The Great Haya
JF-Expert Member
- Apr 6, 2014
- 1,731
- 1,642
Baraza la madiwani lililopita kabla ya hili la sasa lilianzisha mchakato wa kujenga stendi katika manispaa ya Bukoba eneo la Kyakailabwa, na kabla ya kuimaliza muda wao ukaisha na hawakubahatika kurudi tena.
Hili baraza la madiwani la sasa limekuwa na mwitikio mdogo kuendeleza stendi hiyo huenda ni sababu za kisiasa kwa hiyo kuna hela za walipa kodi pale Kyakailabwa zimeota nyasi na badala yake wakaamua kuanzisha mradi wa kwao wa ujenzi wa stendi ya malori eneo la Ijuganyondo. Stendi ya malori mpaka sasa nayo ina kama mwaka imekamilika lakini haifanyi kazi kwa hiyo na hizo hela za walipa kodi ziko pale zinaanza kuota nyasi.
Makamu wa Rais alipofanya ziara mkoa wa Kagera (Bukoba manispaa) aliwaambia wananabukoba kuwa rais ataleta pesa bilioni moja kwa ajili ya kuanza ujenzi wa stendi ya mabasi, na mwaka huu 2023 tukapata taarifa hela tayari ipo kwenye akaunti ya halmashauri. Pamoja na mivutano yote mwishowe baraza la madiwani ikaamua kwenda kuendeleza stendi ya Kyakailabwa.
Cha kushangaza wakati mkandarasi ameshaanza kazi Kyakailabwa mkuu wa mkoa akaagiza ujenzi usitishwe na hiyo hela itumike kukarabati stendi ya zamani akidai stendi mpya isubiri miradi ya TACTIC wakati magari yakitumia stendi ya malori (ambayo haina kazi mpaka sasa) ila mpaka sasa kimya.
Sasa cha kujiuliza kwa nini stendi ya Bukoba imekuwa na sarakasi nyingi na serikali imekaa kimya. Je sio kwamba watu wanaitumia kujipatia mtaji wa kisiasa na kujipigia ela watakavyo?
Tafadhali Rais aingilie kati huenda hata bilioni yake haipo tena na Bukoba mvua zimeshaanza tumechoka kuchafuka kwenye stendi ya matope.