasa au hospital ambayo ukiacha majengo, yatahitaji nguvu kazi (employees) na vifaa pia.

Lakini tukiweka Gharama kando, hoja yako ina matiki kiasi. Kuna wanaosema kua Waarabu walileta utumwa na dini wakati wazungu walileta shule na dini Ndio Sababu mavyuoni (kisha maofisini) wakristo ni wengi kuliko waislam. Ili kutatua hii tofauti waislam tugejikita zaidi kwenye shule pia.
Hata gharama ya hospitali ikiwa ndogo mara mia kuliko ya msikiti, katika sehemu yenye misikiti mia na isiyo na hospitali.

Mtu akiamua, kwa hela zake, kujenga msikiti wa mia moja na moja, wakati hajaamua kujenga hospitali. Ni haki yake.

Ukiona kakosea. Usimseme.

Tafuta hela yako, jenga hospitali.

Onesha kakosea kwa matendo. Kwa hela yako.

Usimpangie mtu cha kufanya kwa hela yake mwenyewe.

Kwa sababu, hata wewe unayeona hospitali ni muhimu kuliko msikiti sehemu hiyo, ukiamua kujenga hospitali, kwa hela yako, halafu mtu mwingine akakupangia ujenge msikiti, kitu unachoona hakihitajiki na si matakwa yako, hutafurahi.

Kila mtu ajenge anachotaka, kwa hela yake, bila kubugudhiwa.

Kama unaona shule ni muhimu, hujakatazwa kujenga shule. Jenga.

Kama unaona hospitali ni muhimu, hujakatazwa kujenga hospitali. Jenga.

Kama unaona msikiti ni muhimu, hujakatazwa, jenga.

Kama unaona kanisa ni muhimu, hujakatazwa, jenga.

Hata ukitaka kujengea spaceship la kwenda sayari nyingine, jenga.

Sasa ya nini kumshupalia mtu anayetumia hela yake kujenga anachotaka yeye?

Unajuaje hiyo shule au hospitali ni muhimu kwake?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata gharama ya hospitali ikiwa ndogo mara mia kuliko ya msikiti, katika sehemu yenye misikiti mia na isiyo na hospitali.

Mtu akiamua, kwa hela zake, kujenga msikiti wa mia moja na moja, wakati hajaamua kujenga hospitali. Ni haki yake.

Ukiona kakosea. Usimseme.

Tafuta hela yako, jenga hospitali.

Onesha kakosea kwa matendo. Kwa hela yako.

Usimpangie mtu cha kufanya kwa hela yake mwenyewe.

Kwa sababu, hata wewe unayeona hospitali ni muhimu kuliko msikiti sehemu hiyo, ukiamua kujenga hospitali, kwa hela yako, halafu mtu mwingine akakupangia ujenge msikiti, kitu unachoona hakihitajiki na si matakwa yako, hutafurahi.

Kila mtu ajenge anachotaka, kwa hela yake, bila kubugudhiwa.

Kama unaona shuke muhimu, hujakatazwa kujenga shule. Jenga.

Kama unaona hospitali ni muhimu, hujakatazwa kujenga hispitali. Jenga.

Kama unaona msikiti ni muhimu, hujakatazwa, jenga.

Kama unaona kanisa ni muhimu, hujakatazwa, jenga.

Hata ukitaka kujengea spaceship la kwenda sayari nyingine jenga.

Sasa ya nini kumshupalia mtu anayetumia hela yake kujenga anachotaka yeye?

Unajuaje hiyo shule au hospitali ni muhimu kwake?

Sent using Jamii Forums mobile app
Haya
 
Hamna cha amali. Mtu ajenge misikiti hata kujaza dunia lakini akawa na mambo ya ajabu ajabu adhabu yake iko pale pale.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe ndie unaehukumu au yupo anaehukumu?
Je unaijua nafsi ya mtu ? Je kama atatubia?
Mbona nyie mnakwenda kutubu kila jumapili?
Mnasema yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zenu iweje bado mna dhambi?

Cᵃʳᵉᵉᵐ ᵀʰᵉ ᴸᵉᵍᵉⁿD
 
Moja ya sababu kubwa ya umasikini ni tabia ya kupenda wengine wakufanyie unachotaka wewe bila ya wewe mwenyewe kufanya hicho specific unachotaka kifanyike.

