Waislam nijibuni hili

Waislam nijibuni hili

USSR,

Mkuu tahariri yako yaonyesha unawatakia mema sana waislam. Hongera, basi tuishauri serikali ya ciciem, au chama chcht kinachotaka maendeleo ya watanzania wakiwemo waislam.

1. Kuondoa sheria kandamizi zinazowazuia waislam kuendeshea miradi yao ya maendeleo. Na sheria moja wapo ni ya ugaidi. Sheria hii imekuwa kikwazo kwa taasisi nyingi za kiislam kukosa misaada. Kwa kile kinachosemwa pesa hizo zitawafanya waislam wawe magaidi.

Mfano wa taasisi hizo ni al haramin tanga, na dhynurain iringa. Taasisi hizi zimetenzwa nguvu kutokana na jitihada zao za elimu na afya. Mfano dhynuran kila walipojenga msikiti waliweka kituo cha afya. Huko tanga taasisi ya al haramain ilijikita kutoa elimu bure, hii ndio hali ya taasisi nyingi za kiislam kuminywa na kutopewa ruhusa ya kupata misaada ya maendeleo.

Pia kuna hali ya viongizi wa bakwata kulazimishwa waombe kujengewa msikiti badala ya mahitaji mengine. Haya tunayaona wanapokuja viongozi kutokana nchi za kiislam duniani.


2. Serikali itoe ajira kwa alimu wa dini na yatambulike kwa ajili ya maadili mema mbadala ya kununua magari ya gharama kubwa kwa ajili ya wanasiasa

3. Serikali iajiri wahudumu wa afya na madakatri kwa hospitali zinazoendeshwa na taasisi za dini badala ya kununua ndege ambazo zinaendeshwa kwa hasara na 99% ya wanyonge hawafaidiki nazo.

4. Waislam wenyewe wajivue ktk ufinyu wa fikra kuwa mambo yanayohusu dini ni Yale yanayojulikana ni ya kiroho tu. Huu ni ufinyu wa fikra. Na ni Ushindi ambao wameupata wapinzani wa Uislam. . Wapinzani wa Vitabu Vitukufu vilivyotangulia walifaulu kufanya hila ya kuvitia mikono na kuviharibu Vitabu hivyo.
Lakini Wapinzani wa Quran wameshindwa katika jitihada zao za kuipotosha Quran. Hata hivyo, wamepata ushindi wa kuifungia Quran ndani ya wigo wa kitawa ambamo kila msomaji wa Quran ameondoka katika lengo lake la mwongozo wa maisha ya kila siku huku akiridhika kuwa anasoma Quran kwa wingi ktk kujenga misikiti kwa ajili ya kuswalia, kufunga nk

Laiti waislam ungefungamana na lengo lilelile lililoifikisha na Mtume (saw) na Maswahaba katika kilele cha mafanikio ya kijamii, kisiasa, kiutamaduni, kitabia, kidiplomasia, basi uilsma ungeonekana kuwa ni mfumo kimbilio la wanadamu.

Leo waislam tumeyaacha mafundisho usahihi kuwa uislam unafungamana na matendo yote kwa ajili ya manufaa ya miwili yetu na matendo kwa ajili ya manufaa ya roho zetu. Na hivyo turudi kwenye uislam kamili kwa kujenga na kusimamia vyote,, msikiti, Madrasa, shule, hospitali, nk
 
Kiongozi, jitahidi kutoingilia imani za watu wengine.

Inawezakana Wakristo tulio wengi hatujenga makanisa kama watu binafsi lakini wengi wetu tunachangia sana ujenzi wake kila wiki. Hata sehemu ambazo makanisa yameisha jengwa, michango haijawahi kusimama. Kwa matiki yako, kwa nini tusipeleke michango hiyo kwenye mashule au hospital?
 
Kumpangia mtu baki matumizi ya hela yake ni wivu au ujinga, inawezekana wivu wa kijinga.

Tafuta zako, fanyia vyovyote unavyotaka.

Sent using Jamii Forums mobile app
umekurupuka kujibu mkuu.


hapana sehemu mleta mada anampangia mtu cha kufanya,ni kama nawewe unaona unaweza kujenga msikiti mwingine pale chang'ombe ni wewe tu na mihela yako.lakini kwa sababu msikiti upo,kama ungejenga shule moja hata ya sekondari uitishe waislamu wasome bure elimu bora,nayo ni sadaka na ingekuwa na mashiko zaidi.

watu wameruhusiwa kusali mpaka majumbani mwao,lakini sina uhakika kama wameruhusiwa kupata elimu ya msingi,sec,au chuo majumbani mwao.tujitahidi kufikiri kwa upana zaidi sio kijinga wakati wote.
 
Kiongozi, jitahidi kutoingilia imani za watu wengine.

Inawezakana Wakristo tulio wengi hatujenga makanisa kama watu binafsi lakini wengi wetu tunachangia sana ujenzi wake kila wiki. Hata sehemu ambazo makanisa yameisha jengwa, michango haijawahi kusimama. Kwa matiki yako, kwa nini tusipeleke michango hiyo kwenye mashule au hospital?
labda sababu ya vichwa mgando vya wengi wetu,ndio tunaona kuna tatizo kwa mleta mada,na hii imefanya hata tz yetu leo kuwa ilipo,sababu ya kupuuzia mapungufu ambayo tunaamini hayatuhusu.

waislam ni jamii yetu.hawawezi kuwa hawatuhusu,maana imani yao ndio maisha yao.
 
