Wadau na wajasiriamali, naomba kujuzwa kuhusu Mr. Kuku Farms na uhalisia wa aina ile ya biashara

Jana bi mkubwa kanitumia voice note eti kuna mmoja wa wadau mr.Kuku amewaambia benki kuu wamezuia account za Mr.Kuku hivyo wasihofu pesa zao walizowekeza zipo lakini benki kuu wamezizuia kwa uchunguzi zaidi.Ni bahati huyu ni mzazi wangu.vinginevyo...... acha tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio mbaya ila si tutakuwa tumejificha kwenye discovery 4's na nyumba tunazo mpaka hio time ikifika.🤣🤣🤣 ama we unaonaje?

Hahaha nani asiependa mambo mazuri,kwa mwendo huu wa mr kuku hizo discovery miezi 6 tu tumeshazipata,watu wame invest 10M na kuendelea aisee Kuna watu hawajui wapeleke wapi pesa zao tuwasaidie tu
 
Juzi kuna jamaa yangu kanipigia simu akawa ananieleza vitu sivielewi elewi.

Ni kitu kinaitwa Mr. Kuku Farms akidai ni mradi mkubwa wa ufugaji kuku una physical presence na ni kampuni iliosajiliwa ndio inaendesha huo mradi.

Yeye ameshawishika kuwekeza huko kwamba kuna faida nzuri compared na kuweka hela benki tu ikiwa baada ya miezi 3 unaweza draw 70% ya ulichowekeza na baada ya miezi sita una uwezo wa kuchota 100% ya pesa yako.

Kama tujuavyo kwamba mtu alieng'atwa na nyoka huwa haishi maseke hata anapotambaliwa na jani, basi lazma atarusha miguu tu.

Naomba kwa heshima na taadhima niambiwe na wadau wenzangu wajasiriamali kwa wafanyabiashara. Je, huu mradi ni halisi?

Ni business model gani wanatumia? Na je, kuna hiyo leverage ya kupelekea kutoa gawio kwa rates hizo kwa muda wanaodai wanaweza?

Kama kuna ambaye amepiga hela kupitia hao jamaa aje amwage terms zao na ushuhuda kuwa kapiga dough kweli.
ni upatu.

kama sifa ya upatu wowote ilivyo, itafika mahali mnyororo utakatika na ndiposa kutakuwa na kilio cha kusaga meno.

ole wenu!

Hosea 4:6
 
Hahaha nani asiependa mambo mazuri,kwa mwendo huu wa mr kuku hizo discovery miezi 6 tu tumeshazipata,watu wame invest 10M na kuendelea aisee Kuna watu hawajui wapeleke wapi pesa zao tuwasaidie tu
Kama ni mwendo wa million 10/10 usishangae jamaa wakawa wamepiga hata B5 kisha wakapotelea kusikojulikana 😁😁😁

Yani miezi 6 mingi wakija watu 20 wanaoweka hadi 20- 50M mnatoka ndani ya miezi 3 tu😂
 
Jana bi mkubwa kanitumia voice note eti kuna mmoja wa wadau mr.Kuku amewaambia benki kuu wamezuia account za Mr.Kuku hivyo wasihofu pesa zao walizowekeza zipo lakini benki kuu wamezizuia kwa uchunguzi zaidi.Ni bahati huyu ni mzazi wangu.vinginevyo...... acha tu

Sent using Jamii Forums mobile app
kumbe pesa zilikuwa kwenye accounts nikafikiri zinazalisha kuku!
 
Kwa 'idea' ya Mr. Kuku ilivyo ni kama kitu kinachoitwa 'Crowdfunding'.. yaani anatokea mtu anakuja na 'idea' yake ya biashara halafu wanatafuta watu wengi(wawekezaji) ambao watatoa fedha ili kuiwezesha hiyo biashara na kunakuwa na 'platform' ya kuwaunganisha ambayo ni biashara ya kuku.
Ukishawekeza fedha zako na wao(Mr. Kuku) wataanza kufuga kuku na kuuza na wateja wakubwa wanakuwa hao hao waliowekeza pamoja na wengine. Kwa hiyo ijapokuwa umewekeza fedha lakini unalazimika kununua kuku, nyama ya kuku, mayai,vifaranga ili kuharakisha faida. Ina maana ikipatikana faida mtagawana lakini ikitokea hasara mtagawana pia.
Kwa nchi zilizoendelea inaaminika sana.

Hapa Tanzania ina changamoto sana hasa kwa wawekezaji kwani:
  1. Hupewi vitabu vya fedha('Income stat. & balance sheet') kujiridhisha kama faida inapatikana.
  2. Gharama ya uhakikisho ni kubwa('Due diligence costs').
  3. Gharama ya ufuatiliaji wa mradi('monitoring') siku kwa siku ni kubwa kwa mwekezaji.
  4. Taarifa zinazotolewa ni za kuvutia na za upande mmoja('information assymetry').
Kwa hiyo miradi kama hii ni rahisi sana kugeuka na kutumika kama vichochoro vya kutakatisha fedha au 'Ponzi Schemes' kama Serikali haitaingilia kwa kuweka kanuni zinazoeleweka ikiwemo kuweka sehemu ya fedha za uwekezaji kama dhamana Benki Kuu.
 
Anaitetea Kampuni Yake Lakini Acha Tuone Serikali Lazima Itaibua Jambo Tu Maana Ufafanuzi Upo Upande Mmoja!!
 
Back
Top Bottom