KERO RITA (Vizazi na Vifo) na Ofisi za Uhamiaji - Tanga, simamieni taratibu na sheria muache kuomba rushwa. Mnaharibu na kudalilisha Taasisi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Nawasalimu kwa jina la JMT!

Ni imani yangu ujumbe huu utafika kwa wote, na kadhalika utawafikia Walengwa na mara Moja wataacha Tamaa na tabia zisizoridhisha..

Kwanza niwasifu baadhi ya Maafisa wa Serikali wanaofanya kazi kwa weledi sana, na kujituma na kuifanya sehemu ya kazi kuwa kama ni sehemu ya uhalisia wao. Kongole sana kwenu..

Kilichonileta hapa si kuwasifia wanaofanya kazi nzuri, ila ni kuoneshwa kutopendenzwa na Taasisi hizi mbili sana sana RITA na UHAMIAJI.

Nimefanya sasa utafiti wa chini chini kwa Mikoa kama mitatu mkoa wa Mwanza, Mkoa wa Shinyanga, mkoa wa Dar es salaam, Mkoa wa Kagera na mwisho nilifanya Mkoa wa Tanga.

Ila kote kwenye Taasisi hizi zinanuka Rushwa sana.

Naomba nielezee Tanga kwa sababu ndo nimefanya mwaka huu, na ndio ya mwisho na ndio ina uozo mkubwa kuliko mwingine.

RITA
Rita Tanga Jiji (Ofisi ya mkuu wa Wilaya) ile ofisi iliyokaribu na Chuo Kikuu Huria (Open University).

Kiukweli huduma zenu zamani zilikuwa nzuri sana ila hivi karibuni Wananchi wamewalalamikia sana kutokana na kuwa na wimbi la kuchukua rushwa.

Sikuamini hilo mpaka nilipojitosa mwenyewe, ikabidi nijivishe jukumu nikawaomba mama watatu kwa nyakati tofauti niende kuwachukulia cheti niwe kama baba wa mtoto, walikubali, kufanya hivyo.

Niliyokutana nayo.
Nilithibitisha kweli rushwa iko wazi wazi tena Mtumishi anaomba bila kificho..(Kwa maana nilipoingia nilikuwa anamuomba Mteja pesa ya chai).

Nitanukuu. "Sasa nimekufanyia kazi yote hiyo naomba ya chai basi nipate kutuliza koo"

Nikiwa bado nipo maeneo yale yale nikiwa Ofisi ya mapokezi Ya RITA aliingia mteja mwingine akiwa ni mwanafunzi akitaka cheti bei zilikuwa zimeandikwa lakini akaambiwa bei hizo asizifuate akatajiwa bei zingine zilizo juu.

Na kabla hajaanza ku-upload Taarifa zake au kuzipeleka Chumba cha Pili alimwambia hivi "Kuna wenzako wameleta Taarifa toka wiki iliyopita hebu fanya mambo taarifa yako iwahi bhana ili na wewe uwahi shule au unapenda uwe unakuja kila siku ukose masomo"

Huku bado nikitafakari sana kauli za huyo mtu...(Huyo mtu kwa kumuelewa kwa haraka ni mtu mwenye lafudhi ya Watu wa Magharibi ya nchi yaani ni Mwanaume kutoka Kigoma nahisi kwa maongezi yake ni Muha)

Bhasi ikafika zamu yangu..

Sasa nikajaribu kuchezesha Karata kwakuwa majina ya Baba na taarifa baadhi nilipewa ila tatizo nilificha doccuments zote ili nione itakuwaje..

Nilifika pale nikiwa sina doccument yoyote ya mtoto, Hata ya Mimi Baba. Nikamueleza "Aisee boss mimi Bwana sina Tangazo, sina kadi ya clinic na kadi yangu ya NIDA nimeisahau ila ninakumbuka namba tu.."

Akajibu "Aisee hilo suala gumu sana mkuu, lakini hakuna kitu kinashindikana umekuja na barua ya Mwenyekiti wa mtaa?"

Nikamjibu "Hapana"

Akanijibu "Dah sasa umekuja na nini"

Nikajibu " Bhasi hakuna shida ngoja nikavitafute nitakuja"

Ndipo aliponizuia na kusema "Hayo mambo yanaongeleka Boss una haraka sana"

Akaniambia Hebu jaza hii form kwanza na cheti cha mtoto ni Tsh 17,000 wakati huo nikiangalia ni chini ya hapo sikutaka kubishana naye kwa sababu nilitaka kuproove kitu.

Baadaye akasema na kwa case yako utakuwa ngumu sana maana mpaka nikawashawishi humo ndani hebu fanya lolote bhasi.

Nikachomoa 17 ya cheti na nikampa 15,000 ya kuficha na kuziba ma-gape akasema hapo ndo umeongea nikamuuliza kinaweza kikatoka lini maana nina haraka sana nataka kesho by Jioni niondoke.

Akasema ngoja nikuitie Mtu akamuita jamaa fulani mnene kutoka chumba cha pili, wakaongea pembeni jamaa akaniita akamruhusu yule aondoke jamaa akachukua form yangu akaniambia Nimpe Tsh 20,000..
Nikaona isiwe tabu nikampa Tsh 20,000..

Akaniambia kesho mchana atanipigia simu nikafate cheti cha mwanangu aisee ni kama masiala kesho yake cheti kikawa kimekamilika.

Sasa kuna watu niliwauliza pia waliokuwa wanafatilia vyeti wengi wenye maisha Duni wanafatilia kwa miezi miwili na wengine wana sema wana miezi sita iliniuma sana roho..

Tafadhali rekebisheni mifumo hii..


UHAMIAJI
Hawa sijawachunguza sana ila kuna tukio walifanya nikiwa Tanga hapo hapo. Kuna rafiki angu alikuja kunisalimia ni Raia wa Uganda alikosa passport ya kusafiria nchini kwake, tukaenda nae pale Tanga Uhamiaji karibu na Forodhani.

Kufika wakamwambia awape NIDA ili wamsajili kwa njia ya Mtandao akawaambia bahati mbaya NIDA yake imeharibika na ilipotea. Wakamwambia kwa Kiswahili hicho huenda yeye sio Mtanzania jamaa alijitetea sana. Wakaomba barua ya Mwenyekiti akaenda kwa Mwenyekiti jamaa akapewa barua..

Kurudi bado wakaomba Vyeti vya Wazazi wake akasema hana walichofanya wakamwambie hawawezi kumsaidia. Jamaa akamwambia yule Askari kuwa anataka kuongea naye pembeni akachomoa Tsh 500K akampa askari akajifanya kuwa mkali kwamba kwanini kapoteza vitu.

Sasa sijui alitumia njia gani ila baada ya wiki Jamaa alifanikiwa kupata Pasport.

Naomba Serikali ishughulikie hii mifumo maana imejaa rushwa sana
 
Back
Top Bottom