Tabia hii inaendana na kutaka watu wengine watumie hela zao kufanya unachotaka wewe kifanyike. Kama kumtaka mtu baki ajenge shule au hospitali unayotaka wewe, badala ya msikiti anaotaka yeye.

Ni umasikini wa mawazo, ni ufukara wa fikira, ni kilema cha akili.

Action speaks louder than words.

Show. Don't tell.

When you have to shoot, shoot. Don't talk.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Indonesia ndio nchi yenye idadi kubwa ya waislamu duniani,kuna vita?au Brunei amani IPO au haipo, nchi ambayo serikali yake ni tajiri inamlipia kila mwanaume safari ya kwenda hijja.uwe una acha kudanganya hadharani.
Acha Ujinga huko unakosema ni Mashariki ya kati???Elewa nimesema Mashariki ya kati nakupa tena nafasi taja nchi yoyote ya Mashariki yenye amani kama Tanzania!!!!
 
Nadhani wengi wakikuelewa vizuri hii ndo ingekua conclusion. Hizi dini tumeletewa tukazikumbatia. Waliotuletea wakatuacha tunazihusudu na kupigana kwa sababu ya hizo dini, wao wakaendelea kusogea mbele (Tumekua kama mmbwa aliyetupiwa mfupa akabaki ameng'ang'ana nao mwizi akaendelea kuiba.

Ndugu zangu waislamu acheni kufuata msichojua kikoje. Walioleta uislamu kwenye nchi zao wanafanya biashara kubwa kubwa na kujenga viwanda kila kukicha. Huku mmeaminishwa kujikita kwenye elim akhera na kusababisha wengi kukosa ufaham wa dunia inavyokwenda.

C kwenu tu. Hata kwa wakristo tunaibiwa sana kwa sababu tu ya kukosa kunyenyekea dini huku ukweli ukiwa unajulikana.

Fungukeni wapendwa. Achaneni na mapokeo. Najua yapo yenye maana ila inabidi kufungua akili ili uweze kuyachuja
Nimepitia karibu comment zote zilizotangulia humu

Nilichogundua waTanzania wengi hatupendi kujifunza na kuchukua hatua

Mimi ni Mkristo ila sio kila kitu kwenye ukristo nakiamini! Na hii ni baada ya kujifunza baadhi ya vitu nikiwa na "open mind"! Unajifunza kitu pasipo kufungwa na hisia au kushikilia ulichokwisha aminishwa!

Mfano, mpaka leo kuna watu wanabandika picha za yule mzungu aliyeigiza picha ya Yesu kwamba ndio Yesu Mwenyewe! Na huwaambii chochote wakakuelewa maana hata baadhi ya vitu vya dini vina picha yake! (Angalau siku hizi waandishi wengi hawaitumii)

Mpaka leo kuna watu ukiwaambia padri fulani amezaa na mwanamke fulani watatamani kukupiga mawe! Hawaamini kitu kama hicho! Wanasahau kwamba sote ni binadamu!

Na hayo ni madhara ya mapokeo ya hizi dini! Tuliaminishwa sana vitu visivyo na uhalisia!

Kwa mfano, wenzetu waislam wanaamini ukitoa Swadaka ya kujenga Msikiti wewe tayari umeshaiona pepo! Yaani kwa Swadaka ya Msikiti tayari umetengeneza njia ya kufika peponi bila kujalisha Maisha yako mengine yakoje!

Kuna vitu hutakiwi kuvimeza kama vilivyo! Kuna vingine unatakiwa utafune, tena vingine utafune kwa uangalifu maana vinaweza kuwa na vipande vya mawe ukatakiwa uteme!

Kwa mfano, Mimi nilishawahi kuhoji! Ukiangalia mitaani hasa Morogoro mjini karibu kila mtaa kuna msikiti na pengine mtaana mmoja kuna misikiti hadi mitatu!

Ukiangalia sio kwamba huwa inajaa yote na wala sio kwamba iko mbali mbali kiasi cha kusema watachelewa wale wanaoswali swala tano! Jibu ni Hapana! Ipo karibu karibu tu!

Cha zaidi utakuta kila Msikiti una jina lake! Huu Msikiti wa fulani na ule Msikiti wa fulani.

Halafu mtaa huo huo utakuta hamna hata zahanati. Wote wakipata shida utakuta wanakutanikia zahadi moja kiasi cha kukaa foleni kwa muda mrefu na kupoteza muda mwingi wa kufanya shughuli nyingine.

