Wahuni wa CCM na Zitto Kabwe wameungana kumchafua hayati Magufuli. Wana kisasi sababu alizuia mianya yao ya kufanya ufisadi

Sema uovu mmoja aliofanya
Wizi wa trillion 1.5 na zaidi.

Manunuzi ya meli hewa ya Mv Dar es Salaam

Kuwafuga na kuwalea watu wasiojulikana

Kuwajaza watu was kabila lake kila sehemu

Sema uovu mmoja aliofanya
 
Wizi wa trillion 1.5 na zaidi.

Manunuzi ya meli hewa ya Mv Dar es Salaam

Kuwafuga na kuwalea watu wasiojulikana

Kuwajaza watu was kabila lake kila sehemu

Thibitisha huo wizi wa 1.5 trilion.
 
Mbona hatusikii watu wakotekwa au kuokotwa maiti kwenye viroba, mbona hatuoni wanasiasa wakipigwa risasi hadharani lazima tujue nchi ilipotea njia
Ila wapo waliobambikiwa kesi ya ugaidi, enzi zake hawakuwepo
 
Ma Rais wote wa Tanzania baada ya kutoka Madarakani Critics wao kwa namna moja au nyingine mapungufu yao yalianikwa kuanzia Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Jakaya na hata sasa Magufuli

Hata Bi Samia akitoka nae upande wake wa pili utaoneshwa

Ma Rais wote walioruhusu kukosolewa wakiwa madarakan baada ya kutoka Madarakan hawakushambuliwa sana kwa kuwa hakukuwa na jipya ila wale waliogoma kukosolewa wakiwa Madarakan walishambuliwa sana baada ya kutoka

Kumbe kuna kundi kubwa la wanasiasa hapa Tanzania wana kinyongo na hayati JPM sababu alisimama kidete kulinda pesa za umma na kuwafanyia makubwa watanzania kwa kipindi kifupi akiwa rais wa JMT.

Kuna kundi la wanaCcm ambao huko nyuma walinufaika na ufisadi kupitia deal kama Epa, Kagoda Escrowa na mizengwe kibao. Ambao baada ya hayati JPM kuingia madarakani aliziba mianya yao na kuwafanya wakose raha kabisa maana walizoea kuwaibia watatanzania

Sasa hivi wanamtumia Zitto kumchafua hayati JPM ili aonekane kama alikuwa kiongozi fisadi na muonevu. Zitto alishughulikiwa na hayati JPM kwa siasa zake za kinafiki za undumila kuwili hiyo hakuwa na nafasi za kupiga dili kama enzi za Jakaya.

My take; Watanzania sio wajinga wameshashutuka juu ya mpango wa kumchafua hayati JPM.
 
Usinisakame Magufuli alikuwa si mtenda haki, alikuwa mtukanaji, hakuwa mnyenyekevu, alikuwa mjivuni I, mwenye dharau na kebehi
Tumuombee kwa Muumba wetu amsamehe dhambi zake,sote tuna mapungufu,alikuwa na mazuri yake ambayo hata baada ya miaka mia hakuna wa kuziba pengo lake,tumepwaya vibaya mno
 
Kasome CAG report achana na maigizo ya kwenye sinema
Iweke hapa hyo sehemu ya wizi kwenye report ya CAG, kingine cha kukusaidia kwenye auditing ikitokea auditing query huwezi ukakimbilia kusema ni wizi moja kwa moja. Mtafute auditor yoyote akusaidie jinsi ya kusoma na kuelewa hizo reports. Haya tufanye ni kweli pesa ziliibiwa.. thibitisha uhusika wa magufuli kua yeye ndie aliyeiiba na sio maafisa wengine.
 
Huyu Zitto wenu ndio alisema msiwaamini wasemacho wanasiasa huku na yeye pia ni mwanasiasa. Huyu ni ndumi lakuwili kama jamaa yule wa mhimili ule wenye watu wengi. Huyu bwana mdogo ni opportunist...... Hii mutu ni tatizo kubwa......
 
Magufuli ndiye Rais fisadi Papa bora wa muda wote kwani haijawahi kutokea tokea uhuru Rais akapiga ufisadi wa TZS 1.5 trilioni ndani ya awamu moja ya uongozi wake.

Ufisadi aliopiga Magufuli ni mkubwa kuliko ufisadi wote wa awamu zote nne za nyuma yake ukijumlisha kwa pamoja.

Sifa na utukufu zimwendee CAG Profesa Musa Assad ambae alifanya kazi nzuri sana ya kuibua ufisadi ule wa historia.

View attachment 2057729View attachment 2057730View attachment 2057732View attachment 2057733
khaaaa ila wewe jamaa kiboko
 
Nimegundua wanasiasa wengi wa Nchi hii ni Majizi ya pesa za Umma.Ila tutamkumbuka sana Magufuli hasa mm binafsi Kwa kz nzuri aliyotufanyia sitabadilika hata siku Moja juu ya huyu Shujaa wa Afrika Mzalendo wa kweli juu ya Nchi yake Tanzania.

Kazi ipi nzuri we Kiroboto ya Kupoteza Watu na Kutupa Coco Beach wakiwa Kwenye Viroba.
 
CAG yupi? Mbona Assad alipohojiwa pale ikuku ya magogoni na JPM mwenyewe alikana hizo tuhuma? Nenda Youtube kaangalie... uthibitisho mwingine?
Awali ni awali tu, hakuna awali mbovu. Sisi wenye akili kauli ya kwanza ndiyo ukweli wenyewe.

Kauli zilizofuata zilitoka baada ya vitisho na CAG Assad alipogoma kushirikiana na majizi ikabidi afurushwe ofisini kinyume na utaratibu.

Sent from my SM-J320H using JamiiForums mobile app
 
Kumbe kuna kundi kubwa la wanasiasa hapa Tanzania wana kinyongo na hayati JPM sababu alisimama kidete kulinda pesa za umma na kuwafanyia makubwa watanzania kwa kipindi kifupi akiwa rais wa JMT.

Kuna kundi la wanaCcm ambao huko nyuma walinufaika na ufisadi kupitia deal kama Epa, Kagoda Escrowa na mizengwe kibao. Ambao baada ya hayati JPM kuingia madarakani aliziba mianya yao na kuwafanya wakose raha kabisa maana walizoea kuwaibia watatanzania

Sasa hivi wanamtumia Zitto kumchafua hayati JPM ili aonekane kama alikuwa kiongozi fisadi na muonevu. Zitto alishughulikiwa na hayati JPM kwa siasa zake za kinafiki za undumila kuwili hiyo hakuwa na nafasi za kupiga dili kama enzi za Jakaya.

My take; Watanzania sio wajinga wameshashutuka juu ya mpango wa kumchafua hayati JPM.
TOKOMEZA WAHUNI
 
Back
Top Bottom