Bajeti ya Wizara ya Ujenzi 2023/24 ilikuwa 812 billioni zilizopokelewa ni asilimia 12 tu?

koryo1952

JF-Expert Member
Mar 7, 2023
380
763
Kwanza nimeshukuru Mhe. Chege - Mbunge wa Rorya kwa ufafanuzi na swali alilouliza kuhusu fedha za barabara zilizoidhinishwa kwenye bajeti na zilizopokelewa.

Mpaka sasa tumebakiza miezi minne tu kuanza na bajeti mpya ya 2024/25. Ninauliza ninyi Wabunge tuliwatuma kuisimamia Serikali, Je kazi tuliowatuma mnaifanya kwa usahihi?

Haingi akilini kuwa bajeti ya barabara ilikuwa 812 billioni na sasa imepokelewa tu 97 billioni. Nchi hii tunaelekea wapi?

Kama kwa wastani utekelezaji wa bajeti ya Serikali kwa mwaka ni 90% kwa mantiki hiyo kila Wizara ingekwishapokea angalau asilimia 70 ya bajeti yake na sasa Wizara zingine utakuta hata asilimia 10 hawajapokea. Ninaomba Mhe. Rais afanye mabadiliko makubwa katika Wizara ya Fedha.

Hakuna maana Wabunge kukaa Bungeni na kupitisha mambo ya hewa. Hii ni aibu kubwa sana.
 
Mkuu, kumbuka Rais JPM alikuwa anazifahamu vyema sekta za ujenzi na uchukuzi, kwa kuwa aliwahi kuhudumu kama waziri mwenye dhamana katika sekta hizo.

Kwa hiyo katika kila bajeti akiwa madarakani kama kiongozi wa nchi, na kwa kutambua unyeti wa sekta hizi, alihakikisha fungu kubwa la fedha linatengwa na kupelekwa kila mwaka katika wizara husika.

Rais wa sasa hana "background" kama hiyo. Naona dhahiri kuwa hana "priority" katika sekta hizi. Yeye kajikita zaidi katika utalii, na kidogo katika afya na elimu ya msingi.
 
Tuelezwe kwa uwazi utekelezaji wa mpango wa Bajeti 2023/24 mpaka sasa kwa kila Wizara/Sekta.
 
Back
Top Bottom