Wafanyabiashara Mwenge waliopisha ujenzi wa Stendi wadai wametupwa na Manispaa ya Kinondoni

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Baadhi ya Wafanyabiashara waliopisha mradi wa ujenzi wa Kituo cha Mabasi Mwenge (Mwenge Bus Terminal) na kudai kuwa waliahidiwa kupewa kipaumbele baada ya mradi kukamilika, mambo hayajaenda kama walivyotarajia.

Wamedai kuwa ahadi hiyo ilitolewa Mwaka 2019 baada ya Mkandarasi Mshauri kukabidhi eneo kwa Mkandarasi Mjenzi.

Wanadai kuwa licha ya kuahidiwa kupewa eneo la biashara na store lakini ahadi hiyo haijatimia hadi Juni 2023 wakati ambapo mradi unaelekea ukingoni.

Wafanyabiashara hao ambao hawakuwa tayari kuweka majina yao kwa sasa wamedai kuwa wanapofatilia wanajibiwa kuwa hawana mkataba wa kisheria wa kupewa kipaumbele kwa kuwa tayari vyumba vya biashara vyote zinauzwa kwa mnada kupitia mfumo wa TAUSI.

Wanadai kuwa hali hiyo ni kinyume na tamko la Waziri Mkuu alipo tembele mradi, akasema watapewa kipauambele mradi ukikamilika.

Kino.JPG
=============

UPDATES...
Jitihada zinaendelea kupata upande wa Manispaa ya Kinondoni kuhusu madai hayo.

MAJIBU KUTOKA MANISPAA YA KINONDONI
IMG_7770.jpeg

Kufuatia tarifa ya malalamiko ya baadhi ya wafanyabiashara ya tarehe 27.06.2023 kupitia mandao wa Jamii Forum kuwa baadhi ya wafanyabiasha wametelekezwa kwenye upangishaji wa 'frame' zilizopo kituo kipya cha mabasi cha Mwenge, tunapenda kutoa ufafanuzi ufuatao:

Katika kuleta usawa kwa watanzania wote, imezimiwa kuwa ni vyema kutumia mfumo wa kupangisha 'frame' hizo kwa mtindo wa mnada mandao. Mwombaji atalazimka kuingia kwenye mfumo wa TAUSI a kisha kufuata maelekezo ya namna ya kuomba kupangishwa na atakayekidhi vigezo atapewa.

Mnada mandao utatoa fursa kwa wote kupitia ushindani huru na wa haki kwani Manispaa imeishapokea zaidi ya maombi 4.000 wakati 'frame' ni chache. Hii pia inawagusa wafanyabiashara waliokuwepo.

Hivo, tunazidi kuwahimiza wananchi wote wenye vigezo kuendelea kuomba wakivemo wafanyabiashara waliopo Mwenge.
 
Back
Top Bottom