Mr. Kuku Farm ni aina mpya ya DESI?

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,109
18,326
Kuna jamaa wanaitwa Mr Kuku Farms, wanasema wanafanya ufugaji wa kuku na wanahkmiza watu kuwekeza kwa ahadi kwamba unavuna mara 2.

Nimeona wamepost na shuhuda mbalimbali motomoto kama zile za kwa mwamposa. Mmoja anasema aliwekeza sh laki 3.5 na anategemea kuvuna 8M.

Swali nalo jiuliza kwanini iwe rahisi kupata fedha kiasi hiki kwa muda mfupi kuliko bank yeyote au soko la hisa?

Napata wasiwasi isije kuwa ni DESI imerudi kiani maana huwezi pata mara 2 kirahisi hivi wakati kuna makampuni yanafuga kuku nanyanapata hasara.

Naomba kwa yeyote anaye jua hawa Mr kukus ni wafugaji kweli wa kuku?

Je, kama kuna mtu amesha fanya nao uwekezaji , atupe ushuhuda wake motomoto?

Je, kwanini kama ni biashara ya uwekezaji wasifanyie soko la hisa DSE?

Serikali ipo wapi kutoa ufafanuzi wa jambo hili walau watu tufuse million kwa myda mfupi.

Kwa wale ambao mnataka kuona shuhuda motomoto tembelea instagram Mr_kukus

Nataka nijitose kwa kuwekeza mil 2 ili zikisha komaa nihune kama mil 80 ndani ya miaka 2.

Sent using Jamii Forums mobile app


UPDATES 10 August 2020

Mfanyabiashara Tariq Machibya maarufu kama Mr. Kuku, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka saba likiwemo la kufanya biashara haramu ya upatu kwa kukusanya fedha za umma zaidi ya Shilingi 17 bilioni. https://t.co/9Ik6wUGj55
 
Kama hao wadau wamekuja na gia hiyo feki na kujiita Mr. Kukus kwa maana ya kificho kuwa wanahitaji ma Mrs. Kukus ilikufanikisha dhamira yao kuwatotolesha hasara na hatimaye kuwaacha solemba.

Mtu yeyote yule akikutangulizia taarifa ya "deal" yenye "return" kubwa bila ya kugusia "factors" nyingine muhimu kama vile "operating risk" kaa mbali naye na muogope kama ukoma.
5a8f097f1e000017087ac8b2.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza kulikuwa hakuna haja ya huu uzi kwa sababu umeshatoa hukumu tayari kwenye kichwa cha uzi ila unatafuta watu wa kuja kujumuika nao muwakatishe tamaa wengine.

Pili wewe sio muwekezaji unapendeza zaidi ukiwa umeajiriwa kwa sababu unaonekana una woga mwingi kupita kiasi kitu ambacho hakitakiwa katika uwekezaji.

Mkiletewa fursa za kilimo mnasema hakuna uhalisia ni kilimo cha instagram, ufugaji nao hamuutaki, biashara mnaleta vitisho kwamba hakuna mzunguko wa hela, mkiletewa fursa za mitandaoni mara kina ontario.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom