Waislam nijibuni hili

Katika duara, nyuzi 0 na 360 kwa kuangalia haraka ni kama sehemu ile ile.

Sasa tazama vizuri, usije ukaona nyuzi 0, wakati hesabu ni nyuzi 360.

Sin (0*) = Sin (360*).

Cos (0*) = Cos (360*)

Tan (0*) = Tan (360*)

Don't get it twisted.

Kiranga is a singularity you don't have the math to unravel.

Sent using Jamii Forums mobile app
aisee.
 
Siku ingine summarize...tuna familia za kuhudumia sio muda ote tunasoma article Jf...
1.Muhammad anabrandiwa kuwa the greatest diplomat lakin ebu fikiria mecca ilavamiwa na waquraysh wakanyanganywa mji wao kwa upanga kwa msemo 'silimu au lipa jizya'...hiyo ni diplomasia???
2.Hapa actually nlikuwa naongelea kipindi cha Muhammad lakini wewe umebase Kwenye "golden age"..... I'm not going to argue about this my friend but keep in mind hakuna dini duniani yenye propaganda nyingi za kujisifu kama uislam
Kipindi hicho unachozungunzia kilikuwa ni baada ya mtume kufariki. Kipindi cha uhai wa mtume kulikuwa na mikataba ya ujirani mwema kati ya waislam, mayahudi na makuraish. Baada ya kufa mtume, kulitokea uasi. Waasisi wakitaka kuiteka madina. Na ikatokea vita. Baada ya waasi kushinfwa vita wakapewa masharti hayo, musilimu au muishi chini ya dola ya kiislam kwa kulipia zakka ili mupate ulinzi dhidi ya maadui wengine.

Pitia hapa

Mkuu, shukrani sana kwa huu uzi, umeandika ukweli ulio wazi..

Matatizo mkubwa ya Waislam hasa hawa wa Tanzania ni ukosefu wa kujua DINI yao..

Waislam wanaamini kuwa kujenga Misikiti ni sadaka kubwa sana ambayo itakulinda siku ya Mwisho uko akhera..

Wasichokijua au wanalijua lakini kutokana a upeo mdogo wa elimu ya dini yao kuwa hata ukijenga SHULE , HOSPITALI , VIWANJA VYA KUCHEZEA WATOTO, NYUMBA ZA YATIMA, VYUO VIKUU nk, vita kulinda vile vile siku ya mwisho uko Akhera..

Uislam unaamini Ibada ni kufanya mambo mzuri kwako wewe au kwa Jamii...

mfano umeona kipande cha KIGAE kipo njiani, ukakiondoa KIGAE kile na kikiweka pembeni au kukitupa kwenye debe la taka ili watu wasidhurike iyo nayo Ibada, na unapata dhawabu kwa hilo..

Ukenda nchi za waislam wanaojua dini yao mambo hayako kama hapa kwetu, Misikiti ni sehemu ya kuabudu lakini kuna kuwa na Vyuo Vikuu, na harakati nyengine katika sehemu husika..
 
Jordan,UAE,Oman zinatosha..umeonyesha ujinga wako kwa kuitolea somalia mfano na yenyewe iko mashariki ya kati?Ila hizo nchi nilizozitaja mwanzo zimekuumiza roho pole sana bwana mdogo!!!
Kati ya nchi zote za mashariki ya kati zenye Amani ni nchi tatu?hapo ndipo utasemakuna Amani??Somalia nilisema kati ya nchi zenye vurugu!!Lakini kwa sababu akili yako imeshikwa utaendelea kubisha!!
 
Bandiko lako limeegemea sana kwenye wivu au chuki juu ya imani flani,lakini je kweli kwamba hakuna waislam ambao wametoa vitu au misaada mbalimbali ya kusaidia jamii? jibu bila shaka litakuwa ni ndio,je hawa hukuwaona? mwisho kwenye kutoa zawadi au msaada mwenye kutoa ndiye huchagua atoa nn na kwa sababu gani.kwa hiyo waache watoe kila ambacho wao wanadhani kitakuwa na maana kwao na jamii inayowazunguka
Nafikiri umemsoma vibaya huyu jamaa, kaka kama wewe ni Muislam unatakiwa ujue kuwa Uislam sio kujenga Misikiti tu..

Uislam ni mfumo wa maisha, kama maisha yako na ya mtoto wako pamoja na familia yako hayako katika mazingira mzuri basi ujue hata huo Uislamu utauona shubiri

Waislam tubadilike Dunia inatiacha, badala ya kujenga sehemu za IBADA, tujitahidi pia na kujenga VYUO VIKUU vyetu, HOSPITALI zetu nk..

Sadaka sio kujenga Misikiti tu..
 
imeandikwa katika Quran kwamba hapa duniani tukiondoka kitu pekee tutakacho kiacha na chenye manufaa baada ya kuondoka kwetu ni swadakatl_jaalia yaan sadaka yenye kuendelea. kwa mfano:
msikiti-watu wataendelea kusalia hata kama haupo
kisima-watu watakunywa na kutumia maji
mti wa matunda,
mtoto uliempa elimu ya dini, nk.

Hivyo watu wana chimba visima, kijenga misikiti, kupanda miti ya matunda, kununua vitabu vya dini(quran) jua sababu kuu ndo hyo hapo juu. Hasa zaidi ni maandalizi ya kesho baada ya kuachana na uhai wa dunia.

Natumai umenielewa. mengine wataongezea wadau.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wamiliki wa 'dini' wana akili sana!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kati ya nchi zote za mashariki ya kati zenye Amani ni nchi tatu?hapo ndipo utasemakuna Amani??Somalia nilisema kati ya nchi zenye vurugu!!Lakini kwa sababu akili yako imeshikwa utaendelea kubisha!!
Unachekesha kweli!! maana hata ulichouliza hukijui ulitoa hoja uthibitishiwe kama kuna nchi mashariki ya kati zina amani zimepatikana unaruka usemi wako!!!huna hoja•
 
Yaelekea unafatilia historia ya uislam, hongera. Ukiisoma historia ya Uislam, wakati wake Muhammad dini haikuwa haya mambo yanayofanywa Leo na waislam, waislam wa Leo wamekopi kutoka kwa ukristo wa kale kuwa dini ni na kufanya mambo ya ukasisi, ukuhani wala utawa pekee sawa na maandiko matakatifu ya biblia. Yaani unapoongelea kuhusu dini kwao ni mambo yanayohusu roho pekee, na kuwa kazi ya makasisi ni ushenga kati ya wanadamu na Mungu. Kwamba kazi ya makasisi ni kukuombea Ili Mungu akufutie dhambi na kukupa pepo. Na mashekhe nao wakaiga na wakajipa hadhi ya kujenga upatanushi kati ya mwanadamu na Mungu. Ni ajabu wenzetu wakristo na hasa wakatoliki Sijui wanafata maandiko gn yanayowahimiza kujenga shule na mahospitali sasa. Kazi hii ilipaswa kufanya na waislam. Na ndio maana tukifatilia historia kuna kipimdi kilichojulikana kama the Golden's age of Islam. Ambapo mambo ya yote ya maelndeleo ulimwenguni waliongzwa na waislam.

Hata hivyo vyeo vya ushekhe havikuwapo wakati wa mtume. Asili ya neno sheikh limeibuka miaka 150 iliyopita linatokana na neno la kigiriki senex likiwa ma maana Mbunge.

