Wageni wa 'ghafla' majumbani mwetu.....

Kwa kawaida mimi sipendi wageni waje kwangu. Na mimi kwa ujumla sipendi kwenda kwa watu. I love my humble abode. Hivyo ndivyo nilivyo.

But every once in a while I do hold some cook outs and invite a few people over. Drop-byes are one of my biggest pet peeves. You drop bye unannounced and for no good reason you risk getting the cold shoulder....
 
Watu mna roho mbaya hamna hata ubinadamu,
mbona sisi watoto wa majirani wanashinda kwetu
na iwe lunch au dinner wanakula sembuse wageni.

hii ni njema sana unajua kabisa watoto wa majirani huwa wanashinda kwako haina neno hapa tunaongelea ugeni wa ghafla bila taarifa wengine unakuta wanatia timu saa mbili usiku
 
Kwa kawaida mimi sipendi wageni waje kwangu. Na mimi kwa ujumla sipendi kwenda kwa watu. I love my humble abode. Hivyo ndivyo nilivyo.

But every once in a while I do hold some cook outs and invite a few people over. Drop-byes are one of my biggest pet peeves.

Hilo neno NN, kama wamekuwa invited basi inaeleweka kabisa na siyo kujenga tabia ya kila Jumamosi, Jumapili na siku za sikukuu kuzuka bila taarifa mnamo nyakati zinazokaribia na msosi. Halafu ni watu wale wale.
 
Kwa kawaida mimi sipendi wageni waje kwangu. Na mimi kwa ujumla sipendi kwenda kwa watu. I love my humble abode. Hivyo ndivyo nilivyo.

But every once in a while I do hold some cook outs and invite a few people over. Drop-byes are one of my biggest pet peeves. You drop bye unannounced and for no good reason you risk getting the cold shoulder....
NN mbona unatishia amani hivi kama nimeibuka kwako ghafla utanitimua?
 
BAK mwenzio ilibidi niingie jikoni kusongoloa ugali mida ya tatu na nusu maana dalili za kuondoka sikuziona mgeni aje kwako saa moja aondoke saa tano unampa juice,mie nilinuna maana nalala saa tatu na nusu watu hawaondoki nimepiga miayo kuwaonyesha kama nimechoka lakini hawasomi alama za nyakati siku nyingine nadhani nikisikia hodi naenda kulala RR usinimalize mwenzio

mimi kuna aina ya wageni ambao ni 'mood killer na very boring' kwa ujumla
yaani ukimuona tu ,unasikia kuchoka kwanza.kabla hajaanza story zake ambazo
unatamani ziishe but waapi...na mtu haondoki mpaka giza liingie na kaja mchana...lol
 
hii ni njema sana unajua kabisa watoto wa majirani huwa wanashinda kwako haina neno hapa tunaongelea ugeni wa ghafla bila taarifa wengine unakuta wanatia timu saa mbili usiku
hapo nitaumia kimoyomoyo ila kuwaambia ukweli nitaona soo,
maana unakuta halafu wamekuja wakifurahi so unapowakatisha stimu dah watajihisi umewafanyia unyama.
 
mimi kuna aina ya wageni ambao ni 'mood killer na very boring' kwa ujumla
yaani ukimuona tu ,unasikia kuchoka kwanza.kabla hajaanza story zake ambazo
unatamani ziishe but waapi...na mtu haondoki mpaka giza liingie na kaja mchana...lol

hahaah Boss! hata hajaanza wewe ushachoka!

Hata huyo kuja mara moja moja sio mbaya anakujengea immune ya kuwa bored kirahisi. Lakini atoe taarifa mapema. Kunahitajika kujipa matayarisho ya moyo kukabiliana nae
 
Unajua mimi huwa sielewi kabisa. Sasa sijui sielewi kwa vile mimi siko hivyo...

Kwangu ni common sense. Mtu huwezi tu kwenda kwa mtu (ukiondoa shida au haja ya dharura) pasipo kumtaarifu. Kwangu ni jambo rahisi sana na wala halihitaji tafakuri. Lakini unakuta mijitu mingine inaona ni jambo la kawaida tu.
 
Tafadhali usije ukathubutu! Sina simile mimi.

