Wafanyakazi wa ofisi za serikali acheni roho mbaya

Captain mopao

Senior Member
Feb 25, 2021
133
379
Mwaka huu nilikua nafatilia maswala ya mirath ya mzee, so ilinifanya nikatembelea ofisi nyingi za kiserikali. Kwa kawaida ukiwa unafatilia mirathi hizi ofisi lazima ufike zote au chache:
  • Mtendaji
  • Vizazi na vifo
  • Mahakama ya mwanzo
  • Mahakama kuu
  • Bank
  • PSSF
Na nyingine ambazo inategemea carrier ya marehemu, mambo niliokutana nayo ktk ofisi hizo ndugu bila pesa hutoboi yaani swala linaloweza kuchukua mwez mmoja unafatilia mwaka mzima.

Ngoja nikupe mfano mmoja baada ya kesi ya mirathi kuisha ilibidi tupate nakala ya hukum itakayotumika bank pssf na ktk taasisi zingine but secretary wa mahakama alituambia ana kaz nyingi hivo tuje baada ya week 2 ilibidi tumpe pesa pale na akaichapa mda huo huo tukaondoka nayo, na kitu kimoja nimejifunza ktk ofis nying nilizopita ofisi ambayo nilikutana na muhusika ni mwanaume nilipita kirahisi ila ofisi zote nilizokuta muhusika ni mwanamke nilikwama na ndo nilitumia sana pesa kwa hawa dada zetu.

Sisi tukiwa kwenye vyeo tusiwe tuna roho mbaya jaman swala unaloweza kulifanya leo unamwambia mtu aje week 2 au 3 hujui unakwamisha watu wangap, kuna watu niliowakuta nao wanafatilia mirathi na wamepigwa kalenda tangu mwaka jana na mambo bado na ukimwangalia hana pesa ya kutoa sehem yeyote ile dah inauma sana.

kitu kimoja nilijifunza baadhi ya ofis nilizokua naenda nasaidiwa bila kuombwa chochote nilikua najikuna nampa ata buku tano mhusika namwambia pesa ya chai, ilinisaidia maana kuna wakati nilikua naambiwa umekosea hapa rudi ofisi flani ukalekebishe ukiludi tu anakusaidia fasta anakumbuka fadhila zako.

Ijapokua mimi nilikua na watu tunaofahamiana baadhi ya ofis ila mpka sasa sijatoboa miez 3 ila nyie mliopo humu km upo kitengo chochote ebu tuache roho mbaya jaman fanyeni kazi kwa utu na moyo, sehemu tulipoenda na tukasaidiwa bila kigugumizi ni bank tu.

Nawasilisha ndugu zangu.
 
kuna wale wanasema nidhamu kazini imerejea, sijui huwa wanamaanisha nini kwa kweli. Pita pita ardhi na idara zake zote ndio utawafahamu vizuri watumishi wa Umma, Mungu awaponye huu ugonjwa kwa kweli.

Kiwanja mwekezaji amenunua 87M bado anatakiwa atoe chai ili hati itoke haraka!!!!
 
... na kitu kimoja nimejifunza ktk ofis nying nilizopita ofisi ambayo nilikutana na muhusika ni mwanaume nilipita kirahisi ila ofisi zote nilizokuta muhusika ni mwanamke nilikwama na ndo nilitumia sana pesa kwa hawa dada zetu
Basi ungebadili title ili kuwatendea haki wanaume. Ungesema "Watumishi wa serikali Wanawake acheni roho mbaya"
 
Tafuta kazi yako achana na kulilia mirathi ya mzee wako henya kutafuta. Pambana kijana acha short cut life. Nyie ndio mnaombeaga wazee wenu wafe
Acha kurukia garimoshi kwa mbele. Sio wote wanaofuatilia mirathi wanakuwa na njaa na hizo pesa.