Historia inatueleza kuwa wakati wa mtume dini ilifahamika kama ni mfumo kamili wa maisha ya mwanadamu. Na kiongozi wa dini hakuwa na kazi ya kuwaombea dua viongozi wengine wa kisiasa au wagonjwa. Bali Kiongozi wa dini alikuwa ndie mtawala. Kwa hivyo dini ilikuwa na maana ya mfumo kamili wa maisha ya mwanadamu ambapo uligusa kila kipengele cha maisha. Uchumi, utamaduni, utawala na idara zake, zikiwemo mambo ya elimu, afya nk. Haya yalifahamika kama mahitaji ya mwili ili uweze kutimiza mahitaji ya roho. Tofauti na sasa MTU anaweza kufanya ufisadi maofisini na akazichukua pesa zile kwa ajili ya kujenga nyumba ya ibada. Na kiongozi akazibariki pamija na kumpa pepo. Huu ni upuuzi kabisa. Binadamu anapaswa mwilini wake ufanye mambo mazuri yanayompendeza Mungu kwa ajili ya roho take baada ya kufa. Na sio kuchanganya hali na batili pamoja.

Hivyo mitume hawakuacha jambo lolote la kijamii kwa kuona haliwahusu. Na kwa vile alikuwa anatangaza ujumbe yoka kwa mungu Mara kadhaa aliwafanyia miujiza ili wapate kumuamini. Sasa nikirudi kwenye hoja zako. 1. Suala la dini na dipolmasia Muhammad (saw) alikuwa ni mwanadiplomasia aliyetukuka, fatilia mkataba wa kidiplomasia uliojulikana kama Sulhu ya Hudaibiya au Hudaibiya Treaty. Mkataba huu haukuwapendeza walio wengi ktk wafuasi wake wakiona wamedhalilika, kwa kuzuiliwa kuingia makka kwenda kufanya hija. Lkn mtume aliyakubali matakwa ya wasiokuwa waislam wa wakati ule na akaepusha vita. Na hicho kinachoitwa Ridda hakikuwapo wakati wa mtume.

2. Kuhusu kujenga hospitali au Universities. Msingi wa kwanza wa dini hii ni kusoma. Iqra, soma. Hivyo dini imetutaka tusome. Na haikusema kusoma nini, soma chcht kwa ajili ya Mungu.

Na Ipo hadithi mtume akisisitiza hilo kwa kuhimiza waislam wakatafute elimu haya ikiwa uchina, kuhusu hospitali wakati wa mtume hakukuwa na majengo mfano wa hospitali tulizonazo. Kipindi kile madakari ndio waliowafata wagonjwa majumbani kwao. Bali kulikuwa na hopstili mfano wa kambi za muda kwa magonjwa ya milipuko na kuambukiza. Ipo hadithi mtume anasema, Mungu hajaleta ugonjwa wowote isipokuwa una dawa. Hivyo utaona jinsi gani alivyohimiza kufanya tafiti juu ya tiba kutokana na magonjwa mbalimbali.

Hata hivyo mapinduzi makubwa ya tiba za kisasa ziligungulika kipindi kinavhofahamika kama muslim goldern age. Kipindi cha haroun rashid ktk dola ya Abbasid Caliph ambapo duniani kote walitegemea mambo ya kielimu ikiwepo tiba ktk jiji LA Baghdad.

Historia pia inaonyesha chuo kikuu cha kwanza kilipatikana Morocco University of Karueein na baadae Cairo, Azhar University. Wakati huo ulaya na hasa ugiriki kulikuwa na mfano wa hospital wakitibu kwa kutumia maombi.
Mgalatia hawezi kuelewa!!!
 
Akhy, naomba unifafanulie kuhusu hiyo asili ya neno "Sheikh" kama ulivyosema. Hiyo kauli uliyosema umeitoa wapi??

Halafu hapo kwenye hadith, hiyo hadith unaweza kuonesha sanad yake na kuniambia kaipokea nani? Je ni hadith sahih, hasan, dhaif au mawdhuu'?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nafikiri umemsoma vibaya huyu jamaa, kaka kama wewe ni Muislam unatakiwa ujue kuwa Uislam sio kujenga Misikiti tu..

Uislam ni mfumo wa maisha, kama maisha yako na ya mtoto wako pamoja na familia yako hayako katika mazingira mzuri basi ujue hata huo Uislamu utauona shubiri

Waislam tubadilike Dunia inatiacha, badala ya kujenga sehemu za IBADA, tujitahidi pia na kujenga VYUO VIKUU vyetu, HOSPITALI zetu nk..

Sadaka sio kujenga Misikiti tu..
Amri ya kwanza katika uislamu baada ya kuamini ni kusoma......hakuna anayepinga lakini huyu mtoa mada anaukashifu uislamu kwa maamuzi ya muislamu mmoja kuamua kujenga msikiti inakuwa ni tuhuma kwa waislamu wote hapo ndio inakuwa shida humu,huyu huyu aliyejenga msikiti akijenga shule au hospitali akaitoa kwa waislamu wAtakuja kulaumu tena mambo ya udini...hawa wagalatia sio wakuwaunga mkono hata siku moja.
 
Lakini wenzao wa Dubai, Saudia na Oman watu binafsi wanajenga mashule na mahospitali ya kisasa kila siku.
Nimepitia karibu comment zote zilizotangulia humu

Nilichogundua waTanzania wengi hatupendi kujifunza na kuchukua hatua

Mimi ni Mkristo ila sio kila kitu kwenye ukristo nakiamini! Na hii ni baada ya kujifunza baadhi ya vitu nikiwa na "open mind"! Unajifunza kitu pasipo kufungwa na hisia au kushikilia ulichokwisha aminishwa!

Mfano, mpaka leo kuna watu wanabandika picha za yule mzungu aliyeigiza picha ya Yesu kwamba ndio Yesu Mwenyewe! Na huwaambii chochote wakakuelewa maana hata baadhi ya vitu vya dini vina picha yake! (Angalau siku hizi waandishi wengi hawaitumii)

Mpaka leo kuna watu ukiwaambia padri fulani amezaa na mwanamke fulani watatamani kukupiga mawe! Hawaamini kitu kama hicho! Wanasahau kwamba sote ni binadamu!

Na hayo ni madhara ya mapokeo ya hizi dini! Tuliaminishwa sana vitu visivyo na uhalisia!

Kwa mfano, wenzetu waislam wanaamini ukitoa Swadaka ya kujenga Msikiti wewe tayari umeshaiona pepo! Yaani kwa Swadaka ya Msikiti tayari umetengeneza njia ya kufika peponi bila kujalisha Maisha yako mengine yakoje!

Kuna vitu hutakiwi kuvimeza kama vilivyo! Kuna vingine unatakiwa utafune, tena vingine utafune kwa uangalifu maana vinaweza kuwa na vipande vya mawe ukatakiwa uteme!

Kwa mfano, Mimi nilishawahi kuhoji! Ukiangalia mitaani hasa Morogoro mjini karibu kila mtaa kuna msikiti na pengine mtaana mmoja kuna misikiti hadi mitatu!

Ukiangalia sio kwamba huwa inajaa yote na wala sio kwamba iko mbali mbali kiasi cha kusema watachelewa wale wanaoswali swala tano! Jibu ni Hapana! Ipo karibu karibu tu!

Cha zaidi utakuta kila Msikiti una jina lake! Huu Msikiti wa fulani na ule Msikiti wa fulani.

Halafu mtaa huo huo utakuta hamna hata zahanati. Wote wakipata shida utakuta wanakutanikia zahadi moja kiasi cha kukaa foleni kwa muda mrefu na kupoteza muda mwingi wa kufanya shughuli nyingine.

Ukienda shule ya msingi au sekondari iliyopo ndani ya kata husika (ambamo kuna misikiti kibao) utakunana na shule moja, yenye upungufu mkubwa wa madarasa, yenye mrundikano mkubwa wa wanafunzi wasio na madawati ya kukalia kitu kinachopelekea ufaulu hafifu!

Unakutana na shule inazaidi ya miaka mitano wahitimu wake hakuna aliyewahi kupata division one na wanaopata division two ni kuanzia watatu hadi watano Kati ya wahitimu zaidi ha 150!

Mbaya zaidi wakishatoka hapo, hakuna hata vyuo vya ufundi watakavyokutana navyo huko msikitini!

Ni kweli kabisa serikali haijengi misikiti wala makanisa hivyo ni jukumu la waumini kujenga nyumba zao za ibada. Lakini hili haliwanyimi fursa waumini hao hao kujenga shule, vyuo, hospital kwa ajili ya maendeleo ya waumini wao na jamii nzima kwa ujumla

Tanzania kuna madhehebu mengi sana, lakini yenye waumini wengi nadhani ni mawili! Uislam na Ukatoliki

Hawa maana yake wanawaumini wengi. Kwa maana nyingine hata huko mashuleni kuna waumini wao wengi. Hospital kuna waumini wao wengi wanaenda kutibiwa huko

Kuna shida gani mtaa ukiwa na Msikiti mmoja halafu badala ya kuongeza misikiti mingine miwili (ambapo sio kwamba huo wa kwanza unajaa) wakajenga shule au zahanati?

Tunaaminishwa kwamba mambo ya Imani za watu sio vizuri kuyahoji, lakini hii sioni kama ni sahihi kwasababu walio kuja na hizi dini ndio hao hao wanatukazania tuache kuhoji hoji baadhi ya mambo.

Mwenyezi Mungu anatupenda sana, ametupa akili ili tuzitumie. Hakuna mipaka ya kuhoji kwasababu anayehoji anatafuta maarifa au majibu ya kutatua tatizo fulani

Wao walipokuja huku walihoji Imani za Babu zetu wakaziita Imani potofu! Kwanini sisi tuamini tu wao wako sahihi kwenye kila jambo? Inamaana wao walipewa akili nyingi kuliko sisi? Hii sio sahihi! Kuna vitu vingi tu wanataka tuvitimize kwa kigezo cha Imani za dini za kutohoji baadhi ya mambo

Kwamba ukijenga shule au hospital wakatumia wote wenye dini na wasio na dini peponi panakuwa mbali!?

Kwamba kukikwa na Msikiti kila baada ya mita kumi ndio kumfarahisha Mungu wakati jamii hiyo hiyo yenye Msikiti kila baada ya mita kumi kuna janga la umasikini, watu wake wakiumwa watahitaji kutembea zaidi ya kilometa kadhaa kufuata huduma na watalazimika kuisubiria kwa masaa kadhaa.

Watu hao hao watoto wao hawana shule za chekechea, wana shule moja ya msingi mkondo mmoja wanafunzi 100 na robo tatu wanakaa chini

Watu hao hao wanashule moja ya sekondari ya kata yenye uhaba mkubwa wa madawati, matundu ya vyoo hayatoshi, hakuna maji, mkondo mmoja wanakaa wanafunzi zaidi ya 90 !

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akhy, naomba unifafanulie kuhusu hiyo asili ya neno "Sheikh" kama ulivyosema. Hiyo kauli uliyosema umeitoa wapi??

Halafu hapo kwenye hadith, hiyo hadith unaweza kuonesha sanad yake na kuniambia kaipokea nani? Je ni hadith sahih, hasan, dhaif au mawdhuu'?

Sent using Jamii Forums mobile app

Akhy ukisoma historia ya Uislam (taarikh) wa Marne tatu bora za hatuoni neno Sheikh likitumika. Makhalifa wote waongofu hakuna aliyeitwa Sheikh.

Neno sheikh lilianza kutumia karne za hivi karibuni. Na ndio maana haya znz kiongozi wa serikali za mitaa wanaitwa Sheha, asili yake shekhe.

Unaweza kupitia hapa kwa ufafanuzi zaidi

Kuhusu sanadi ya hadhithi ya mtume; hadithi hiyo haina hadhi ya Sahihi, lkn bado inatazamwa kuwa Ni hadithi. Hata hivyo upon ushahidi mwengine juu ya kutafuta elimu; taarikh inasema moja ktk vita vilivyopiganwa wakati wa mtume na waislam wakashinda, mateka wa vita vile mtume (saw) aliamrisha wasiuwawe kama baadhi ya maswahaba walivyotaka. Bali mtume (SWA) aliamrisha wale mateka wa vita kuwa wangeweza kuachiwa huru kama wana elimu au ujuzi Fulani wangewafundisha Waislamu ujuzi waliona au kuwafundisha kujua kusoma na kuandika ndipo watawaachia. Na wasio na ujuzi walipe kikomboleo (fidia).
 
Amri ya kwanza katika uislamu baada ya kuamini ni kusoma......hakuna anayepinga lakini huyu mtoa mada anaukashifu uislamu kwa maamuzi ya muislamu mmoja kuamua kujenga msikiti inakuwa ni tuhuma kwa waislamu wote hapo ndio inakuwa shida humu,huyu huyu aliyejenga msikiti akijenga shule au hospitali akaitoa kwa waislamu wAtakuja kulaumu tena mambo ya udini...hawa wagalatia sio wakuwaunga mkono hata siku moja.
Kaka inabidi tumshukuru mtoa mada, bila shaka yeye sio Muislam, kwahiyo hivyo ndivyo anavyowaona Waislam, sioni kama kawakashifu au kuwa sema vibaya Waislam..

Mkuu, hapa kwetu Tanzania kuna tafauti kubwa ya yale yanayofanywa na Wakristo na wnayofanywa na Waislam katika jamaii..

Angalii hapo unapoishi Hospitali kubwa ni ya nani, Vyuo Vikuu ni vya akina nani, Waislam hatujui dini yetu ukweli ndio huo, inatakiwa tujitizame tumekosa wapi..

Ukisoma historia ya Uislam na mambo waliyofanya katika Dunia na vipi wamebadilisha Jamii tafauti duniani,..utaona UMUHIMU wa dini ya kiislam

Humu humu katika JF, kuna mada inayoeleza Kuwa IKULU ya Daresalam pamoja na hospital ya Ocean Road ilikuwa Madrasa kwa Waislam wa wakati huo, nyumba hiyo ilikuwa inaitwa "Daru Salam" yenye maana "nyumba ya salama"..

Daru Salam ilikuwa kama unavyoiona sasa ilikuwa imezungukwa na nyuma za wageni, sehemu ya kusali(misikiti), sehemu ya kusoma madrasa nk
.
Waliojenga hiyo sehemu walikuwa wanajua nini maana ya SADAKA, walikuwa wanajua Sadaka ya kukusaidia siku ya mwisho sio kujenga misikiti tu, bahati mbaya au nzuri Waliojenga walikuwa sio WAAFRIKA walikuwa WARABU, hapo ndio utajiuliza sisi Waafrika tunakosea wapi?? Au Uislam wetu tafauti na watu wengine??

Lazima tujirekebishe au Dunia itatuacha, Akhera tutajibu maswali mengi kwa Mungu wetu.. Tafakari
 
Akhy ukisoma historia ya Uislam (taarikh) wa Marne tatu bora za hatuoni neno Sheikh likitumika. Makhalifa wote waongofu hakuna aliyeitwa Sheikh.

Neno sheikh lilianza kutumia karne za hivi karibuni. Na ndio maana haya znz kiongozi wa serikali za mitaa wanaitwa Sheha, asili yake shekhe.

Unaweza kupitia hapa kwa ufafanuzi zaidi

Kuhusu sanadi ya hadhithi ya mtume; hadithi hiyo haina hadhi ya Sahihi, lkn bado inatazamwa kuwa Ni hadithi. Hata hivyo upon ushahidi mwengine juu ya kutafuta elimu; taarikh inasema moja ktk vita vilivyopiganwa wakati wa mtume na waislam wakashinda, mateka wa vita vile mtume (saw) aliamrisha wasiuwawe kama baadhi ya maswahaba walivyotaka. Bali mtume (SWA) aliamrisha wale mateka wa vita kuwa wangeweza kuachiwa huru kama wana elimu au ujuzi Fulani wangewafundisha Waislamu ujuzi waliona au kuwafundisha kujua kusoma na kuandika ndipo watawaachia. Na wasio na ujuzi walipe kikomboleo (fidia).
Shukran sana Akhy. Ila hili la matumizi ya neno "Shaikh" nitalifuatilia zaidi nijue kwa hoja na dalili za kielimu. Hayo maelezo ya kwenye hiyo website bado hayajaniridhisha vizuri naona tu kwa kiasi kikubwa yametarjumiwa kutoka Wikipedia.

Vile vile mara nyingi watu wanapoinukuu hiyo "hadith" ya kutafuta elimu mpaka China wanainukuu wengi wao bila ya kujua ni mawdhuu. Na cha kusikitisha imekuwa maarufu mpaka watu wengine wengi huitumia sana kama hoja na hata kuichukulia kama hadith sahih.

Pia tunapotaka kuonesha umuhimu wa elimu katika Uislam ni bora zaidi tutumie hadith sahih na hasan kuliko kuzitanguliza hadith dhaif wakati sahih na hasan zipo na zinatosha kuonesha umuhimu wa elimu katika Uislam.

Ila shukran sana Akhy.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shukran sana Akhy. Ila hili la matumizi ya neno "Shaikh" nitalifuatilia zaidi nijue kwa hoja na dalili za kielimu. Hayo maelezo ya kwenye hiyo website bado hayajaniridhisha vizuri naona tu kwa kiasi kikubwa yametarjumiwa kutoka Wikipedia.

Vile vile mara nyingi watu wanapoinukuu hiyo "hadith" ya kutafuta elimu mpaka China huwa hawaibainishi kuwa ni dhaif. Hii huwafanya watu wengine wengi kuitumia sana kama hoja na hata kuichukulia kama hadith sahih.

Pia tunapotaka kuonesha umuhimu wa elimu katika Uislam ni bora zaidi tutumie hadith sahih na hassan kuliko kuzitanguliza hadith dhaif wakati sahih na hassan zipo na zinatosha kuonesha umuhimu wa elimu katika Uislam.

Ila shukran sana Akhy.

Sent using Jamii Forums mobile app

Shukran Akhy. Inshallah jikinaishe kwa kufatilia taarikh ya neno Sheikh. Na ikiwezekana utuletee mrejesho inshallah.
 
6. Hizo Zahanati ziwe nyingi kiasi hicho zipate kuwatibu maradhi ya zinaa na blood.poisoning related to alcoholism?
Hapa napo weye umeharibu points zako. Mbona humo humo misikitini wanaingia waliotoka kufanya uchafu nao wanajifariji kuwa wesha koga na sasa wana tawadha tu waingie kuswali?? Hatuwaziki kwa vifo vya magonjwa hayo hayo ya zinaa??
Point ya mleta hoja ni kuwa; Je, ni lazima tujenge msikiti?? Kwa nini nisinunue vitabu vya dini nikavimwaga penye ule msikiti?? Weka Kuruani za kumwaga hapo watu waji sevie wenyewe ili kila nyumba ipate kitabu hicho kitakatifu. Mwaga Juzuu za kutosha na vitabu vingi vya dini ambavyo watu wengi hawana uwezo wa kuvinunua. Vigawe bure ili watu waisome dini yetu waielewe. Fadhili mihadhara ielezee dini yetu, Misikiti mingi mitaani sio kuwafanya watu kusilimu.
 
Kaka inabidi tumshukuru mtoa mada, bila shaka yeye sio Muislam, kwahiyo hivyo ndivyo anavyowaona Waislam, sioni kama kawakashifu au kuwa sema vibaya Waislam..

Mkuu, hapa kwetu Tanzania kuna tafauti kubwa ya yale yanayofanywa na Wakristo na wnayofanywa na Waislam katika jamaii..

Angalii hapo unapoishi Hospitali kubwa ni ya nani, Vyuo Vikuu ni vya akina nani, Waislam hatujui dini yetu ukweli ndio huo, inatakiwa tujitizame tumekosa wapi..

