Kwanini Zitto Kabwe anapotosha taarifa ya CAG ili kumchafua Hayati Magufuli?

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Oct 2, 2020
4,086
6,568
Kama anajua fika kuwa ni utaratibu wa kawaida CAG akiibua hoja basi lazima PAC na LAAC wazipitie na kuhakiki kama kuna ubadhirifu basi wao ndio watatoa majumuisho. Lakini amekomaa kumchafua hayati JPM kwa nini?

Huyu kiongozi wa Act Wazalendo anatumika na wanaCCM kwa manufaa ya gani kumchafua hayati JPM?

Huyu ni mpiga madili kama ilivyo Nape Nnauye,January Makamba na kundi lao. Kuna uwezekano hawa ndio wanatumika kumchafua hayati JPM kwa manufaa yao tu sababu tu aliwakataa kwa maovu yao.
 
Kwa nini CAG anaandika report inayoifanya zitto amkosoe JPM?

Kwa nini serikali Inamuajiri CAG aandike report ya kumchafua JPM?

Kwa nini printers na makaratasi zinakubali kutumia kuandikiwa report ya kumchafua JPM

Jibu ni jepesi

'kwa sababu alikuwa mchafu'
 
Kwa nini CAG anaandika report inayoifanya zitto amkosoe JPM?

Kwa nini serikali Inamuajiri CAG aandike report ya kumchafua JPM?...
Kila kitu ulichoandika kinawezekana kabisa. CAG alituambia mpaka stendi ya mbezi na masoko ya kisasa yaliyojengwa karibu nchi nzima hayana manufaa. Tafakari!!
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema Ikulu sio sehemu ya kukimbilia kusaka Uraisi ni pahala patakatifu.

Kama Mjomba Magu alifanya kinyume chake asingeweza kuchunguzwa achia mbali kushtakiwa kwa kuwa yupo juu ya sheria hata akingatuka kwenye wadhifa huo.Ni sheria zilizopitishwa na bunge letu kuwa Raisi asishtakiwe.

Lakini hata kama ripoti ya CAG inabaini mapungufu ya wasaidizi wake,watadai ni amri toka juu.

Tuache kuabudu watu tufuate haki na msingi ya utu, usawa, kuheshiminiana,kutonyanyaswa katika nchi yetu.
 
Back
Top Bottom