Kakuambia alipita mpaka ofisi za vizazi na vifo, hiyo inatosha kukujulisha kwamba mzazi wake amefariki.

Hauruhusiwi kufuatilia mirathi kama muhusika ni mzima wa afya, hata kama hajiwezi kitandani mtabeba hivohivo.
Unforgetable
 
Tafuta kazi yako achana na kulilia mirathi ya mzee wako henya kutafuta. Pambana kijana acha short cut life. Nyie ndio mnaombeaga wazee wenu wafe
Wapi ameandika analililia mirath ya baba yake mkuu?!!! Na ulitaka afatilie mirathi ya nan kama si Baba yake ambaye ni marehemu!!! Si kila afatiliaye hayo mambo ukafikiri ni njaaa japo ni haki yao kabisa ya marem baba yao!! Msijifanye watafutaji sana kuliko wengine,! Si ajabu huyo mwamba hapo anakaz yake na maisha yake tuu..

Ila amefanya kufatilia pengine yeye ndiye anayejua kuingia hapa na pale pia kumsaidia Mama kupata haki ya marehem mumewe! Lakini pia Si ajabu ni yeye ndo yupo karbu na familia ndugu zake wengine wapo mbali, au wapo Katibu but yeye ndo kapewa jukumu LA kufatilia!!! Wengine hamuwez kufatilia mirath coz Hanna cha kufatilia coz wazaz wenu walikuwa Si watumishi..

Au mmeamua kupambana kivyenu.. Lkn hata kma mzaz hajawaachia kiwanja utafatilia nini kwa mfano!!!! Maana hata maandiko yanasema Baba mwema na mzuri huacha urithi kwa watoto mpka kwa watoto wa watoto wake (wajukuu) kwahiyo Kama mzee wenu hakuacha kitu kwenu huna cha kufatilia.

Na Kama kipo wewe hutaki kufatilia waache ndugu zako wagatilie maana ni haki yao!!! Hivyo basi Kama hamkuachiwa kitu vunga mkuu!!! Si dhambi kufatilia jasho la baba yao Bali ni haki yao!!
 
Kupata mirarhi lazma uhenye kama mzee wako alivohenya kuipata mali, unataka mali kirahisi rahis? Ili ukipata ukaweke heshima bar. Lazma uhenye mirathi haitoki kirahisi mkuu pambana n
 
Kuna ofisi za serikali unaenda unaweza subiri mtu wa kukuhudumia hadi masaa mawili.
kuna wale wanasema nidhamu kazini imerejea, sijui huwa wanamaanisha nini kwa kweli. Pita pita ardhi na idara zake zote ndio utawafahamu vizuri watumishi wa Umma, Mungu awaponye huu ugonjwa kwa kweli.

Kiwanja mwekezaji amenunua 87M bado anatakiwa atoe chai ili hati itoke haraka!!!!
 
kuna wale wanasema nidhamu kazini imerejea, sijui huwa wanamaanisha nini kwa kweli. Pita pita ardhi na idara zake zote ndio utawafahamu vizuri watumishi wa Umma, Mungu awaponye huu ugonjwa kwa kweli.

Kiwanja mwekezaji amenunua 87M bado anatakiwa atoe chai ili hati itoke haraka!!!!
Watumishi wasipoongezewa mishahara huwa mnachekelea sana.

Haya mambo yanataka maamuzi sio kuchekelea matatizo ya wenzenu
 
Nchi hii bila kutoa rushwa huwezi kufanikisha jambo lako kwenye ofisi za umma.....nenda ardhi, tra,tfda, TANESCO usipotoa hela huduma usahau
 
Ukikwama mahali popote mpigie mwenezi wa chama katika kile kipindi chake cha papo kwa papo kinachorushwa mubashara chanel ten . Bila shaka ni kila jumamosi kuanzia saa tatu usiku.. au unaenda ofisi ya chama, nimeona watu wengi wanasaidiwa..asante..
 
Back
Top Bottom