Ukisoma historia ya Uislam na mambo waliyofanya katika Dunia na vipi wamebadilisha Jamii tafauti duniani,..utaona UMUHIMU wa dini ya kiislam

Humu humu katika JF, kuna mada inayoeleza Kuwa IKULU ya Daresalam pamoja na hospital ya Ocean Road ilikuwa Madrasa kwa Waislam wa wakati huo, nyumba hiyo ilikuwa inaitwa "Daru Salam" yenye maana "nyumba ya salama"..

Daru Salam ilikuwa kama unavyoiona sasa ilikuwa imezungukwa na nyuma za wageni, sehemu ya kusali(misikiti), sehemu ya kusoma madrasa nk
.
Waliojenga hiyo sehemu walikuwa wanajua nini maana ya SADAKA, walikuwa wanajua Sadaka ya kukusaidia siku ya mwisho sio kujenga misikiti tu, bahati mbaya au nzuri Waliojenga walikuwa sio WAAFRIKA walikuwa WARABU, hapo ndio utajiuliza sisi Waafrika tunakosea wapi?? Au Uislam wetu tafauti na watu wengine??

Lazima tujirekebishe au Dunia itatuacha, Akhera tutajibu maswali mengi kwa Mungu wetu.. Tafakari
Mtoa mada siyo muislamu,kwa hiyo hakuna jema hata moja anautakia uislamu,Labda ungesema wewe tungekuunga mkono na so kinyume chake.....kwenu katika maisha yako yote hakuna waislamu waafrika waliojenga shule au vyuo vya dini si dhani kama huko sahihi kwa hili.
 
Hapa napo weye umeharibu points zako. Mbona humo humo misikitini wanaingia waliotoka kufanya uchafu nao wanajifariji kuwa wesha koga na sasa wana tawadha tu waingie kuswali?? Hatuwaziki kwa vifo vya magonjwa hayo hayo ya zinaa??
Point ya mleta hoja ni kuwa; Je, ni lazima tujenge msikiti?? Kwa nini nisinunue vitabu vya dini nikavimwaga penye ule msikiti?? Weka Kuruani za kumwaga hapo watu waji sevie wenyewe ili kila nyumba ipate kitabu hicho kitakatifu. Mwaga Juzuu za kutosha na vitabu vingi vya dini ambavyo watu wengi hawana uwezo wa kuvinunua. Vigawe bure ili watu waisome dini yetu waielewe. Fadhili mihadhara ielezee dini yetu, Misikiti mingi mitaani sio kuwafanya watu kusilimu.
Nyie mnashida kumuunga mkono mtoa mada,hakuna msikiti unaokosa madrasa kwa ajili ya kupata elimu lakini cha ajabu wewe unayetetea huoni umuhimu Wa elimu ya dini pia vitabu vipi vinavyotolewa Bure kabisa na waislam mbalimbali na hata wako watu wanaojitoleya kusafiri kwenda kufundisha dini na wala hawaonekani kwenye TV lakini kazi ya dini wanaifanya.
 
Kuna tafauti kubwa sana kati ya Waislam na Wakristo katika hili, hata kama kuna waislam wamejenga Shule lakini kidogo sana..

Kwa vile mtoa mada sio Mwislam ndio inakuwa vizuri kumsikiliza mawazo yake kuhusu Uislam na usaidizi wa Jamii kitu ambacho dini yetu imesisitza

Kusaidia WAJANE , MAYATIMA na MASKINI ni jambo lililosisitizwa sana katika dini ya Kiislam

Quran zimejaa aya zinazosisitiza kusaidia Jamii hasa ya makundi hayo,..

Swali langu utawasaidiaje hao Maskini, Mayatima na Wajane kwa kujenga Misikiti, Misikiti ni sehemu ya Ibada sio chengine..

Tuamkeni Waislam, tujaribu kuisoma dini yetu na kuifahamu..

Back
Top Bottom