wadau tutangaze mali zetu!!

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,889
watanzania huwa tunashabikia sana viongozi kutangaza mali zao sasa ili kuonyesha ni jambo jema na sisi wanajamvi tutangaze zetu, tuwe wakweli.
Naanza: Mi nnamiliki kalaptopu ya laki nane, redio ya laki tatu, feni ya elfu hamsini ,shelfu la vitabu kama hamsini nilinunua ubungo bukubuku na kwenye akaunti nina laki nane.

kwa ujumla ninamiliki mali za kama milioni mbili.

haya wanajamvi tiririkeni!
 
Mimi ni mwanafunzi
ila ninamiliki ka-simu ka laki moja unusu,ka kompyuta kamoja used laki 5, nina kashamba ka ndizi na mibuni na vanira kaurithi bukoba hekari 3 unusu, nina vitabu kadhaa thamani yake kama laki moja.. Nina tv moja na radio moja..
Nitarudi kutoa thamani halisi.karibu
 
sorry nilisahau simu nina simu MTN ya elfu ishirini na nne
 
hp computer full set
Toshiba satelite laptop
Ipad 2, 32 gb
Nokia C3 Phone
Samsung Dual sim Phone
Viatu pair 37
Saa ya TAGHeuer Carella
Saa ya Seiko 5
Bracelet gram 45 Silver
Pete tatu za Silver gram 15,6,9
Necklace ya silver gram 24
sina kitanda wala godoro nalala kwenye mkeka
 
mimi nina simu ya tochi ,laptop ya laki nne, na vijitabutabu kama vya elfu thelathini hivi halafu nina laki moja na thelathini elfu benki.
 
hp computer full set
Toshiba satelite laptop
Ipad 2, 32 gb
Nokia C3 Phone
Samsung Dual sim Phone
Viatu pair 37
Saa ya TAGHeuer Carella
Saa ya Seiko 5
Bracelet gram 45 Silver
Pete tatu za Silver gram 15,6,9
Necklace ya silver gram 24
sina kitanda wala godoro nalala kwenye mkeka
umenikumbusha malima, kompyuta tatu, bunduki, bastola na masimu kibao utafikiri pusha
 
Me ninamilik BMW 3,hammer 2,AK47 2,Mabegi 10 ya nguo,a/c zangu zina kama bill 900tsh,pete 5 za dhahabu,mikufu 7 ya dhahabu,nyumba 8 ziko arusha na 5 zko niwi yoki.
 
Magunia 8 ya mahindi, debe 21 za nyanya ila zinaweza kuharibika sio muda mrefu kwa kukosa soko,Kuku kama 100 wanaweza wakafa wote muda si mrefu kwa kuwa wanakideri,Maharage gunia 4 ila yamegongwa sana muda si mrefu ninawza nikayatupa,Alizeti gunia 9 ila panya wananisumbua sana wanaweza wakanibakizia 2 mpka mwezi ujao kwangu ndo mali zangu mkuu
 
senator tunakuundia tume
mzinga hayo mazao hakuna kuuza nje nchi ina njaa
 
hapa tatizo sio kutangaza hizo mali, unatakiwa pia kueleza ulizipataje. Kama ni urithi, utueleze umerithi kwa nani na ulikuwa na haki kisheria ya kurithi hizo mali?? hasa kwa kiwango utachotaja??? kama ulinunua utueleze fedha ulitoa wapi????? eleza na risiti ulikohifadhi, na duka au mahali uliponunua panatambulika kisheria au ulijinunulia kiholela kwani manunuzi yote ya kiholela hayahesabiwi, ni vigumu sana kudhibitisha inawezekana mali ilikuwa ya wizi!!
 
namiliki shamba robo heka huko kileleni mwa mlima sofe,viatu used pea 2 jumla 4000,gauni 3 za mtumba za marinda na mikanda nyuma jumla 3000 na baiskeli ya foenix niliyoachiwa urithi na baba yangu mwaka 85.
 
namiliki magunia 9 ya bangi mabegi 21 ya madawa ya kulevya aina ya cocain madumu 78 ya gongo. thaman ya vi2 vyote nitawaletea baada ya kufunga hesabu katika danguro langu ambalo lipo maeneo ya buguruni vijana wakimaliza kazi
 
Wakuu mimi namiliki madini yote yaliyoko chini ya aridhi, nimeachiwa urithi na mwenyezi mungu.
 
Magunia
8 ya mahindi, debe 21 za nyanya ila zinaweza kuharibika sio muda mrefu
kwa kukosa soko,Kuku kama 100 wanaweza wakafa wote muda si mrefu kwa
kuwa wanakideri,Maharage gunia 4 ila yamegongwa sana muda si mrefu
ninawza nikayatupa,Alizeti gunia 9 ila panya wananisumbua sana wanaweza
wakanibakizia 2 mpka mwezi ujao kwangu ndo mali zangu mkuu
Hujasema unamiliki panya wangapi mkuu.
 
hapa tatizo sio kutangaza hizo mali, unatakiwa pia kueleza ulizipataje. Kama ni urithi, utueleze umerithi kwa nani na ulikuwa na haki kisheria ya kurithi hizo mali?? hasa kwa kiwango utachotaja??? kama ulinunua utueleze fedha ulitoa wapi????? eleza na risiti ulikohifadhi, na duka au mahali uliponunua panatambulika kisheria au ulijinunulia kiholela kwani manunuzi yote ya kiholela hayahesabiwi, ni vigumu sana kudhibitisha inawezekana mali ilikuwa ya wizi!!

kweli kuna watu wamerithi mali za wajane humu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom