Wahindi wanaletwa na nani kiasi hiki?

Wahindi wanaletwa na nani kiasi hiki?

Ni Kauli ya Kibaguzi.
Kwa taarifa yako Nchi ya Tanzania ina jamii ngeni chache sana.
Wazungu ni wa kutafuta, unaweza zunguka mjini siku nzima Daresalaam usikutane na wazungu, labda Arusha mjini.
Wahindi waarabu na wa mashariki ya mbali ni wachache sana.
 
Habari zenu wanajamii forum natumai mko na afya njema kabisa..sasa niende kwenye mada
Hivi ni nani anawaleta wahindi kiasi hiki?

Hili suala wabongo inabidi mliangalie na mjitafakari kwa weledi wa hali ya juu. Kwa muda mchache niliokaa bongo nilichokishuhudia karibia asilimia 85% uongozi wa juu katika sekta nimetembelea wapo wahindi( yaani almost 85% ngazi za juu ni wageni )

Kilichonifikirisha zaidi ni ile Jana nilikaa na muhindi mmoja kwenye moja ya hotel ipo mjini huku tukiwa tunaongea katikati ya maongezi alisema "'I know almost the price of each officer in the immigration department" hili neno lilinifanya niunganishe dots nyingi sana na kuniacha na maswali.

Sasa shida ni nini mpaka asilimia kubwa ngazi za juu wamejaa wahindi kuliko wazawa.

Je hakuna sheria za kulinda ajira za wazawa hasa kwenye ngazi za juu? Je wazawa ni wavivu, hawajitumi au sio waaminifu?

Mamlaka iliyopewa dhamana wanashikishwa kitu? Au hakuna maexpert wenye uweledi mzuri wa kusimamia kazi?

Naomba wanazengo tujuzane hapa..
Hoja ni mbovu. Mleta mada ni mjinga. Haya maongezi yameshapitwa na wakati. Na sisi watanzania tunajitambua.

Mtu wa kukushangaza kwenye mambo haya ni mzungu na mchina tu! Wahindi na waarabu hapa ni kwao kama wewe.

Acha chuki zisizokua na msingi. Na jwa hasira hao wahindi watanzania waliokua nje wote warudi nyumbani kujenga taifa.

Nyumbani kumenoga.
 
Na bado! Watakuja wengi sana na kwa spidi hii ya vijana wengi wa kibongo wanataka kuwa wanamuziki na ha waigizaji au kujikita kwenye siasa na kusoma hamtaki.Mnategemea wataalamu kwenye hivi viwanda tunavyoanzisha watatoka wapi? Acha umbea nenda kasome
 
Reginald Mengi alikua mtetezi sana wa wazawa/wazalendo lkn cha ajabu kwny ma Co. Yake yote Top bosses ni hao hao wahindi.

So jibu ni 1 tu wahindi kwny usimamizi wa ma-biashara/hizi mambo za Accounting&finance wako njema sana na hua hawacheki na kima wakipewa kuisimamia Co/Excuses za kikuda ni marufuku na sikatai pia wahindi wabababishaji wako kwa sana tu.

Nimesoma na wahindi Primary,tukiwa Primary sisi tukirudi home ni kucheza chandimu tu wkt mtoto wa kihindi anashinda dukani kwa baba yake na saa nyingine weekends anaachiwa duka full day auze bila usimamizi wa mtu mzima na wala hana interest za kudokoa maana anakwambia baba ameniambia nikimaliza shule Mtaji wa kuanzisha duka langu utatokea hapa hapa so nikimuibia ni sawa na najiibia mwenyewe.

Secondary nilisoma darasa 1 na watoto wa kihindi kama 8 hivi,3 baada ya kumaliza form 6 wakajoin shughuli za baba zao,3 wakaenda kusoma nje na hawakurudi mazima na 2 wakaenda kusoma Muhimbili udaktari wakapiga mpk internship yao na walipomaliza hakuna hata mmoja aliyeenda kuajiriwa kwny hosp. Yoyote ile either ya Private or Govt wakarudi kusimamia biashara za familia ambazo hazihusiani kabisa na mambo ya udaktari.

So nadhani Business kwao iko ndani ya damu iwe ni kwa kupenda au ni kwa kujua kabisa kwamba kwa mazingira haya tuliyonayo biashara ndio itatutoa mambo ya kuajiriwa tuwaachie wazawa.

Ingawa sikatai pia Wako wahindi kibao wamekuja kutoka nje kufanya kazi bongo kwa njia yoyote ile iwe halali au haramu.
So point ni kwamba wanajua business kuliko wengine
 
Kazi wanazofanya watanzania! Kazi zipi? Watanzania hawa wanaoamka kwa kuvalia kujilinganisha na Diamond Platnumz na Chris Brown kisha kuchukua picha kwenye barabara mpya au hawa wenye kuamkia katika vilinge vya kamari na pool table? Au wenye kuketi vibarazi na kuanza kujadili ngono na watu? Au hawa wenye mawazo ya ajabu kupitia mitandao kama mtoa mada?
Nenda india kama utapata kazi zao hata kama una sifa kuwazidi, nenda mahoteli ya kitalii kaangalie wapishi walioajiliwa toka nje nafikiri ni Tanzania pekee ndio unakuta mwenyeji anatetea mgeni ndio maana hata mtanzania akiwa na issue polisi na mgeni polisi wataanza kumkandamiza mwenyeji tembea nje ya Tanzania uone tofauti ya mwenyeji na mgeni
 
Jiulize kwanza mkuu,kwanini kuna maeneo kwenye mikoa mingi kama sio yote ile mikongwe kuna maeneo yanaitwa uhindini?,hata kama ukiwazuia kuingia nchini,hawa waliopo humu kabla ya hata wewe hujazaliwa wakiamua kuzaana kwa nia ya kuongeza idadi lazima wawe wengi tu...
 
Hoja ni mbovu. Mleta mada ni mjinga. Haya maongezi yameshapitwa na wakati. Na sisi watanzania tunajitambua.

Mtu wa kukushangaza kwenye mambo haya ni mzungu na mchina tu! Wahindi na waarabu hapa ni kwao kama wewe.

Acha chuki zisizokua na msingi. Na jwa hasira hao wahindi watanzania waliokua nje wote warudi nyumbani kujenga taifa.

Nyumbani kumenoga.
Kwa kauli zako wewe ndo unakuwa mjinga sasa, kama mwenyewe ashakwambia anajua bei ya kila officer hapa nchini wewe unazungumzia nini hapo
 
Nenda india kama utapata kazi zao hata kama una sifa kuwazidi, nenda mahoteli ya kitalii kaangalie wapishi walioajiliwa toka nje nafikiri ni Tanzania pekee ndio unakuta mwenyeji anatetea mgeni ndio maana hata mtanzania akiwa na issue polisi na mgeni polisi wataanza kumkandamiza mwenyeji tembea nje ya Tanzania uone tofauti ya mwenyeji na mgeni
Nimezaliwa na naishi na race tofauti na tunaishi the same, sijaelewa mantiki yako.

Ukosefu wa ajira millioni 4 ni sababu ya watu wenye asili ya Uhindini katika taifa lenye wakazi millioni 60?
 
Back
Top Bottom