Stories of Change - 2023 Competition

saadala muaza

Member
May 12, 2023
38
37
Uhai unasiri kubwa sana ambayo kila mwanadamu anatamani kuupata angalau ufunguo wa siri hii ili kuchungulia hata akiba ya pumzi yake japo jambo hili laweza lisimsaidie chochote.

~~~

###### Ilikuwa ni usiku wa giza totoro sanaa, giza ambalo weusi wake uliyapiga kibao macho yangu na kuyafanya yasiweze kung'amua chochote kilichokuwa mbele yangu,ukungu wake ulizifunika kope za macho yangu, baridi kali likiupapasa mwili wangu na huku sauti kali zenye kutisha zikiupasua moyo wangu. Akili yangu haikufanya kazi kwa sekunde kadhaa nikiitafakari hali hii, hali ambayo ilinifanya niongeze kasi ya kufikiri na kukumbuka kuwa mara ya mwisho nauweka ubavu wangu wa kulia kitandani niliiacha simu yangu kwenye mfuko wa nyuma wa suruali yangu ambayo sikuivua maana nilikuwa nimechoka sana kwa usiku ule.

Kwa haraka sana akili ikautuma mkono wa kuume kuupapasa mfuko ambao uliitikia."oooh!" Ilikuwa ni mshangao baada ya kugundua kuwa hakukuwa na kitu chochote mfukoni mwangu. Wakati nikiwa bado katika wimbi zito la mawazo, mara nikasikia sauti ikilitaja jina langu na kuniamuru nisimame pale nilipo na kisha nipige hatua tatu mbele bila kukosea.Taratiibu nikaipa kazi mikono yangu kuubeba mwili ambao ulikuwa ni kama mzigo, tena mzigo haswaa.wakati nikiwa bado najivuta vuta ili niweze kusimama vizuri nikahisi mtu ameung'ang'ania mguu wangu,moyo wangu ukapusa tena kwa mara ya pili "paaaah!"

"Ni nini hiki Mungu wangu!" bila ya kupoteza muda nikainama haraka sana na kushika lile eneo nililohisi kuna mikono ya mtu.Sikuamini nilichokigusa,ndioo! ilikuwa ni mikono ya binaadam tena mikono ambayo ilikuwa na ubaridi sanaaa na huku ikiwa na majimaji ambayo sikuweza kugundua kwa haraka kilikuwa ni kitu gani, nikapaza suti "niachiee" lakini haikuwahi kuwa hivyo baada ya kugundua kuwa sauti yangu haitoki kabisa kwenye koo langu.Wakati wote huu nikihangaika kuutoa mguu wangu pale ulipokwama,ile sauti iliyoniamuru nipige hatua tatu ikasikika tena na mara hii ikiashiria msisitizo zaidi "tumekwambia utembee hatua tatu kwenda mbele lakini inaonekana unakibri,fanya hivyo haraka sana".

Hili likanifanya nizidi kuwa na wasiwasi zaidi, mapigo ya moyo wangu yakaongezeka mara dufu zaidi,mwili ukaanza kutetema na wasiwasi ukajaa ndani ya nafsi yangu juu ya mahali hapa, mahali ambapo sikujua mpaka wakati huu nimefika fika vipi.Waswahili husema "liishalo ni dogo kuliko linalokuja" hivi ndivyo ilivyokuwa kwa upande wangu. Nikauvuta mguu wangu wa upande wa kushoto kwa nguvu mara tatu zaidi ya nilivyo fanya mara ya kwanza ili niweze kujinasua kutoka katika mikino ile ambayo iliukamata mguu wangu kwa ustadi mkubwa sana,wakati huu nikafanikiwa kuutoa mguu wangu katika mikono lakini kwa bahati mbaya nikajikuta naanguka kama hatua tano mbele yangu bila kujua,"inaonekana huwezi kufanya ulichoelekezwa sasa utaadhibiwa kwa utovu huu mkubwa wa nidhamu,hatuishi na watu wapumbavu hapa".

Ilikuwa ni sauti ilele iliyoniamrisha mara kadhaa namna ya kufuata utaratibu,lakini kwa wakati huu ikionesha ni kwa namna gani wameudhika na kile kilichotokea. itaendelea.......
IMG_16838091528361664.jpg
 
Ilikuwa ni sauti ilele iliyoniamrisha mara kadhaa namna ya kufuata utaratibu,lakini kwa wakati huu ikionesha ni kwa namna gani wameudhika na kile kilichotokea. itaendelea.......View attachment 2619876
Bonge la story
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom