Mange, Mbonie Masimba, Sinta & Shamim Mwasha, Kumenuka

Muke Ya Muzungu

JF-Expert Member
Jun 17, 2009
3,448
0
[h=1]UKWELI WA MAMBO........[/h] I had a busy day leo mpaka basi ndo maana mnaona sikuapprove comments zenu. I was just sooooo busy...... Ila sasa hivi nimetulia nipo ndani ya ndege na familia yangu tukielea L.A. Ndo nkona niblogue sasa.
Unajua nini mwezi wa Ramadhan hamzuii mtu kusema ukweli kwa hiyo acheni niongee.


Nimeoingia online tu natumiwa link nimeingia naona watu au hata labda inawezekana ikawa ni mtu mmoja tu kaandika zote si mnamjua yule hamnazo alivyo. Anyays, it doesnt matter kama comments kaandika mtu mmoja au wameandika wengi au kama Sinta mwenyewe kaandika ili watu wamwonee huruma sijui ila what matters is mtu ambae hajui kwanini nilifanya vile jana anaweza kuniona mimi ni mtu mbaya sana, nina wivu na wanawake wenzangu, ninawavunja moyo na kuwaharibia majina yao. Kwa kweli siwezi kukubali kuwa na kashfa kama hii sababu mimi ni mgombea mbunge mtarajiwa wa jimbo la Kawe kupitia Chama Cha Ukweeeeeee ,CCM. Nimeona bora nijiteteee angalau.
Nawaomba sana baada ya kusoma ntakachokiandika ukipenda kutuma commnets tuma comments zenye busara na kujenga tafadhali usitume comments za kumdhalilisha mtu.
Like i said malalamishi yanatembea mimi nimeamua kumuumbua Sintah kwa kutangaza kuwa kachukua mkopo access bank sababu sijapendezewa na yeye kufungua duka, nina wivu etc. Naomba mjue kwamba huo sio ukweli hata kidogo.
Hizi taarifa za Sintah kuchukua mkopo nipewa kama mwezi au miezi miwili iliyopita kupitia mtandao wa FB na alinieleza kuwa amekasirishwa sana na comments ambazo bibie JLO TZ alikuwa ameweka siku hiyo kwa hiyo akanipa hiyo data ili na mimi nijibu mapigo. Nilimshukuru huyo dada kwa habari nilimshukuru sana sana mpaka kwa mapenzi aliyoonyesha kwangu sababu aliamua ku risk kazi yake sababu yangu mimi. Although kuna wanaoniona mimi ni mpenda ugomvi na kubully watu nilimweleza huyo dada sitaki kuweka hii habari sababu ni serious sana yeye maneno anayoniandika ni ya kitoto im sure watu wameshayazoea so nitamwacha aendelee.Nikakaa kimya.
Im sure wote mtakubaliana na mimi kuwa toka last time balaa lilivyozuka ikawa vita ya karibia wiki nzima nilisema sitaki ugomvi and i tried my very best to keep my word, Ila mwenzangu yeyee aliendelea kunidonyoa donyoa kidogo kidogon nikasema mwache ajifurahishe na hata siku moja sikuweka comment humu kuhusu yeye sababu mimi nikishamdharau mtu yani huwa nasahau kama yupo hai.
Huyu SInta ananitafuta kwa shari on a daily basis, yani hanipi hata day off mutoto wa kike. Alikuwa anadiriki mpaka kuweka comments za link kuwaonyesha watu eti kuwa nguo zangu nanunua naweka label, anaweka comments vitenge vyake ni feki. Akawa anaweka comments za BEDUI Mange anaishi hapa kwenya watu maskini, hivi ile address ingekuwa kweli ni yangu ningedhuriwa je? We all know how much BEDUI hates me ,angekuwa nauwezo angesha hire hitman animalize. Nikaenda zangu L.A mwenyewe nikaona nijishebedue mnione babkubwa nikaenda kwa jirani yangu nikapiga picha ndani kwake nikawaekewa, mkanisifia weeee, mara akaweka comment za kuniumbua kuwa nakaa kwenye ki apartment , maneno kibao.aliniumbuaje sasa??? LOL...
Mnakumbuka nilivyokuja US nikaweka porche yangu nawaringishia, bidada akarusha macomment gari yenyewe ya mkopo, akawa kila akipiga picha chini anaandika siishi kwa mkopo. Maskini nilikosaje raha kaniumbua gari la mkopo. Imagine mpaka alidiriki kuweka comments kuwa muke ya muzungu mimba imeingia chooni. Imagine wakati anaweka hii comment taayri nilikuwa najua mambo ya mkopo na nilikuwa nakumbuka anavyosema haishi kwa mikopo lakini stili nilijikaza nikasema bwana eeeh mwache kila mtu ananijua mimi taifa kubwa sina haja ya kumjibu. Sasa alivyofungua duka ndo akadata kabisa comments zoote ni muke ya muzungu alikuita mlala hoi aone sasa, muke ya muzungu atakuheshimu sasa, yani ni kama vile alifungua duka kwa ajili yangu mimi. Imagine hata baada ya hapo nilijikaza sikutaka kutoa hii infomation, ou know why? i though to myself, God has blessed me so much more than her and i know deep down she doesnt hate me but rather she wishes to have what i have kwanini nisimwache aenjoy this moment? kumbuka hapo just a weeka before yeye hakutaga hata nii enjoy mashauzi yangu ya kuwadanganyia ile mingazi kumbe nimeenda kwa jirani kwenye lobby ya watu woooote nkajifanya kwangu. Akaniumbua fasterrrrrrrrrrr.LOLEST.....
Maskini ya Mungu mimi i was sooo happy for her nikasema Mungu sitomwaribia huyu mtoto swagga zake amestruggle sana kutafuta status mujini, kapitia mengi mnoooo ili aonekane na yeye yupo juu,nikasema her dream has come true, although alikuwa ananibeza anasema yeye haishi kwa mkopo..... Na pia mkopo sio kitu kibaya at all. Mkopo ndo sababu kubwa ya watu wa nchi zilizoendelea kuweza kuishi maisha mazuri. Ningekuwa mtu mbaya mimi ningejitumia hata comments za kuwataarifu kachukua mkopo tu huyo na msingejua comment nimetuma mimi ila sikutuma hata comment sbabu i wanted her to enjoy her moment. Kweli unaweza kuniita mimi mtu mwenyewe wivu ? Choko choko zoooote alizonifanyia SInta and still niliamua kumstiri kama mwanamke mwenzangu ili aipate ile heshima aliyokuwa anaitafuta muda mrefu. Hapo anavyoshangalia furaha yake na kuringishia watu bado comments zote ni za kunishushua mimi tu na bado nilijikaza.
Sintah akaona mbona huyu Mange hatikisiki jamani akaona atoke na style ingine,ndo jana akaamua kuweka comment ya BEDUI ya kumnanga mwanangu. Hapa ndo niliposema ok now im justified.Chief, ukishatukana mtoto wa mtu all bets are off. Bedui kama nikiachia comments za kumtukana mwanae ni sawa tu maana BEDUI alikuwa anatukana wanangu facebook tena kwa jina lake bila woga. Pale waliponitajia Bhoke wangu bila haya wala huruma ndo nikasema ngoja nijiachie.
Sasa leo anaweka comments sijui anaziandika mwenyewe au vipi eti Sintah mlilie Mungu, Mange anajifanya tajiri wadunia, Mungu atamlipa. Nyie wajinga sikilizieni. Kama huyo Mungu wenu ndo Mungu yule yule aliemuumba mwanangu basi dua zenu hazinipati ng'oooo. Mumtukane malaika alafu mama yake awajibu then ndo mkumbuke kumlilia Mungu wajinga wakubwa. Nyie mtaadhibiwa kwanza then ndo ntaadhibiwa mimi.
Sasa kwa wale mnaojifnaya mnajua sana kunikosoa na kunisema je ingekuwa ni wewe Sintah kakufanyia hivi, je usingefanya nilichofanya mimi? MNIKOMEEEEEEEEEE NA MUMKOMEEEE BLACK BEAUTY WANGU..... Sinta nakurudia tena kwa vile mtoto wako anahitaji privacy zaidi ya watoto wa Klyn so huwezi kumwonyesha kwenye internet angalau tembea nae, angalau nenda nae kwenye birthday party na wewe uonekane mama.Kama yupo Uganda kamfate uende nae Dar ukae nae hata holiday tu uwe a proud mother even for a day. UKIWEZA KUFANYA HILO IM SURE UTAUJUA UCHUNGU WA MWANA NA UTAACHA KUNITUKANIA MWANANGU. MAANA A FEW MONTHS AGO ULIDIRIKI KUMTUKANA KWENYE POST YAKO. Naelewa kwa nini hujui ubaya wa kumtukania mtu mtoto ni kwa sababu wewe una moyo mkavuu wa kuweza kuishi maisha huku ukimficha kiumbe wako, kiumbe uliembeba mienzi tisa na kumzaa kwa uchungu. Im sure hata kama nikiamua kutumua data za yule dada alizonitumia siku zile kuhusu mtoto wako nikamchambua mtoto wako im sure hutoumia at all, yani sidhani hata kama utaajali maana hutaki hata kuwa mama yake, im sure ungeweza kumgawa ungemgawa fasta. Hata kama baba wa mtoto wako akijulikana itakuchafua sana still sio sababu ya kumchukia mtoto wako. YES, WAMESHANITUMIA MPAKA DETAILS ZA BABY DADDY WAKO ILA NITAKUSTIRI SABABU WEWE NI MWANAMKE KAMA MIMI SINA HAJA YA KUKUAIBISHA AU KUMUAIBISHA MTOTO WAKO. ILA BE CAREFUL SINTAH CHUNGA HILO DOMO LITAKUPONZA........USITAKE KUREKEBISHA TABIA ZA WATU WAKATI WEWE YAKO NDO INAHITAJI MAREKEBISHO KWANZA.
IM DONE NA CHAPTER YA KUKUPA USHAURI. SOMA VIZURI SIJAKUTUSI WALA KUKUDHARAU KAMA NILIVYOFANYA LAST TIME, ILA NIMEKWAMBIA UKWELI UKIPENDA UFANYIE KAZI USIPOPENDA UPOTEZEE.... SASA NAINGIA KWENYE KIPENGELE MUHIMU SANA.....MWENYE MACHO NA AYAONE....
Unajua mara nyingi binadamu tunakuwa hatumalizi matatizo yetu sababu tunakuwa na haraka ya kudeal na tatizo bila kuangalia chanzo cha hili tatizo ni nini. Huyu SInta akiulizwa na mtu kwanini unamchukia Mange sidhani kama atakuwa na jibu la msingi. kwa kweli sidhani.Sasa jiulize kwanini SInta amekuwa Adui yangu mkubwa? ngoja niwapeni mambo ya mujini leo.Swaumu haikatazi kuongea ukweli inakataka kuwa mshari though.
Mnakumbuka that first trip nimerudi Bongo for the 1st time, kutua bongo tu kesho yake naamshwa naambiwa sinta kaweka macooment huko ya ugomviii. Nikashangaa huyu ananini? ofcourse ndo siku zile hakuna mtu anajua blog yake so akawa anaindika kwa chati ili watu wakasome. Sikumchelewesha nikimpigia simu shamim Mwasha sababu nilijua anaurafiki na SIntah nikamwabia naomba number ya Sinta, akanipa nikaruka hewani fasterrr, Nilimfurumushia Sinta matusi kama yake ya Wema kwenye ile video, ila nilikuwa nna hasira sana so full kigugumizi sidhani hata kama alikuwa ananielewa, yani angenirekodi siku ile kama Diamond alivyomrekodi Wema akanirusha mngecheka mpaka mlie machozi....lol...Sintah akawa mpoleee akanijibu kweli kuna comments sijaona ngoja nazitoa Mange, na ukweli akazitoa in 5 mins. Na kesho yake akaamka akawashushua msinigombanishe na Mange tumejuana toka enzi za polisi wanavaa kaptura...hahahahahahhahaha... Alfu ni kweli nimemjua Sinta toka nipo Chuo first year aliwahi hata kuja kunitembelea mabibo hostel.
Basi yakaisha maisha yakaendelea akaacha kunifatilia issue zangu. But after about a week tu ndo akaibuka na matusi ya kunitukana mara 10 ya before, yani kama alikuwa kapagawa na kitu, akawa kama vile adui yangu. Nikaa kimya coz nilikuwa nisharudi US. Then 2 months later nikarudi Bongo.The day nimeingia Bongo naamka tu Sintah akaweka yale maeil ya mimi kumcheat mume wangu. Nikamtwangia Shamim tena nikamwmabia Shamim mwambie Sintah hata anitafute vipi siwezi kumwandika kwenye blog au kumjibu sababu she is not my class yani mimi kugombana na SIntah ni kama Beyonce agombane na Cassy wa Pddy atakuwa kajishusha mnooo. SO atajijua, Shamim akacheka alafu nikamwmabia yani last time nilimtukana akaogopa akatoa akajifanya msinigombanishe na Mange, Shamim akastuka akaniuliza ulimtukana? nikasema ndio?akasema wewe mwenzio kaniambia ulimpigia ukamwambia unaomba atoe hutaki mgombane, ukamwomba msameheane, ndo akakuonea huruma,. Nikachekaaaa nikamwambia uwiiiii kawadanganyajeee nani amwombe yule? hana hadhi hiyo.Kesho yake nikamuuliza hivi Sinta anafnaya wapi kazi akanijibu anasemaga yeye ni secretary wa Manji ila sijui ofisi zao. nikasema poa.maana mpaka hapo nilikuwa nimesema haya mambo ya internt ya kitoto ngoja nikamfate face to face tumalizane. Still nikawa na avoid kurespond kwenye blog maana ingekuwa kubwaa balaa so nikampigia tena Shamim, Shamim akanijibuje aah mie siongei na Sinta bwana nimechoka, ila Mange unajua kwamba wewe ndo ulianzisha hii style ya kutukana watu kwenye blg? Sinta anakuiga tu ila wewe mwneywe ndo ulianzisha. Nikamwmabia Shamim sikatai mie ndo nilianzisha hiyo ila mind you naandika mtu alieniletea shobo sio mtu ambae simjui hanijui. Mtu mzima akikutana sio lazma akwambie shenzi, nikaelewa pale pale Shamim anachosema ni kwamba i deserve yale matusi Sintaha aliyotukana sababu mie ndo nimemfundisha Sintah hapo mambo.Baada ya kupata jibu la shamim nikajua kimenuka tayari, mpare kama mnavyonijua sio zoba nikajumlisha moja na mbili, nikamtwangia mtu huyo mtu alikuwa anajua story yoooote kwa kuhadisia na Sinta yeye ndo akanipa mkanda mzima.
Sasa this is what happened....... Mnakumbuka nimesema first time nilimpigia Sintah nikamtukanaaaaaaa matusi ya nguoni akaogopa akatoka comments na kesho yake akawashushua mukome kutugombanisha??? To be fair alivyoandika ile SInta alimaanisha na alijiskia vibaya na tuka move on na maisha. Sasa guess what changed things? Si mimi nilimwambia shamim kuwa nilimtukana Sinta atoe makoment akaogopa? Shamim akamtwangia Sinta, shoga mbona ulisema Mange alikuomba msamaha kaniambia alikutukanaaaaaaaaaaa, ukawa mdogo kama piriton, anasema ulitetemekaaaa yani alikukomesha. Sasa kama mnavyojua kila binadamu kaumbwa na pride na yeye Sintah akaona kwanini nimejigamba? Ndo sasa ikabidi amuonyeshe Shamim na wapambe wengine kuwa haniogopi. Shamim akamwambia kuwa nimesema mimi ni beyonce siwezi kugombana nae, Imagine sikusema mimi Beyonce nilimdharau ofcourse ila maneno yalirembwa zaidi. Akamwambia pia kuwa nilikuwa namuulizia anapofanya kazi au anaopishi, so huko JLO TZ akapandisha mzuka balaaaa ndo akazidisha mara elfu nane kunisengenya. Ila mie nilijiuliza hivi what has changed since Sinta kuniomba Mange natoa na kuweka ile article kuwaaambia Najuana na Mange long time na ghalfa kubadilika vile nilijua lazma kuna kitu but nilikaa kimya.
So as much as yule Sinta ni mtafuta shari muda wote ila mwisho wa siku ugomvi wangu wooooooooooote ule na JLO usingetokea kama sio Shamim Mwasha. Shamim ndo aliepanda mbegu na mzizi wa fitna. Kwa wale mliokuwa mnanisema kuwa mimi ni m mbaya kwa nini niachie comments za kumtukana mume wa Shamim na maswali mengine kibao. Naombeni mkae mkijua kuwa mimi sio kichaaa siwezi eti kuanza kumtukana mtu eti sababu harusi nzuri eti nna wivu. Chief sina wivu na pesa sembe.....lol... Ila kwa kweli niliona kwamba nimetukaniwa wazazi wangu,ndugu zangu,biashara yangu, wanangu, mimi mwenyewe, na Sinta katukaniwa mama yake, mtoto wake na yeye mwenyewe wakati alisababisha katulia pembeni anajifnaya dada wa heshima. Nikaona bora na yeye atukanwe ajue utamu wake. Alafu akiulizwa na watu huko bongo kwanini Mange anakufanyia hivi? anajibu si mnamjua Mange ana matatizo yani sijui nilichomkosea itakuwa ni sbabu Sintah alivyomchamba alinitaja jina langu na nilimwmabia Sinta atoe jina langu wasinihusishe Sinta hakutoa nilichukia sana.
Sasa ndo mjua hawa wadada mnaowaona wana heshima zao hawagombani na watu blog zao hazina matusi mkadhani wanafanani na blog zao. Ni mafisadi na mahasidi , wanafki , waswahili , wapenda ugomvi kushinda Mange na Sinta. Bora Mange Kimambi nawaonyesha tabia zangu ubaya wangu na uzuri wangu kuliko hawa wanaokaa kujidai ni wenye heshima kwenye jamii kumbe kasheshe zote zinazotokea kwenye jamii ni kazi yao.
Shamim mimi sipendi unafki kama ulikuwa hunipendi ulikuwa unanichekea ya kazi gani? nILIKUWa nakupa wewe malalamiko ya Sinta sababu na mimi nilidanganyika kama jamii yote nikawa nkuona mtu mwenye hekima nikasema ngoja Shamim ayamalize chini kwa chini kuliko na mimi kwenda kwenye blog kumjibu Sinta nikanufaisha watu, Kumbe nilikuwa nimeingia choo cha kike bwana, badala ya kusulihisha anatengeneza balalaaa. Wewe mtu umeshaona kwamba Sinta kaweka post kwamba sina tabu na Mange kwanini usifuahi ukaayache, hata kama Sinta alikuwambia Mange alinilamba miguu ndo nikaona nitoe macomment ulikuwa na haja gani kwenye kumtia Sinta moto kumwambia Unamwogopa Mange Kasema amekutukana mpaka ukatia akili? hukujua kama Sinta kama binadamu lazma na yeye angetaka kuwaonyesha nyie kuwa haniogopi? Ulijua sana.


dada wa kistaarabu uliemfano wa kuigwa na wanawake wengine. Kwa vile unataka kuonekana decent mbele za watu huku unachonganisha watu alafu unakaa pembeni ngoja niwafahamishe who you really are. Although umeweza kujipenyeza penyenza kwa nguvu mpaka ukaingia kwenye cirlce ya wadada wa mujini aisee wewe bado ni mwanamke wa uswahili hutokaa kuacha asili. Ndo maana ni mnafki.
Wewe mwanamke decent mwneye blog ya heshima umeolewa ndoa ya funika bovuuuuuuuuuuuu umewaeleza wanawake wenzio mume umemtoa wapi? Mambo ya wenzenu mnapenda kuyaweka wazi ya kwenu kimyaaaaa kisa muonenekani hamna drama. Naomba ueleze kadamnasi kwanini Mbonie Masimba who was your best friend, wa pika na kupakua hakushiriki wedding yako wakati alikuwa hapo hapo Bongo? Umewaeleza kuwa Huyu "businessman" wako alikuwa ni bwana wa Mbonie ukamwibia mwezio na kuua urafiki.,hata kama Mboni hakuwa mke ila umejua kama mtu wa Mbonie, umeemuza sana sana sana mwenzio. Unadanganywa watu kuwa hakuwahi kutembea na Mbonie , Mbonie ndo alikuwa anamataka, Mboni sio kichaa and you know what you will never admit ulichomfanyia Mbonie sababu wewe ni 'decent' Kutwa kunisema Ωmimi mgomvi , mimi nna matatizo chief maugomvi yangu yoooooooooooote im sure hujawahi kusikia nimfanyia mtu unyama uliofanya wewe. Yani wewe huo umgovi mmoja ni umefunika miugomvi yangu yooote.