Kwahiyo akhera inajengwa kwa kutoa misaa ya bia, pombe mbali mbali, kitimoto na damu ya yesu?

Cᵃʳᵉᵉᵐ ᵀʰᵉ ᴸᵉᵍᵉⁿD
fanya ujinga mwingine halafu,komaa kujenga misikiti,uone kama kuna pepo ya bei rahisi kiasi hicho.
 
BAHARI J, ndio ujue wengi wanasoma kitabu chao na wanameza ila hawaelewi wanakaririshwa.

kwamba msikiti tu ndio sadaka endelevu.shule,zahanati,kituo cha watoto yatima ni kikomo.
 
Nadhani hili laendana na Dini ya mtu.

Kwa Muislamu kuacha zawadi ya Dini ndiyo iliyokubwa.

Nadhani wazo bora ni kujenga kilicho haba.
ndio point yake,misikiti ipo,watu wanatumia mwanya huo kujinufaisha kiumaarufu,waislamu bila kujua wanakubali kuingia mkenge.

sawa msikiti ukiishajengwa hauwezi kukataliwa,sharti utoe huduma ilitokusudiwa,lakini kubishia hili swala la msingi hivi,nimeshangaa sana.
 
USSR,
Labda umetaja misikiti kwa kuwa ndio unayoisikia kuna taasisi inaitwa african muslim agency hawa wamechimba visima kila wilaya unaiyoijua wewe tanzania.au hili huna taarifa zake ???
 
Wasaidieni watoto yatima wapate mahitaji yao na waende shule,wagonjwa wasio na uwezo,wafungwa na maskini waweze kuinuka labda mnaweza kuipata hiyo akhera njema.
Kwahiyo akhera inajengwa kwa kutoa misaa ya bia, pombe mbali mbali, kitimoto na damu ya yesu?

Cᵃʳᵉᵉᵐ ᵀʰᵉ ᴸᵉᵍᵉⁿD

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Labda umetaja misikiti kwa kuwa ndio unayoisikia kuna taasisi inaitwa african muslim agency hawa wamechimba visima kila wilaya unaiyoijua wewe tanzania.au hili huna taarifa zake ???
sasa kwani jamii inahitaji visima na misikiti peke yake!!!

afadhali sasa hao walioona maji ni shida zaidi ya misikiti.
 
Wasaidieni watoto yatima wapate mahitaji yao na waende shule,wagonjwa wasio na uwezo,wafungwa na maskini waweze kuinuka labda mnaweza kuipata hiyo akhera njema.

Sent using Jamii Forums mobile app
hilo sio swala la kusema labda.ni pie hiyo.

biblia imeandika dini ya kweli ni ile inayosaidia yatima wajane na wasiojiweza.ukijikita hapo mzee baba wakupindua pepo yako labda general GOD himself.
 
ndio point yake,misikiti ipo,watu wanatumia mwanya huo kujinufaisha kiumaarufu,waislamu bila kujua wanakubali kuingia mkenge.

sawa msikiti ukiishajengwa hauwezi kukataliwa,sharti utoe huduma ilitokusudiwa,lakini kubishia hili swala la msingi hivi,nimeshangaa sana.
Labda umenielewa vibaya..

Naendelea kusisitiza...wazo bora ni wewe kujenga unachoona kwako ni haba.
 
Mtoa mada umepost bonge la kontent... Ila wanajibu upumbavu.
Magufuli pia aliwahi kwenda Sumbawanga suluhisha mgogoro wa kiwanja cha msikiti...
Mwaka jana kaenda uzindua Basi wao rohoo kwatu..

Kifupi achana nao.
 
Si ndiyo mnavyofanya mnauana harafu mnasingizia Marekani na Israel kuwa zinawachonganisha!!!
Bado mnaongea hisia...hujui hata kama mimi ni muislamu au la.

Unampangiaje mtu cha kujenga ilihali anatumia pesa yake? Wewe tafuta zako jenga shule au zahanati...tusiende mbali hata kujadili umuhimu wa vilivyojengwa.

Mimi hata ujenge jengo lisikaliwe na mtu ilimradi umetumia jasho lako siwezi nikahoji.
 
Kama Marekani au Uingereza ingeamua kujenga makanisa kila kona. Wangekuwa super power country leo hii? Leo ukipewa visa ya kwenda kuishi nchi yoyote Uarabuni, Uingereza na Marekani. Utaenda kwenye nchi gani? 99.9% watachagua Marekani. Kwanini? Kwasababu ni nchi yenye uchumi mkubwa. Huo uchumi wangeupataje kama wangeamua kujenga makanisa kila kona?

Wafrika wajinga sana. Wao wanaona dini ni muhimu kuliko maendeleo. Kuna wajinga wengine nimewaona wanaona dini ni maendeleo. Nani alikuambia dini ni maendeleo?

Ukijenga msikiti wewe unaenda peponi moja kwa moja. Kumbe peponi unaweza kwenda baada ya kujenga msikiti hata kama unamatendo mabaya.

Wanaongoza kuwa matajiri ni waislamu? Kwahiyo kwasababu Manji, Mo au Bakheresa ni tajiri muislam basi na wewe huo utajiri unakuhusu? Nilikuwa nashangaa mbona ngozi nyeupe wanajichagulia wafrika watumwa wanavyotaka?

Kumbe akili nazo hakuna. Dini zilizoletwa na wafanyabiashara wa watumwa na pembe za ndovu mnaziona za thamani sana.
 
Back
Top Bottom