Ukienda shule ya msingi au sekondari iliyopo ndani ya kata husika (ambamo kuna misikiti kibao) utakunana na shule moja, yenye upungufu mkubwa wa madarasa, yenye mrundikano mkubwa wa wanafunzi wasio na madawati ya kukalia kitu kinachopelekea ufaulu hafifu!

Unakutana na shule inazaidi ya miaka mitano wahitimu wake hakuna aliyewahi kupata division one na wanaopata division two ni kuanzia watatu hadi watano Kati ya wahitimu zaidi ha 150!

Mbaya zaidi wakishatoka hapo, hakuna hata vyuo vya ufundi watakavyokutana navyo huko msikitini!

Ni kweli kabisa serikali haijengi misikiti wala makanisa hivyo ni jukumu la waumini kujenga nyumba zao za ibada. Lakini hili haliwanyimi fursa waumini hao hao kujenga shule, vyuo, hospital kwa ajili ya maendeleo ya waumini wao na jamii nzima kwa ujumla

Tanzania kuna madhehebu mengi sana, lakini yenye waumini wengi nadhani ni mawili! Uislam na Ukatoliki

Hawa maana yake wanawaumini wengi. Kwa maana nyingine hata huko mashuleni kuna waumini wao wengi. Hospital kuna waumini wao wengi wanaenda kutibiwa huko

Kuna shida gani mtaa ukiwa na Msikiti mmoja halafu badala ya kuongeza misikiti mingine miwili (ambapo sio kwamba huo wa kwanza unajaa) wakajenga shule au zahanati?

Tunaaminishwa kwamba mambo ya Imani za watu sio vizuri kuyahoji, lakini hii sioni kama ni sahihi kwasababu walio kuja na hizi dini ndio hao hao wanatukazania tuache kuhoji hoji baadhi ya mambo.

Mwenyezi Mungu anatupenda sana, ametupa akili ili tuzitumie. Hakuna mipaka ya kuhoji kwasababu anayehoji anatafuta maarifa au majibu ya kutatua tatizo fulani

Wao walipokuja huku walihoji Imani za Babu zetu wakaziita Imani potofu! Kwanini sisi tuamini tu wao wako sahihi kwenye kila jambo? Inamaana wao walipewa akili nyingi kuliko sisi? Hii sio sahihi! Kuna vitu vingi tu wanataka tuvitimize kwa kigezo cha Imani za dini za kutohoji baadhi ya mambo

Kwamba ukijenga shule au hospital wakatumia wote wenye dini na wasio na dini peponi panakuwa mbali!?

Kwamba kukikwa na Msikiti kila baada ya mita kumi ndio kumfarahisha Mungu wakati jamii hiyo hiyo yenye Msikiti kila baada ya mita kumi kuna janga la umasikini, watu wake wakiumwa watahitaji kutembea zaidi ya kilometa kadhaa kufuata huduma na watalazimika kuisubiria kwa masaa kadhaa.

Watu hao hao watoto wao hawana shule za chekechea, wana shule moja ya msingi mkondo mmoja wanafunzi 100 na robo tatu wanakaa chini

Watu hao hao wanashule moja ya sekondari ya kata yenye uhaba mkubwa wa madawati, matundu ya vyoo hayatoshi, hakuna maji, mkondo mmoja wanakaa wanafunzi zaidi ya 90 !

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Punguza jazba muelewe alichosema kwa jicho la tatu. Kuna waislamu baadhi wanalalamika juu ya mfumo kristo kwamba unetawala tanzania viongozi wengi wa serikali ni wakristo hata teuzi za raisi nyingi ni wakristo sababu ndio hiyo aliyoitoa jamaa kuwa waislamu tupo bize na madrasa na misikiti bila kujenga shule na vyuo,hatukatai tusijenge misikiti lkn tukumbuke na shule na vyuo.

Vitu wanavyomiliki wakristo Tanzania ni St.thomas St mary st joseph chuo SAUT mwanza ruvuma mtwara st john dodomast francis chuo cha tumaini iringa st agnes chipole na kadha wa kadha.Haya tuje waislamu tuna mabasi yaendayo mikoani abood mashalah tawfiq pia tuna wasanii diamond kiba konde boy tid mnyama chid benz fid q msodoki mzee wa bwax manfongo shilole msaga sumu dulla makabila mo dweji azam bakharesa na nk.kwahiyo wao wanamiliki elimu sisi tunamiliki biashara na wasanii wavuta bangi.ndio mana wakristo wanatutawala kwa hiyo jamaa yupo sahihi kabisa inabidi tuamke tuanze kujenga shule zaidi vyuo vingi zaidi hii misikiti inatosha sasa.
KCMC Hospital na nyingine nyingi.

Mueleweshe huyu ndugu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa nn wasikupe msaada wa shule, kiwanda, hospitali, n.k. Kwa nn misikiti tu. Utasema kukujenge misikiti wanajenga akhera yao. Sawa

Sasa, kwa nn wasijenge kule kwao wewe wakusukumie kuabudu wao wajivutie biashara na maendeleo.

Funguka akili
Nahisi una uvimbe kichwani. Hayo ya kwao lakini misaada wanayotoa inalenga kujenga akhera zao. Una jipya?!

Cᵃʳᵉᵉᵐ ᵀʰᵉ ᴸᵉᵍᵉⁿD

Sent using Jamii Forums mobile app
 
USSR,

Mkuu tahariri yako yaonyesha unawatakia mema sana waislam. Hongera, basi tuishauri serikali ya ciciem, au chama chcht kinachotaka maendeleo ya watanzania wakiwemo waislam.

1. Kuondoa sheria kandamizi zinazowazuia waislam kuendeshea miradi yao ya maendeleo. Na sheria moja wapo ni ya ugaidi. Sheria hii imekuwa kikwazo kwa taasisi nyingi za kiislam kukosa misaada. Kwa kile kinachosemwa pesa hizo zitawafanya waislam wawe magaidi.

Mfano wa taasisi hizo ni al haramin tanga, na dhynurain iringa. Taasisi hizi zimetenzwa nguvu kutokana na jitihada zao za elimu na afya. Mfano dhynuran kila walipojenga msikiti waliweka kituo cha afya. Huko tanga taasisi ya al haramain ilijikita kutoa elimu bure, hii ndio hali ya taasisi nyingi za kiislam kuminywa na kutopewa ruhusa ya kupata misaada ya maendeleo.

Pia kuna hali ya viongizi wa bakwata kulazimishwa waombe kujengewa msikiti badala ya mahitaji mengine. Haya tunayaona wanapokuja viongozi kutokana nchi za kiislam duniani.

2. Serikali itoe ajira kwa alimu wa dini na yatambulike kwa ajili ya maadili mema mbadala ya kununua magari ya gharama kubwa kwa ajili ya wanasiasa

3. Serikali iajiri wahudumu wa afya na madakatri kwa hospitali zinazoendeshwa na taasisi za dini badala ya kununua ndege ambazo zinaendeshwa kwa hasara na 99% ya wanyonge hawafaidiki nazo.

4. Waislam wenyewe wajivue ktk ufinyu wa fikra kuwa mambo yanayohusu dini ni Yale yanayojulikana ni ya kiroho tu. Huu ni ufinyu wa fikra. Na ni Ushindi ambao wameupata wapinzani wa Uislam. . Wapinzani wa Vitabu Vitukufu vilivyotangulia walifaulu kufanya hila ya kuvitia mikono na kuviharibu Vitabu hivyo.
Lakini Wapinzani wa Quran wameshindwa katika jitihada zao za kuipotosha Quran. Hata hivyo, wamepata ushindi wa kuifungia Quran ndani ya wigo wa kitawa ambamo kila msomaji wa Quran ameondoka katika lengo lake la mwongozo wa maisha ya kila siku huku akiridhika kuwa anasoma Quran kwa wingi ktk kujenga misikiti kwa ajili ya kuswalia, kufunga nk

Laiti waislam ungefungamana na lengo lilelile lililoifikisha na Mtume (saw) na Maswahaba katika kilele cha mafanikio ya kijamii, kisiasa, kiutamaduni, kitabia, kidiplomasia, basi uilsma ungeonekana kuwa ni mfumo kimbilio la wanadamu.

