Wadau wa kanuni na sheria za fedha na bajeti za wizara bungeni,suala la matumizi ya fedha nje ya bajeti ya wizara limekaaje?

HOPEfull

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
1,726
2,082
Kazi iendelee kwema jamani.

Jana nimemsikia waziri wa wizara mmoja bungeni akijibu swali kuhusu matumizi ya fedha nje ya bajeti.Amejibu majibu rahisi as if anawajibu watu wa gani sijui na kinachonishangaza wabunge wameridhika na kukaa kimya.

Kitu kingine kinachonisikitisha ni kuwa sheria na kanuni za bunge naona zinambana sana mbunge kushindwa kuendelea kuhoji ama kwa sababu ya muda ama nafasi yake imekwisha ya kuuliza labda ajipange siku nyingine.

Hiyo husababisha waziri akishamjibu mbunge aridhike asiridhike inakuwa imetoka ikirudi pancha.Na kitu kingine sielewi Spika nae anakubali kufunika Kombe watu wapite Hata Kama majibu hayaridhishi. sielewi spika nae anatetea upande gani wa serikali au wabunge.

Spika anaonekana ana power kubwa Sana ya kumaliza mjadala hata Kama majibu hayaridhishi.Nawaonea huruma wabunge wanakaa bungeni kinyonge sana yaani wamelowa mvua,hawana nguvu ya kutetea hoja yao akiambiwa kaa kimya au kaa chini basi imetoka hiyo.Kuna haja ya kutafuta namna ya kumbana Spika ana power kubwa Sana.

Kuna hilo suala la matumizi ya fedha nje ya bajeti ya wizara kisheria limeekaaje.Utaratibu ukoje wa kuidhinisha matumizi ya fedha..na utoaji wa taarifa ya hayo matumizi nani anahusika.Hizi Ni fedha zetu tunazokatwa wananchi kwenye kodi mbalimbali ikiwemo tozo.Fedha za ziada hutolewa wapi na kwa utaratibu gani.

Kwenye masuala y account unapofunga mahesabu kuna kanuni za kubalance mahesabu na majina mbalimbali Kama balance sheet,, balance brought forward,, balance nini sijui.Sasa kwenye bajeti za wizara hivi vitu vimeekaje?

Wapi wananchi wanapata au wapi taarifa inatolewa ya bajeti ya wizara kama kuna fedha zinetumika nje ya bajeti.Kwa Nini kusiwe na utaratibu wa kila mwaka wa bunge wa wizara kutoa au kufanya balance sheet na balance brought down ya bajeti kila Mwaka kabla ya wizara kusoma bajeti mpya ili ijulikane kama Kuna matumizi ya ziada kuliko ilivyo sasa ya kutoa majibu mepesi mepesi.

Utaratibu wa sasa imekuwa business as usually.Ni kusoma figure tu ya bajeti mpya kila Mwaka hakuna taarifa extra ya bajeti ya wizara ndio maana inaleta maswali kwa baadhi ya wabunge makini lakini wabunge hao hawapati majibu ya kuridhisha aidha kwa kubanwa na sheria au na Spika.

Majibu yakishatoka kwa waziri biashara inakuwa imekwisha wapi Tena mbunge anaweza kukimbilia ili kupata ridhiko lake la suala analohoji.Na sijui kama wapo wabunge wa aina hiyo maana unaweza ukaonekana mgomvi na mtatala.

Halafu mawaziri Sasa hivi wanatoka bungeni wamerelax hakuna maswali kungwi ya kuwabana kama zamani na upinzani hakuna ndio kabisa inawafanya mawaziri kurelax.
 
Wote lao moja hao ndugu. Wote wanajuana. Jina lao kamili - walamba asali.
 
Back
Top Bottom