Uchambuzi wa ziara ya Rais Samia aliyoifanya Davos na Dakar, Bashe amtaja Mr Kuku kuwa anafuatiliwa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Zuhuru Yunus pamoja na Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe; Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Gerald Geofrey Mweli pamoja na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mazao, Wizara ya Kilimo, Nyasebwa Chimagu wakizungumza na vyombo vya habari kuhusu ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan nchini Uswizi na Senegali katika Ukumbi Wa Jakaya Kikwete - Ikulu jijini Dares Salaam tarehe 30 Januari, 2023.


Yunus.jpg

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu Zuhura Yunus


Bashe:
Takwimu za sasa zinaonesha ikifika mwaka 2050 Dunia itakuwa na watu Bilioni 9 na kati ya hao Bilioni 2 itakuwa wapo Afrika lakini kwa takwimu za sasa Dunia ina watu takribani milioni 800 waliopo kwenye njaa na moja ya tatu ya watu hao wapo Afrika.

Bashe.jpg

Bashe

Lakini tuna zaidi ya 65% ya ardhi ya kuzalisha chakula lakini haijatumika.

Sisi Tanzania tunatarajia kufikia mwaka 2030 tutakuwa na watu milioni 80.

Eneo la kilimo ni zaidi ya hekta milioni 44 na si tunatumia si zaidi ya hekta milioni 10, eneo linalofaa kwa umwagiliaji ni eneo si zaidi ya hekta 29, kwa miak 60 tumeweza kutumia 2.7% ya hiyo milioni 29 na inaonekana eneo linaloweza kutengeneza ajira ya uhakika ni eneo la kilimo.

Serikali ya Awamu ya 6 tangu iingie madarakani imekabiliwa na changamoto kubwa 4 ambazo ni; COVID-19, Vita ya Ukraine, mabadiliko ya tabia Nchi na gharama za mafuta Duniani.

Gharama za maisha zimeoanda kutokana na mazingira hayo.

Mwaka 2020 fharama ya kusafirisha mahindi au mchele gharama zimepanda kwa kuwa gharama ya mafuta pia imepanda.

Serikali ya Aawamu ya 6 inachukua hatua mbili, kwanza ni kutoa ruzuku ya mafuta, mbolea na kwenye mbegu.

Pili, naelewa concern ya Watanzania kuwa sisi hakututakiwa kulalamika, lakini mwelekeo wa Serikali ya sasa ni mipango ya muda mrefu, tumeamua kuwekeza miundombinu ya uzalishaji ilitusipate shida ambayo tunaweza kukabiliana nayo.

Tazameni takwimu za mwaka 2018 hasa mazao ya nafaka, kumekuwa na tabia ya bei kupanda hasa mwezi wa Oktoba hadi Februari, lakini mjadala wa Nchi tujadili tija na tusijali bei.

Kuhusu hofu ya maeneo ya kilimo ni kweli kuna migogoro baadhi ya sehemu ya wakulima na wafugaji, Nchi yetu ina hekta milioni 44, tumetumia hekta laki saba na kitu, kuna hekta nyingi hatujazitumia.

Kuna vijana 16,000 walioomba online, tunawachukua kwa ajili ya kwenda kuwafundisha kilimo biashara hata kama wametoka vyuoni.

Watafundishwa kwa kipindi cha miezi mitatu hadi minne bure, baada ya hapo atapewa kipande kisichozidi heka 10 na tutamwezesha.

Mpaka tunafikia hatua hiyo tayari Serikali tunakuwa tumeshaandaa mazingira na kutengeneza mazingira mazuri ya miundombinu, kama ni mbegu atapata na mtaji atapata, ili kuondokana na kasumba kuwa kilimo ni adhabu.

Tunataka kubadilisha kilimo kutoka kwenye dhana ya kuwa ni adhabu.

Kwa mara ya kwanza katika historia, miradi yte ya umwagiliaji iliyotengewa bajeti imeshasainiwa na baada ya miaka miwili tutaanza kuzindua hii miradi.

Mazao ya wakulima ni haki yao, wana hai ya kuyauza popote, Serikali kama tunahitaji tutaenda kuyanunua kwa bei iliyopo, lakini Serikali tutachukua hatua kwa lengo la kumlinda mlaji, mfano tutanunua chakula na kukiuza kwa bei nafuu kwa walaji.

Sasa hivi uwezo wetu wa kuhifadhi umeongezeka kutoka tani 200,000 hadi tani 500,000, hivyo katika msimu wa kuvuna tutanunua mahindi sana na mahindi sana tutahifadhi lakini hatutazuia Mkulima kuuza mazao yake popote,

Na mazao yakianguka serikali itayanunua kwa bei nzuri kama tunavyofanya sasa.

Mfano sasa hivi vijijini kwenye Halmasharauri tumeanza kujenga vituo vya kuuzia mazao, wakulima watavuna na kwenda kuuza ili tukifanye kilimo biashara.

Niwakumbushe tu kuwa hatua hizi tunazochukua sio za matokeo ya kesho, ni mchakato, mabadiliko ya kilimo ni mkakati wa muda mrefu.

Rais aeamua kuunga mkono sekta binafsi kwa ajili ya kuzalisha mbolea na chokaa.

Serikali imeamua kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina, mabone yote ya Nchi nzima yanayofanya kwa kilimo, mwaka huu tutatumia Bilioni 36 kwa usanifu na upembuzi yakinifu kwa mabonde 22 ya kwanza katika Nchi yetu ili tuweze kutumia rasilimali za maji ambazo hazihitaji kusubiri mvua, tuwe na uhakika wa uzalishaji.

Kwa sasa tunakua kwa 4%, kwa hatua tunazozifanya, kufikia 2050 asilimia 50 ya shughuli za kilimo zitaendeshwa kwa umwagiliaji, hivyo tunaamini kilimo chetu kitakuwa kwa 10%.

Serikali inamfuatilia Mr Kuku
Serikali imetoa angalizo kwa watu wanaojihusisha na kilimo kuwa wanatakiwa kuwa makini na kuacha kuamini kilimo cha mtandaoni badala yake wanatakiwa kufanya kilimo kwa matendo.

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema "Tunatoa uelewa acheni kulima kwa Twitter, Instagram na What’sApp, hakuna anayeweza kukuambia lete milioni 10 na baada ya mwezi utapata 15.

Ameongeza kuwa “Katika kilimo hakuna njia ya mkato, kama una hela nenda kanunue ardhi, ajiri kijana wa chuo kikuu, zalisha, Wizara tumepokea makalamiko mengi kuhusu Mr Kuku.









 
Mi naona huwa anaenda kutimiza takwa la kuhudhuria vikao lakini mateo yake hata kama angepiga simu yangetokea tu .

Matumizi makubwa kuliko mapato yatokanayo.
 
Uzi mchungu kwa BAVICHA huu, sasa hivi wanafanya maombi umeme ukatike tusisikie faida ya ziara ya Madame President kutoka kwa Bi.Zuhura Yunus
 
Back
Top Bottom