Leo waislam tumeyaacha mafundisho usahihi kuwa uislam unafungamana na matendo yote kwa ajili ya manufaa ya miwili yetu na matendo kwa ajili ya manufaa ya roho zetu. Na hivyo turudi kwenye uislam kamili kwa kujenga na kusimamia vyote,, msikiti, Madrasa, shule, hospitali, nk
Tatzo mnaoelewa haya mambo ni wachache sana. Wengi wamebase kwenye isue ya KUTENGENEZA AKHERA. Waneshindwa kuwa na ufahamu ulio nao wewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa nn wasikupe msaada wa shule, kiwanda, hospitali, n.k. Kwa nn misikiti tu. Utasema kukujenge misikiti wanajenga akhera yao. Sawa

Sasa, kwa nn wasijenge kule kwao wewe wakusukumie kuabudu wao wajivutie biashara na maendeleo.

Funguka akili

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani hasa nyie mnawashwa na nini sisi tukijengewa miskiti?? Si muwaambie na nyie watu wenu wawajengee makanisa!

Cᵃʳᵉᵉᵐ ᵀʰᵉ ᴸᵉᵍᵉⁿD
 
Kwani hasa nyie mnawashwa na nini sisi tukijengewa miskiti?? Si muwaambie na nyie watu wenu wawajengee makanisa!

Cᵃʳᵉᵉᵐ ᵀʰᵉ ᴸᵉᵍᵉⁿD
Mtu baki anaposhindwa kufanya unachoona kinatakiwa kufanyika, kitu cha maana kabisa hapo ni wewe unayeona hajafanya kinachotakiwa kufanyika ukifanye, halafu yeye aone kwa mfano.

Sio kuleta maneno mengi hajafanya hiki au kile.

Ukileta maneno sana hapo utaonekana inawezekana una propaganda zako na ajenda binafsi ambayo huisemi.

Wanaoona kuna haja ya shule kujengwa, wajenge shule. Hawajakatazwa.

Wanaoona kuna haja ya hospitali kujengwa, wajenge hospitali. Hawajakatazwa.

Wanaoona kuna haja ya misikiti kujengwa, wajenge misikiti. Hawajakatazwa.

Wanaotaka kuchezea kamari hela zao, wachezee kamari, hawajakatazwa.

Ili mradi wanatumia hela zao na hawamuingilii mtu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Punguza jazba muelewe alichosema kwa jicho la tatu. Kuna waislamu baadhi wanalalamika juu ya mfumo kristo kwamba unetawala tanzania viongozi wengi wa serikali ni wakristo hata teuzi za raisi nyingi ni wakristo sababu ndio hiyo aliyoitoa jamaa kuwa waislamu tupo bize na madrasa na misikiti bila kujenga shule na vyuo,hatukatai tusijenge misikiti lkn tukumbuke na shule na vyuo.

Vitu wanavyomiliki wakristo Tanzania ni St.thomas St mary st joseph chuo SAUT mwanza ruvuma mtwara st john dodomast francis chuo cha tumaini iringa st agnes chipole na kadha wa kadha.Haya tuje waislamu tuna mabasi yaendayo mikoani abood mashalah tawfiq pia tuna wasanii diamond kiba konde boy tid mnyama chid benz fid q msodoki mzee wa bwax manfongo shilole msaga sumu dulla makabila mo dweji azam bakharesa na nk.kwahiyo wao wanamiliki elimu sisi tunamiliki biashara na wasanii wavuta bangi.ndio mana wakristo wanatutawala kwa hiyo jamaa yupo sahihi kabisa inabidi tuamke tuanze kujenga shule zaidi vyuo vingi zaidi hii misikiti inatosha sasa.
Tatizo hata mkijenga shule
Au vyuo hamjengi vya elimu ya kawaida...kwa shule utakuta shule inakuwa maarufu kwaajili ya elimu ya dini na maadili au kubanwa kwa wanafunzi wala sio ufaulu...na upande wa vyuo vingi utakuta vyuo vya dini,,,hii inapelekea hata wazazi kutopeleka watoto wao kwa wingi huko...
Hili nalo linahitaji marekebisho
Maendeleo hayana dini
 
Punguza jazba muelewe alichosema kwa jicho la tatu. Kuna waislamu baadhi wanalalamika juu ya mfumo kristo kwamba unetawala tanzania viongozi wengi wa serikali ni wakristo hata teuzi za raisi nyingi ni wakristo sababu ndio hiyo aliyoitoa jamaa kuwa waislamu tupo bize na madrasa na misikiti bila kujenga shule na vyuo,hatukatai tusijenge misikiti lkn tukumbuke na shule na vyuo.

