Kama ni kweli Hayati Magufuli alifanya Ufisadi kupitia Katiba hii ya 1977 kwanini Zitto Kabwe anazuia mchakato wa Katiba Mpya?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,998
142,025
Penye ukweli uwongo hujitenga.

Kama ni kweli hayati Magufuli alifanya ufisadi mkubwa huku kila mtu akiogopa kumwambia labda yule kidume Tundu Lisu tu, maana yake ni kuwa Katiba yetu ni mbovu sana.

Kinachonishangaza Zitto Kabwe ndiye mwenye Hoja ya ufisadi wa Magufuli lakini Zitto Kabwe huyo huyo hataki Katiba mpya ipatikane sasa hadi baada ya miaka kenda ijayo.

Zitto Kabwe anataka Tume mpya ya uchaguzi kana kwamba ndio itasimamia rushwa na ufisadi.

Kama Rais Magufuli alifanya ufisadi wakati Zitto Kabwe akiwa bungeni na alishindwa kukemea basi ni vema Zitto awaishwe Milembe hospital kabla hajaathirika zaidi.

Ramadan kareem!
 
yeye anatafuta vitu viwili
1. Kuingia bungeni haraka akidhani kuwa tume huru bila katiba itamuingiza bungeni
2. Kumfurahisha Samia ili kupata cheo

basiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii Zito amefikia hapo
 
Mzee nikuulize swali. Ukijiangalia vizuri ungependa au ungetamani mwanao akulie katika Tanzania unayoiishi wewe? Tanzania ambayo kupata fursa lazima uwe chawa wa CCM? How sure are you kwamba mwanao na yeye atakuwa chawa kama wewe? na asipokuwa chawa una uhakika atatoboa kweli?

Personally, sijali sana maana ingawa CCM siwapendi lakini niko miongoni mwa wachache tunaofaidi hii "system". Lakini kila nikijiangalia nisingependa mtoto wangu akulie ndani ya Tanzania iliyo chini ya hii CCM. Ningependa katiba mpya ambayo inatoa fursa kwa wote. Yenye kuheshimu utawala wa sheria. Yenye kuweka mazingira ya ushindani wa kisiasa sawa kwa wote. CCM ambayo haihitaji kuwa chawa kupata fursa zilizopo.

Kwa sasa naangalia vijana wengi wanaopiga kelele kuitetea hii "CCM yetu" mitandaoni na kwingineko..., lakini ukiangalia future zao ni zero nyingi. Sana sana wanaambulia kuwa wakimbiza mwenge au hivyo vyeo vya kulamba miguu watawala.

Anyway, kila mtu anakula kwa urefu wa kamba yake.
 
Penye ukweli uwongo hujitenga.

Kama ni kweli hayati Magufuli alifanya ufisadi mkubwa huku kila mtu akiogopa kumwambia labda yule kidume Tundu Lisu tu, maana yake ni kuwa Katiba yetu ni mbovu sana...
Guys...
Katiba mpya has nothing to do with crime. Kwani wenye katiba nzuri hawana wizi?
Uhalifu
Ufisadi
Ubaguzi na mauaji?
Angalia Kenya Afrika kusini na hata Marekani
Je hawana kesi kama zetu?

Katiba mpya ni jambo zuri lakini tusiseme uongo eti itakuja kuondoa matatizo yote.
 
Mzee nikuulize swali. Ukijiangalia vizuri ungependa au ungetamani mwanao akulie katika Tanzania unayoiishi wewe? Tanzania ambayo kupata fursa lazima uwe chawa wa CCM? How sure are you kwamba mwanao na yeye atakuwa chawa kama wewe? na asipokuwa chawa una uhakika atatoboa kweli?...
Tanzania ya sasa ni afadhali ile ya Nyerere!
 
Back
Top Bottom