Alafu ooooh women's day, wnanawake tupendane, tupongezane, wewe mwenyewe umeshindwa kumpenda shosti wako Mboni ukamwimbia bwana wake hukujali urafiki ili mradi upate mume mwenye pesa ndefu utingishe mji alafu unawaambia wenzio tupendane womne's day. Ingawa ulijaribu sana kuficha kila mtu anajua how close you were with Mboni na Mboni anajulikana ni mpenda mashughuli , sijui kama kuna harusi Mboni hajaenda mji huo, hata yangu alikuja maskini akachangamsha , hana wivu na mtu ukiolewa anakupa full support. Leo hii mboni hakuonekana kwenye shamra shamra za harusi unadhani ingebaki siri? Mdada wa watu mkampeleka invitation siku ya harusi...lol
Mboni usiumie mpenzi, malipo dunian, Karma is a bitch. Kwa sasa hivi jamii inakuheshimu kuliko yeye, hata kama huna maisha kama yake ila unajituma n apesa yako ni ya halali,usiumizwe roho wala usirushwe roho na mashauzi ya pesa zilizozajaa damu za vijaa wa Kitanzania na machozi ya kina mama wa kitanzania wanaowaliliwa watoto wao waliokuwa mateja.


Ulivyokuwa huna kitu hakuna aliekujali mjini kama huyo mbonie wengine wote walikuwa wanakualika for pictures basi. Umepata visenti wanakukenuliwa unawasahau waliokupenda enzi zile....Lol...
Narudi kwako Sinta, umejitafuta mabalaa kibao kwa kusikiliza maneno ya kumpapiwa , haya sasa ulivyomtaja jina lake siku zale alikununiajeeee???? sasa huyo ni rafiki? angekuwa anakupenda ange stand with you, ila hakutaka kujihusisha na wewe. Unachonganisha watu alafu ukitajwa hadharani kama mpeleka maneno uanijanya kumind ili tu umentain status yako ya u'decent'. Sinta penda unapopendwa na wewe usijipendekeze sababu sijui umepewa duka bure, unajua mwenyewe, Unaendaga Sea clif kula mwenyewe kwenye meza kama mchawi unaweka picha kwenye blog mbona usiende na dadako Shamim? Birthday walialikwa wenye class mwenzangu na mie hukupata mwanaliko sababu huna hadhi ya kukaa meza moja na wadada wa mujini, alafu bado unagombana na watu ili umuonyeshe Shamim we gangwe?
Kama ulikuwa hujui Dar hupati marafiki kama huna kitu. Umeona mwenzio alivyopata marafiki wa kona zote sasa hivi eeeh? sasa hata ujipendekeze vipi kwake, hata ufanye nini huwezi kupaka mialiko ya juu sababu wanakuona hujafuka.
Ila usingenitafuta maneno na watu wasingejua umepataje pataje hata duka la Wedding dresses hata wewe ungepata angalau shoga wa kwenda nae now. Ila ndo hivyo tena umeharibi mwenywe. Mwenzi hapa hata nigombane vipi na watu siwezi kukosa wa kula nae bata bongo....
sasa wewe mwenzangu na mie umejiingiza kwenye maisha ya kutafuta shari, mji mzima wamekuchukukia alafu ukiongeza juu ya hapo wanakuona huna kitu, chief utatembea peke yako mpaka basi, na mume ukimpata itakuwa bahati sana. usigeze ubabe wangu mwenzio nimejikamilisha.......shauri zako.....
Na kama unataka kufanya mashauzi uwaogopeshe kidogo mimi sina roho mbaya ya kutaka kutaka kukuumbia, ila sasa ukitaka kufanya mashauzi huku unanichokoza ndo hivi utakuwa unajiharibia.
SINA KINYONGO NA WEWE SINTA,NAJUA HAIKUWA AKILI YAKO ULIKUWA UNATAFUTA DUKA LA BIASHARA. I CAN RESPECT THAT. ISHI KWA AMANI.....


Nimemaliza jamani, sasa muache kuwasifu wadada wa mji huu sababu tu eti hawatukani wapo kimya mkiwajua mambo yao mtaona bora kina Mange.......
Wadada wa mujini na nyie kwa kupenda watu wenye pesa na kupapatikia harusi zisizo na michango, yangu ilikuwa na haki ya kupapatikiwa kwa kutochangisha sababu mume wangu anajulikana anafanya nini, ila nyie mnachetukaaaaaaaaaaaaaa na kupagawa na harusi ambazo hamjui pesa zimetoka wapi. Kuna siku mtajakuta mihela mliochetuka nayo ndo iliyosababisha ndugu yako kawa teja.... Mlikuwa mnamnyali before, sasa hivi mmemuona class yenu....lol.....


Shikamooni wakubwa, MSIJISTRESS KUSOMA HILI GAZETI PAPO KWA PAPO, TUMIA HATA SIKU MBILI MSIJE FUKUZWA KAZI MAKAZINI HUKO....


PS Narudia tena staki comments kijinga na matusi kama una comment naoimba uwe ya kiutu uzima,. Everyone is welcome to comment except you Bedui.Please take a break today, maana najua hii topic itakupandisha BP.....

[h=2]Joomla
Joomla
[/h]


[h=3]Comments (98)[/h]

 • [h=3]Shubira[/h] 18 July 2013 at 07:31 | #

  Nimesoma mpaka macho yakalia, Mange sikuwezi aisee, nakutakieni kila la kheri wewe na sintah Pia. Huwa naingia kote nasoma na namaliza siku yangu swafiii. Sipendi ugomvi basi tu, hope miyamalize salama.
  reply  • [h=3]Lala[/h] 18 July 2013 at 09:06 | #

   Dah! Okey [-O
   reply • [h=3]Muke ya mswahili[/h] 18 July 2013 at 07:44 | #

  Shamim poyeeeeee
  reply • [h=3]Anonymous[/h] 18 July 2013 at 07:46 | #

  Wadada wa mujini ni noumerr, mbwa mwitu ndani ya ngozi ya kondoo
  reply  • [h=3]Cheerlicious Chick[/h] 18 July 2013 at 10:26 | #

   Mi huwa najiuliza wadada wa mjini kwa lipi hasa? hata hapa niliwahi kusema zamani, sioni u dada wa mjini wowote kwa hilo kundi! malimbukeni wanaojipatia pesa za ziada na za kucheZea kwa njia zisizo halalai kama waume za watu, n.k ndio maana wana uwezo wa kuzunguruka kila sehemu mjini kujionyesha ujinga. WA MJINI TUPO, TUMEZALIWA HAPA KATI, TUMESOMEA HAPA KATI, TUPO HAPA KATI, NA SHUGHULI ZETU HALALI, VIPATO HALALI, MAISHA HALALI. NO ULIMBUKENI!!!
   Nawadharaugi wote. By the way, i have always loved Mange tangu anasemwa enzi za Utamu kwavile mwenye akili, thru all that has gone about around her all these years, unaona kabisa jinsi SHE STANDS OUT FROM THE CROWD! SHE'S DEFINITELY NOT ONE OF THEM!!!
   reply  • [h=3]Cheerlicious Chick[/h] 18 July 2013 at 10:26 | #

   Mi huwa najiuliza wadada wa mjini kwa lipi hasa? hata hapa niliwahi kusema zamani, sioni u dada wa mjini wowote kwa hilo kundi! malimbukeni wanaojipatia pesa za ziada na za kucheZea kwa njia zisizo halalai kama waume za watu, n.k ndio maana wana uwezo wa kuzunguruka kila sehemu mjini kujionyesha ujinga. WA MJINI TUPO, TUMEZALIWA HAPA KATI, TUMESOMEA HAPA KATI, TUPO HAPA KATI, NA SHUGHULI ZETU HALALI, VIPATO HALALI, MAISHA HALALI. NO ULIMBUKENI!!!
   Nawadharaugi wote. By the way, i have always loved Mange tangu anasemwa enzi za Utamu kwavile mwenye akili, thru all that has gone about around her all these years, unaona kabisa jinsi SHE STANDS OUT FROM THE CROWD! SHE'S DEFINITELY NOT ONE OF THEM!!!
   reply


 • [h=3]Anonymous[/h] 18 July 2013 at 07:49 | #

  daaaaaaaaaaaaaaaaaaaa thas wasup...dunia uwanja wa vita they say dont judge a book by its cover nilivoona harusi i went like wtf hawa wanaume wanawapata wapi?ohhhh god tusitamani tusivojua
  reply • [h=3]LOL[/h] 18 July 2013 at 07:51 | #