Vitu wanavyomiliki wakristo Tanzania ni St.thomas St mary st joseph chuo SAUT mwanza ruvuma mtwara st john dodomast francis chuo cha tumaini iringa st agnes chipole na kadha wa kadha.Haya tuje waislamu tuna mabasi yaendayo mikoani abood mashalah tawfiq pia tuna wasanii diamond kiba konde boy tid mnyama chid benz fid q msodoki mzee wa bwax manfongo shilole msaga sumu dulla makabila mo dweji azam bakharesa na nk.kwahiyo wao wanamiliki elimu sisi tunamiliki biashara na wasanii wavuta bangi.ndio mana wakristo wanatutawala kwa hiyo jamaa yupo sahihi kabisa inabidi tuamke tuanze kujenga shule zaidi vyuo vingi zaidi hii misikiti inatosha sasa.
Wanaolalamika waache walalamike.

Kulalamika ni sehemu ya haki za kikatiba za Watanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
USSR,

Mkuu tahariri yako yaonyesha unawatakia mema sana waislam. Hongera, basi tuishauri serikali ya ciciem, au chama chcht kinachotaka maendeleo ya watanzania wakiwemo waislam.

1. Kuondoa sheria kandamizi zinazowazuia waislam kuendeshea miradi yao ya maendeleo. Na sheria moja wapo ni ya ugaidi. Sheria hii imekuwa kikwazo kwa taasisi nyingi za kiislam kukosa misaada. Kwa kile kinachosemwa pesa hizo zitawafanya waislam wawe magaidi.

Mfano wa taasisi hizo ni al haramin tanga, na dhynurain iringa. Taasisi hizi zimetenzwa nguvu kutokana na jitihada zao za elimu na afya. Mfano dhynuran kila walipojenga msikiti waliweka kituo cha afya. Huko tanga taasisi ya al haramain ilijikita kutoa elimu bure, hii ndio hali ya taasisi nyingi za kiislam kuminywa na kutopewa ruhusa ya kupata misaada ya maendeleo.

Pia kuna hali ya viongizi wa bakwata kulazimishwa waombe kujengewa msikiti badala ya mahitaji mengine. Haya tunayaona wanapokuja viongozi kutokana nchi za kiislam duniani.

2. Serikali itoe ajira kwa alimu wa dini na yatambulike kwa ajili ya maadili mema mbadala ya kununua magari ya gharama kubwa kwa ajili ya wanasiasa

3. Serikali iajiri wahudumu wa afya na madakatri kwa hospitali zinazoendeshwa na taasisi za dini badala ya kununua ndege ambazo zinaendeshwa kwa hasara na 99% ya wanyonge hawafaidiki nazo.

4. Waislam wenyewe wajivue ktk ufinyu wa fikra kuwa mambo yanayohusu dini ni Yale yanayojulikana ni ya kiroho tu. Huu ni ufinyu wa fikra. Na ni Ushindi ambao wameupata wapinzani wa Uislam. . Wapinzani wa Vitabu Vitukufu vilivyotangulia walifaulu kufanya hila ya kuvitia mikono na kuviharibu Vitabu hivyo.
Lakini Wapinzani wa Quran wameshindwa katika jitihada zao za kuipotosha Quran. Hata hivyo, wamepata ushindi wa kuifungia Quran ndani ya wigo wa kitawa ambamo kila msomaji wa Quran ameondoka katika lengo lake la mwongozo wa maisha ya kila siku huku akiridhika kuwa anasoma Quran kwa wingi ktk kujenga misikiti kwa ajili ya kuswalia, kufunga nk

Laiti waislam ungefungamana na lengo lilelile lililoifikisha na Mtume (saw) na Maswahaba katika kilele cha mafanikio ya kijamii, kisiasa, kiutamaduni, kitabia, kidiplomasia, basi uilsma ungeonekana kuwa ni mfumo kimbilio la wanadamu.

Leo waislam tumeyaacha mafundisho usahihi kuwa uislam unafungamana na matendo yote kwa ajili ya manufaa ya miwili yetu na matendo kwa ajili ya manufaa ya roho zetu. Na hivyo turudi kwenye uislam kamili kwa kujenga na kusimamia vyote,, msikiti, Madrasa, shule, hospitali, nk
Muhammad alianzisha shule au hospitali???
Uislam haukukua kwa diplomacy ndugu bali fuatilia historia ya vita vya Ridda
 
Back
Top Bottom