Uchaguzi 2020 Wafahamu baadhi ya Watia nia ya Ubunge wa CCM ambao hawakushinda katika kura za maoni lakini wamepitishwa kugombea katika majimbo yao

Screenshot_20200820-190046.png
 
Kuna umuhimu wowote wa kuendesha zeozi la kura za maoni kwa wagombea ubunge ccm?
Why Gwaji
Why Shigongo
Why Mwambe
Why Kimei
Why Katani
Kwanini?
 
Shinyanga Mjini hilo jimbo Chadema washindwe wenyewe, huyo Katambi 2015 alijaribu hapo Shinyanga akiwa CDM akakosa, naamini yule Masele lazima ana kinyongo.
Actually, kitendo cha kutoa Masele, ni uonevu wa hali ya juu. Labda ni Ule ugomvi wake na Ndugai. Masele looks to be a more leadership material.
 
Kuna umuhimu wowote wa kuendesha zeozi la kura za maoni kwa wagombea ubunge ccm?
Why Gwaji
Why Shigongo
Why Mwambe
Why Kimei
Why Katani
Kwanini!!!????

Sigongo unamuonea mkuu alipata kura sawa na mtetea kiti chake,nadhani ikaone mbunge mtetea kiti katumia rushwa hakubaliki kuliko shigongo
Ndo kapewa haki yake
Njoo wewe na chauma yako uchuane naye
 
Gwajima-Ndiye mwenye ubavu wa kumtikisa Mdee. Mchungaji ni rahisi kumdhibiti kondoo wake. Huko nyuma Mdee na hata Mwakiembe walishajihudhurisha madhabahuni pa huyu Askofu.
Pengo la mama wa upepo wa kisulisuli linazibwa nafikiri.

Kimei ni mzoefu wa mambo ya biashara ya fedha na mabenki. Uzoefu wake utasaidia mahalimahali. Atajibeba kirasilimali. Sijui aliiachaachaje crdb, alipostaafu.

Shigongo ni media tycoon kiswazswaz. Pengeni Diallo kapwaya ndiye mbadala.
 
Niamini mimi mkuu kama kuna watu waliotoa rushwa Kawe basi Askofu katoa hela nyingi kuliko wagombea wote nilikuwa karibu sana kwenye huu mchakato
Yeye si ameokoka na Ni mtumishi wa Mungu kwanini atoe rushwa na Ni dhambi, kwa mtindo basi kuona langu la mbingu wataenda hata machangu wallah
 
Jimbo la Muheza, CHadema na ACT mkiunganisha nguvu mnachukua asubuhi kabisa...kunakwenda kutokea kura za hasira...
Unaongelea Shinyanga mjini ipi,masele na gaki hawatakiwi kabisa tena huyo masele ndio ovyo kabisa bora kidogo huyo gaki.Gaki angeenda kugombea kwao moshi kwa huku shy bado sana
 
Boss Suley2019 Hao wamepitishwa kutokana na kuwa na Mtaji wa Watu aka Connection aka Kura


Dar es Salaam
Jimbo la Kawe
- Askofu Josephat Gwajima

Tanga
Jimbo la Muheza
- Hamis Mwinjuma (Mwana FA)

Mbeya
Jimbo la Tunduma
- David Silinde

Manyara
Jimbo la Babati Mjini

- Pauline Gekul

Kilimanjaro
Jimbo la Vunjo

- Charles Kimei

Shinyanga
Jimbo la Shinyanga Mjini
- Patrobas Katambi

Mtwara
Jimbo la Ndanda
- Cecil Mwambe

Geita
Jimbo la Busanda

- Tumaini Braison Magesa

Kagera
Jimbo la Bukoba Mjini
- Stevine Lujahuka Byabato

Katavi
Jimbo la Kavuu
- Jofrey Mizengo Pinda

Kigoma
Jimbo la Kusini/ Uvinza
- Nashon Bidyanguze

Rukwa
Jimbo la Nkasi Kusini
- Vincent Mbogo

Ruvuma
Jimbo la Mbinga Mjini

- Jonas Mbunda

Jimbo la Namtumbo
- Kawawa Vita Rashid

Njombe
Jimbo la Wanging'ombe
- Dk. Festo John Dugange

Tabora
Jimbo la Kaliua
- Aloyce Kwezi

Shinyanga
Jimbo la Kishapu

- Boniface Butondo

Lindi
Jimbo la Liwale
- Zuberi Kuchauka

Wafuatao ni wagombea Waliogongana idadi ya kura za maoni lakini akapitishwa mmoja:
Morogoro
Jimbo la Mlimba

- Godwin Kunambi

Mwanza
Jimbo la Buchosa

- Erick Shigongo

Mara
Jimbo la Mwibara
- Charles Kajege


= Orodha zaidi inakujia hivi punde =

KUJUA ORODHA YA JUMLA YA WAGOMBEA KATIKA MAJIMBO YOTE SOMA HAPA:
= > Uchaguzi 2020 - Yaliyojiri Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM: Majina ya walioteuliwa kuwania nafasi za Ubunge kwenye Majimbo mbalimbali nchini

PIA SOMA

= > Uchaguzi 2020 - Yaliyojiri upigaji kura za maoni za wagombea wa Ubunge na ujumbe wa Baraza la Wawakilishi kupitia CCM - Julai 20-21, 2020
 
Na hii ni kutokana na uonevu tuliofanyiwa wa wazi wazi kwa kukatwa majina yetu baada ya kuibuka washindi kura za maoni za Chama cha Mapinduzi lakini chama hicho kimetukata na kuteua watu wengine.

Sasa wamechokoza mziga wa nyuki wote tuliokatwa majina yetu tusikubali bora tuuze ramani ya vita kwa maadui ili tukose wote hakuna mwenye hati miliki ya CCM tukutane kwenye Kampeni CHADEMA jiandae kuchukua Nchi.
 
Na hii ni kutokana na uonevu aliofanyiwa wa wazi wazi kwa kukatwa majina yetu baada ya kuibuka washindi kura za maoni za Chama cha Mapinduzi lakini chama hicho kimetukata na kuteua watu wengine. Sasa wamechoka mziga nyuki wote tuliokatwa majina yetu tusikubali bora tuuze rama ya vita kwa maadui ili tukose wote hakuna mwenye hati miliki ya ccm tukutane kwenye Kampeni Chadema jiandae kuchukua Nchi.
Unaharakia wapi mkuu?

Sent from my SM-N910W8 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom