Ila tuache kuwalaumu sana. Ukipanga nae kutoka na akakukubali fanya basi hata kumrushia pesa ili ajiongeze mwenyewe na kuja kwako akiwa msafi vile utakavyo wewe. Unajua mwanamke nae ukiwa unamuhudumia vizuri, nae atajitahidi kujiweka katika mazingira ya kukuridhisha. Lakini wewe unaita tuu, unapiga na kusepa, humpi chochote, humfanyii chochote, na ukimkuta ni zaidi ya vile unavyotarajia, yani msafi sana na anapendeza wakati haumuhudumii kwa chochote, unaanza maswali, umepata wapi, nani kakupa, blah blah blah kibao.