Kama sitakuuliza 'umekuja kutafuta nini?' au 'shida yako nini?' basi nitakwambia waziwazi kuwa 'leo sitaki wageni'....lol

Jee mtu kupiga simu tu bila mpango, "kupiga story"?

Mimi hata simu sitaki, mtu akipiga simu hana sababu ya msingi ananirusha stimu ile mbaya.
 
Tafadhali usije ukathubutu! Sina simile mimi.

Kama sitakuuliza 'umekuja kutafuta nini?' au 'shida yako nini?' basi nitakwambia waziwazi kuwa 'leo sitaki wageni'....lol

mimi nina ndugu yangu alikuwa na rafiki mzungu wa south africa hapa bongo
ukienda kwake ghafla anaongea na wewe bila 'kufungua geti' wewe uko nje ya geti
yeye yupo ndani ya geti lol
 
Jee mtu kupiga simu tu bila mpango, "kupiga story"?

Mimi hata simu sitaki, mtu akipiga simu hana sababu ya msingi ananirusha stimu ile mbaya.

afadhali hiyo.
mwingine ana beep kutwa hadi unampigia
halafu 'anakusalimia tu' lol
 
Jee mtu kupiga simu tu bila mpango, "kupiga story"?

Mimi hata simu sitaki, mtu akipiga simu hana sababu ya msingi ananirusha stimu ile mbaya.

Nimekuelewa. Ila hiyo kuna namna ambayo wewe mpigaji simu ukichomekea maneno mawili matatu inapunguza kidogo ule usumbufu kwa yule uliyempigia.

Kwa mfano, unampigia mtu na kumwambia kuwa hujamsikia siku nyingi na ulikuwa unataka kumsalimia tu na kujua anaendeleaje, basi. Hiyo nadhani itamfanya hata yule uliyempigia kuona kuwa hukuwa unataka kumsumbua kwa stori zisizo na mbele wa nyuma.

Ila sasa na wewe mpigaji simu usiendeleze stori. Ishia hapo hapo halafu mtakie siku njema na umwambie mtaongea siku ingine panapo majaaliwa, kwaheri. Short and sweet.
 
Jee mtu kupiga simu tu bila mpango, "kupiga story"?

Mimi hata simu sitaki, mtu akipiga simu hana sababu ya msingi ananirusha stimu ile mbaya.

tena simu ndo kabisa mtu unakuwa hauko ktk mood harafu mtu anakupigisha ma story yasiyoeleweka
 
afadhali hiyo.
mwingine ana beep kutwa hadi unampigia
halafu 'anakusalimia tu' lol

Mtu umekuwa nae kazini wiki nzima. Weekend mpaka akupigie basi!! Huwa wananikera ile mbaya.

Huwa natamani kuwaambia "weekend nataka kuitumia kupumzika kazi na yatokanayo"
 
tena simu ndo kabisa mtu unakuwa hauko ktk mood harafu mtu anakupigisha ma story yasiyoeleweka

Mimi huwa namwambia "I'm in the middle of something, siwezi kuongea sana sasa" mwenyewe anajua akate.
 
Mtu umekuwa nae kazini wiki nzima. Weekend mpaka akupigie basi!! Huwa wananikera ile mbaya.

Huwa natamani kuwaambia "weekend nataka kuitumia kupumzika kazi na yatokanayo"

au mko kwenye starehe na mwenza wako
labda beach,labda restaurant .pengine mnazungumza 'yaliyo yenu wawilli'
ghafla mtu. kwa kuwa anawafahamu. anajiunga tu....
mnajikuta mko wa tatu na 'hanyamazi na story zake ' lol
 
Hivi na nyinyi mshawahi kufeki kama unaongea kwenye simu pale umwonapo kwa mbali mtu ambaye unayemfahamu anakuja eneo ulipo wewe?

Ile umwonapo tu unachomoa simu yako halafu unaiweka sikioni kama vile uko bize kwenye maongezi....lol

Hii yote ni katika kum-avoid tu huyo mtu maana akisimama kuongea na wewe itachukua forever na wewe huna muda ama hujisikii kumsikiliza na mistori yake.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom