Wahindi wanaletwa na nani kiasi hiki?

Wahindi wanaletwa na nani kiasi hiki?

Sekta nyingi ni ngapi na ni zipi hizo?
Kama sekta binafsi kwenye biashara huko hakuna shida hao wengi ni raia halali wa Tanzania na ukiona siyo raia hao ni expert au kuna udanganyifu(rushwa) ambao upo hata kwenu Kenya.
Wahindi wengi raia wa Tanzania hawapendi kuajiriwa na serikali hivyo wanakuwa kwenye biashara zao na za wahindi wenzao, kwa vile wao ni raia halali sheria ya wazawa na wao inawalinda sababu wengi karibu uliowaona ni wazawa.

Mkoloni alileta wahindi wengi kusaidia kujenga reli na kuwapa ajira flani ambazo wakati wa mkoloni watu weusi walikuwa hawana ujuzi nazo.
Hao wahindi wengi walibaki hapa Tanzania na vizazi vyao ndio ulio waona.
Hawa ni aina ya watu ambao hawafikirii kwa kutumia akili zao. Huongozwa na chuki za kikabila au kidini.

Angalia baadhi ya nyuzi zake humu
 
Habari zenu wanajamii forum natumai mko na afya njema kabisa..sasa niende kwenye mada
Hivi ni nani anawaleta wahindi kiasi hiki?

Hili suala wabongo inabidi mliangalie na mjitafakari kwa weledi wa hali ya juu. Kwa muda mchache niliokaa bongo nilichokishuhudia karibia asilimia 85% uongozi wa juu katika sekta nimetembelea wapo wahindi( yaani almost 85% ngazi za juu ni wageni )

Kilichonifikirisha zaidi ni ile Jana nilikaa na muhindi mmoja kwenye moja ya hotel ipo mjini huku tukiwa tunaongea katikati ya maongezi alisema "'I know almost the price of each officer in the immigration department" hili neno lilinifanya niunganishe dots nyingi sana na kuniacha na maswali.

Sasa shida ni nini mpaka asilimia kubwa ngazi za juu wamejaa wahindi kuliko wazawa.

Je hakuna sheria za kulinda ajira za wazawa hasa kwenye ngazi za juu? Je wazawa ni wavivu, hawajitumi au sio waaminifu?

Mamlaka iliyopewa dhamana wanashikishwa kitu? Au hakuna maexpert wenye uweledi mzuri wa kusimamia kazi?

Naomba wanazengo tujuzane hapa..

Wewe unaongea nini?Mhindi kakwambia anajua bei ya kila afisa uhamiaji (kiwango cha rushwa), sasa jikite kwenye rushwa na idara husika hayo mengine ni redundant kwa kauli ya huyo mhindi.
 
Wewe kama unamfahamu Mhindi (au mtu wa kabila yoyote) ambaye ameingia nchini kwa kuhonga afisa wa Uhamiaji si useme tu? Kwanini usitoe taarifa kwa TAKUKURU au Ikulu au kwa Waziri wa Mambo ya Ndani? Una haki hiyo ITUMIE badala ya kutuletea hadithi za Alinacha hapa ili kuchochea hisia za kibaguzi. By the way hiyo 85% ngazi za juu ni wizara gani au kampuni gani? Mimi nimezaliwa bongo lakini sijaona hiyo

Ukweli ndio huo kwamba kuna wahindi wengi sana mpaka kwenye ajira ndogo ndogo kama Security/Mgambo na hii binafsi nimeenda kule Lugoba ambako kokoto zinazotumika Dar na kwingineko zinazalishwa nimekuta Mgambo wa kihindi hajui hata Kiswahili mpaka awepo mkalimani ndio mnaelewana, Nenda kwenye Kampuni za ujenzi pia utakuta wageni wakifanya kazi za kawaida kabisa wakiwa na vibali vya kazi kupitia wizara ya mambo ya ndani, viwandani, migodini mchezo ni huo huo
 
Tukiwamaliza kuwabagua wahindi tutaanza wachaga, nk

Mtu atuhumiwe kwa jinai yake iwapo kafanya - sio kwa asili yake.

Jihadhari na simplicity, ipo hoja na inamaslahi kwetu sote kwa vizazi vyote, ndiomaana kuna sheria na miongozo, utumwa ukitawala unakuwa kama dini,
 
Ukweli ndio huo kwamba kuna wahindi wengi sana mpaka kwenye ajira ndogo ndogo kama Security/Mgambo na hii binafsi nimeenda kule Lugoba ambako kokoto zinazotumika Dar na kwingineko zinazalishwa nimekuta Mgambo wa kihindi hajui hata Kiswahili mpaka awepo mkalimani ndio mnaelewana, Nenda kwenye Kampuni za ujenzi pia utakuta wageni wakifanya kazi za kawaida kabisa wakiwa na vibali vya kazi kupitia wizara ya mambo ya ndani, viwandani, migodini mchezo ni huo huo

Tatizo watz wengi Utopolo tu vitu viko wazi wazi mostly wako enclosed na wanajifanya wanajua. Tembeeni myaone yaliopo Tanzania
 
Habari zenu wanajamii forum natumai mko na afya njema kabisa..sasa niende kwenye mada
Hivi ni nani anawaleta wahindi kiasi hiki?

Hili suala wabongo inabidi mliangalie na mjitafakari kwa weledi wa hali ya juu. Kwa muda mchache niliokaa bongo nilichokishuhudia karibia asilimia 85% uongozi wa juu katika sekta nimetembelea wapo wahindi( yaani almost 85% ngazi za juu ni wageni )

Kilichonifikirisha zaidi ni ile Jana nilikaa na muhindi mmoja kwenye moja ya hotel ipo mjini huku tukiwa tunaongea katikati ya maongezi alisema "'I know almost the price of each officer in the immigration department" hili neno lilinifanya niunganishe dots nyingi sana na kuniacha na maswali.

Sasa shida ni nini mpaka asilimia kubwa ngazi za juu wamejaa wahindi kuliko wazawa.

Je hakuna sheria za kulinda ajira za wazawa hasa kwenye ngazi za juu? Je wazawa ni wavivu, hawajitumi au sio waaminifu?

Mamlaka iliyopewa dhamana wanashikishwa kitu? Au hakuna maexpert wenye uweledi mzuri wa kusimamia kazi?

Naomba wanazengo tujuzane hapa..
Unauliza swali huku jibu tayari unalo?

Hiyo 'fungua na funga semi' ya kimombo uliyoiweka kwenye mada yako hii ndiyo jibu lake na hapa tungeijadili hilo tu, ikiwezekana hao mumiani kama wanafahamika, waanikwe hadharani ili wawajibishwe.
 
hannibali Tanzania huwakilishwa na race zote ulimwenguni toka enzi na enzi. Generation unayoitizama leo ni ndogo sana baina ya awali. Watu wenye asili ya Uhindini wamekuwepo kwa muda mrefu.

Tanzania ya miaka 70's ilikuwa na watu wenye asili mbalimbali kwa wingi kabla ya wengi kuondoka, kuhama au kuhujumiwa. Mfano, katika miaka ya 70's mji wa Bukoba ulikuwa na watu wenye asili ya Uhindini takribani 2300+ ilhali hivi sasa ni takribani 1000+ utaona waTanzania wengi walivyohama taifa.

We share the common blood, needs and totally we the same! #HumanWithoutBorder #OneNation #OneWorld Upendo, Amani, Furaha, Hekima, Busara na Umoja ni Nguvu!
Wabaguzi hao mnawasupport hivi?hatari sana
 
Tanzania ilisha wahi kuwa na Waziri mhindi

Nafikiri unamwongelea Amir H Jamal ambaye yeye hakuwa kama hawa wagonga ulimbo tunaowaongelea hapa au mtu kama Shivji huwezi kusema ni Mhindi kwa tafsiri ya mtu wa kuja toka nje ya inchi, taabu yetu ni hawa wanaokuja na upepo wa kisulisuli hata kiswahili hawajui halafu unamkuta ofisini akiwa ni cashier, karani, HR etc
 
Back
Top Bottom