Waislam nijibuni hili

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
9,896
22,664
Nilisikia na baadae kuona Mbwana Samatta katoa sadaka ya kujenga msikiti eneo lile lingetosha shule, hospital au kiwanda kidogo, kwa nini msikiti na pale kuna misikiti kibao inamaana zawadi ni msikiti tu hamtaki maendeleo zaidi ya misikiti?

Wakati nikiwa Morogoro nilishuhudia IGP mstafu mzee mahita akikabidhi msikiti licha ya eneo lile kuwa kubwa angeweza kujenga shule, zahanati au kitega uchumi chochote kitoe ajira watu wanufaike ,nikajiuliza zawadi ya maana ni msikiti

Misaada mingi ya mataifa ya kiislamu yaliyopiga hatua kama Qatar, Saudi Arabia,Brunei, Irani, Kuwait ,Oman na n.k wanaleta pesa wajenge misikiti mfano ule msikiti mkubwa pale Dodoma wa ghadafi angeweza kujenga chuo,shule ,zahanati na pale Dodoma misikiti ipo kibao kwa nini msikiti?

Juzi nimemuona msanii mkubwa yule ambaye anhmgeweza kujenga shule pale kigoma,zahati au hata kiwanda amechoma pesa kwa kujenga msikiti na pale kigoma misikiti imejaa kila mtaa hivi hakuna cha maana zaidi ya misikiti.

My take
Kuna haja mjipange maana mnatumia nguvu kubwa kujaza misikiti lakini maeneo mnayokaa yamejaa changamoto za shule, zahanati, vyuo na kero chungu mzima, jiongezeni

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani kila mmoja anahaki ya kutoa zawadi aitakayo labda kama hili kisheria haliruhusiwi mtanisahihisha.

Wewe ni nani hadi uwaamulie cha kutoa. Wewe tafuta penye eneo jenga hospitali au shule. Mwenyezi Mungu ndiye katijaalia kila tulichonacho.

Kwangu nawaunga mikono...sioni la zaidi zaidi ya kujenga misikiti/nyumba za ibada watu wamwabudu Muumba.

Tusisahau.
-Dini inaleta amani.
-Inaunganisha watu.
-Inaadabisha jamii.
-Inakusanya watu.
 
imeandikwa katika Quran kwamba hapa duniani tukiondoka kitu pekee tutakacho kiacha na chenye manufaa baada ya kuondoka kwetu ni swadakatl_jaalia yaan sadaka yenye kuendelea. kwa mfano:
msikiti-watu wataendelea kusalia hata kama haupo
kisima-watu watakunywa na kutumia maji
mti wa matunda,
mtoto uliempa elimu ya dini, nk.

Hivyo watu wana chimba visima, kijenga misikiti, kupanda miti ya matunda, kununua vitabu vya dini(quran) jua sababu kuu ndo hyo hapo juu. Hasa zaidi ni maandalizi ya kesho baada ya kuachana na uhai wa dunia.

Natumai umenielewa. mengine wataongezea wadau.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulikuwa na point nzuri lakini umeiburunga kwa ignorance na chuki zako dhidi ya dini ambayo huijui.

1. Uamuzi ni wa mtoaji mwenyewe though angeshauriwa pia. Kama hujui basi nakjuilisha leo, aya ya mwanzo katila Quran basi inasema, " SOMA" ikisisistiza kutafuta knowledge.

2. Ikiwa waislamu wao wangeweza kujenga zahanati ama shule, lakini huja question mapadre na wakuu wa makanisa kutumia pesa nyingi kuishi maisha ya kifahari kwa pesa ziwe zao ama za sadaka.

3. Visima vingi vya maji utaona ni misaada ya kutoka hizo nchi unazozitaja na utaona vimeandikwa kwa Kiarabu.

4. Waislamu tumeambiwa lengo la.kuletwa duniani ni ibada tu, na ibada hufanywa msikitini.

5. Misikiti nayo hujengwa na sehemu ya kutowa elimu.

6. Hizo Zahanati ziwe nyingi kiasi hicho zipate kuwatibu maradhi ya zinaa na blood.poisoning related to alcoholism?

7. Kinachotakiwa ni serikali kuwapa wananchi wake ajira na kuwajali ili wajinunulie lishe bora kujenga afya zao!
 
Nyenyere sababu kwa waislam jambo lolote ambalo Allah yuko radhi nalo ni ibada so usipokunya utaumwa kisha kuna ibada utashindwa kufanya kwa usahihi.
SO USIFIKIRI NILUKUWA NADHIHAKI WAISLAM
 
Hujui historia ndio maana unasema dini inaleta amani
Nadhani kila mmoja anahaki ya kutoa zawadi aitakayo labda kama hili kisheria haliruhusiwi mtanisahihisha.

Wewe ni nani hadi uwaamulie cha kutoa. Wewe tafuta penye eneo jenga hospitali au shule. Mwenyezi Mungu ndiye katijaalia kila tulichonacho.

Kwangu nawaunga mikono...sioni la zaidi zaidi ya kujenga misikiti/nyumba za ibada watu wamwabudu Muumba.

Tusisahau.
-Dini inaleta amani.
-Inaunganisha watu.
-Inaadabisha jamii.
-Inakusanya watu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leo umekuwa mtu mzima na like yangu nimekupa bado mdogo wako kawe alumni
 
Bandiko lako limeegemea sana kwenye wivu au chuki juu ya imani flani,lakini je kweli kwamba hakuna waislam ambao wametoa vitu au misaada mbalimbali ya kusaidia jamii? jibu bila shaka litakuwa ni ndio,je hawa hukuwaona? mwisho kwenye kutoa zawadi au msaada mwenye kutoa ndiye huchagua atoa nn na kwa sababu gani.kwa hiyo waache watoe kila ambacho wao wanadhani kitakuwa na maana kwao na jamii inayowazunguka
 
Daby,
Mdau katoa ushauri mzuri, Dini ni upuuzi
Dini inaleta utengano, dini inaleta machafuko, dini ipo kinyume na logic, kinyume na elimu
nchi kama Somalia, Nigeria, Pakistan n.k zina machafuko yasiyoisha sababu ya Dini..Waarabu wamekuwa wakiuawa hapo mashariki ya kati tangu karne na karne sababu ya dini
 
Back
Top Bottom