  Kweli nimeamini mange sio snitch, ni watu wachache wanaoweza kua na huo ujasiri,mtu akikuuzi mpe lake akalale nacho mfyuuuuuuuuuu

  reply • [h=3]PIPII[/h] 18 July 2013 at 07:57 | #

  Uwiii Hii mzalendo ama....riwaya ya alfa lela ulela ....too long hadi inatia uvivu kusoma. how many days did u take to write these book chapters
  ......????MAJANGA

  reply • [h=3]YOUSOU[/h] 18 July 2013 at 08:05 | #

  Mange me huwa naogopa sana unapoandika gazeti kama hivi...naamini umejipanga na best lawyers in town....na pia hizi details kama huyo dada wanna be kumchukulia mwenzake umepata toka chanzo cha kuaminika na una proof zote....Na hiyo issue ya huyo mume wa wanna be kuwa anadeal na bwimbwi pia una ushahidi.Dont get me wrong its just for your own safety.Naomba ukienda Tanzania ujipange aisee manake watu watakuwa wamekupani sana manake umeuwa image za watu kabisa.Jamani msichokoze wapasua kokoto ikiwa mnaishi kwenye nyumba ya vioo sasa haya ndio matokeo yake.Swali kwako Mange uko tayari kwa wao kutafuta siri zako pia?!manake hapo ni kama unadeal na wadada wa mujini ambao nadhani wengi wao used to be in your life sasa wakianza kuzimwaga zako uko tayari?!.Hakikisha una receipt ya kila bidhaa mlizoshop pamoja dubai na kila kitu...im just saying.Okay wana Uturn let the church say Amen....Amen.
  reply  • [h=3]Anonymous[/h] 18 July 2013 at 08:16 | #

   Najua wanapesa za ma lawyer ila chief tutahangaishana makahami milele sidhani Kama neno sembe Lina maana yoyote mbaya kisheria.... Labda Kama wao watajistukia
   reply   • [h=3]Anonymous[/h] 18 July 2013 at 09:29 | #

    kuhusu siri zangu kutoka, Chief mimi nimeanza kutolewa siri zangu toka 2008 wakati wa utamu mpaka leo hii umeona nini cha maana juu yangu zaidi ya mashauzi, ujinga ujinga na kunitukania marehemu baba yangu kwa story sizizo na kichwa wala miguu ili waniumize sababu wanajua i was daddy's girl? Siri zangu kutoka hainipi presha maana najua siri watakazo kuja nazo ni zile zile za miaka miaka rudi...Alafu hazina hata utamu wa kuuza gazeti...lol
    reply    • [h=3]Cheerlicious Chick[/h] 18 July 2013 at 10:32 | #

     Watatoa wapi jipya?!!! tena jamani Mange, anawafichia mengi sana sana sana. kuna mengi chini ya kapeti na hatumsikii Mange akiyasema...
     reply


  • [h=3]CHAUDERE[/h] 18 July 2013 at 09:00 | #

   1) Mange hana siri, nini usichokijua kuhusu huyu dada???
   2) Kazidi huyo shamimu muke ya muuza mwache apewe ukweli anapenda kuchochea kuni moto ukiwaka anasogea pembeni....
   3) Hiyo ndoa haidumu na haina amani, ukiiba mwanaume wa mtu huna jipya as he dont love you rather wajipendekezaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
   reply


 • [h=3]Anonymous[/h] 18 July 2013 at 08:12 | #

  she looks so innocent usilojua ni usiku wa giza.....mboni pole wanakutaga mwizi wa waume za watu kumbe wewe victim
  reply • [h=3]Louis VNITTON[/h] 18 July 2013 at 08:14 | #

  Mimi nilikwambia siku nyingi sana kuhusu huyu dada wa "heshima", maana mwanzoni ile Bedui ameanza kudai tu kuwa "unamgeza" basi yeye alikuwa wa kwanza kumpromoti kwenye blogu yake kwa kuweka "duka" lake na mapicha mengine. Kiupande mwingine nilimuelewa kuwa anampa sapoti dada wa shogake - ex miss aliyekuwa anasoma IFM. Na hata huyo Linus naye nilijua anakuparamia kwa sababu ya kumpa sapoti dada wa shostito. Kwa hiyo kama ulikuwa hujui hawa walikuwa mashoga wakiunganishwa na huyo shoga mmoja.

  Dada wa "heshima" ni kwa wale wasiomjua katokea wapi, na alikuwa anafanya kazi gani kwanza. Zeze alikuwa moderator wa Dar hotwire, yaani kule kulikuwa na matusi ya kufa mtu, halafu eti leo anasema watu wanakuiga matusi yako? Amesahau matusi ya Darhotwire? Au nyie kina Mange mlikuwa bado under 18 mlikuwa hamuingii kule kwenye forum za Darhotwire? Inawezekana, maana ile ilikuwa hot hot hot kuliko pilipili enzi zile hata JF haijafikiriwa kuzaliwa, ndio enzi za Darhotwire! lol!

  Kitu kingine Mange, kuufunga hakukatazi mtu kusema ukweli, hakukatazi mtu kujitetea, na wala hakukatazi mtu kupigania haki yako. Ukiwa umefunga na una kitu kimekukera eti ukakaa kimya unasemea pembeni huo ndio unafiki na hauruhusiwi. Hapo ulipo hujamsenegenyenya wala kumteta mtu, kitu ambacho wengi wanaofunga wanakifanya, wewe umeweka kila kitu wazi, wote wataona na kujisoma humu. Nafikiri watu wengi wangekuwa kama wewe, hizi tabia za unafiki, uwongo, umbea na majungu zingepungua kama sio kwisha kabisa.

  Jamani wanawake tupendane, acheni makundi yasiyo na kichwa wala miguu, acheni tabia za kujiona nyie ndio bora kuliko wengine, tusaidiane panapobidi tunyanyuane sio kunyanyapaana. Maana chanzo cha yote hayo ni kutaka kujiona nyie ni bora kuliko wanawake wengine. Nilishasema humu kitambo kama wengine mlikuwa hamjapata ujumbe wangu leo narudia tena, ANAEWEZA KUJIDAI KUWA YEYE NI WA MUJINI NI LILE SANAMU LA BISMIN TU PEKE YAKE, maana yeye pekee ndie yuko tangu Darisalama inaitwa Mzizima, wakati bibi yangu analima shamba lake viwanja wa Ikulu mpaka leo hii Darisalama limekuwa jiji lenye kila uchafu, vitimbi na vituko.

  Ni mimi Dada wa Kijijini niliyezaliwa katikati ya Darisalama.
  reply • [h=3]Anonimausi[/h] 18 July 2013 at 08:46 | #

  Yani Mange K hunijui sikujui ila ningekutumia moet ufuturie na mie huku nifungue tusogoe tuuuu kwa simu!! Am in love with ur heart!! Lakini am sure u got that kind of a heart with xtra baada ya kuzaa!!!
  Amen to u sister!!!!!!! Just keep on the motto YOLO!! Blessed!
  reply • [h=3]MUKE YA MCHAGGA[/h] 18 July 2013 at 08:49 | #

  Maskini Mange wa watu I am always on your side hata wakikunanga vp sijui kwanini. Pole sana dia unazidi kutufungua akili na wengi wetu mapenzi yetu kwako yanazidi kuongezeka.
  reply • [h=3]mbwiga[/h] 18 July 2013 at 08:50 | #

  mange achana na mbweha huyo hafikii levo yako uko juu. huyo kima anatafuta umaarufu kwa nguvu.
  reply • [h=3]mupher[/h] 18 July 2013 at 08:51 | #

  wallah napenda kuingia in your blog kusoma kuangalia picture ilove you dada mange coz unajitambua wewe ni nani na unahitaji nini lakini kwa issue ya leo dada yangu kwa kila aliekukusudia ubaya mungu atamlipa ubaya huo, na hakuna jambo baya kama kumtukana mtoto ambae hana hatia hajawahi kukuvunjia heshima hilo limenkera kuingizwa watoto na kuwatia watoto manuksi angali hawajui yanayoendelea katika dunia hii..mungu atakustiri na atakuwekea kivuli katika kila baya ambalo mtu analitia nia
  reply • [h=3]ANONYMOUS[/h] 18 July 2013 at 08:55 | #

  i see no problem na kukopa. yani mkopo wa sinta gunzo je the celebrities wanaochukua mortgages sio mikopo ile? hebu acheni ushamba.
  reply • [h=3]mbwiga[/h] 18 July 2013 at 09:01 | #

  WAKUACHE, WAKUKOME, WAKUTUE NA WANAO. MANGE UKO JUU MIAKA MIA 8
  reply • [h=3]Anonymous[/h] 18 July 2013 at 09:10 | #

  HARIKAAA.. NAPITA TU HAPPY BIRTHDAY MANDELA
  reply • [h=3]baby ya Mange[/h] 18 July 2013 at 09:10 | #

  Alaah kumbe!....sasa nimepata majibu ya maswali yangu...serious nimeumia sana tena sana baada ya kuyajua haya pole sana Mangenitha wangu sasa nimeelewa hata na sababu hasa ya wewe kufanya uliyonifanyia kama baby yako...manake nakumbuka the day huyu dada amecoment kwenye picha yangu is the day ulifanya yako...baby mahusat wangu sikuwahi kuyajua haya yote jamani!naandika kwa uchungu sana asubuhi ya leo sababu now I know n I'm sure she is the reason behind....sababu hata ingekuwa mimi nisingependezwa... kwa hisani yako mahusat wangu nakuomba unisamehe sikuwa nayajua yote haya....I pronounce her to be deleted and blocked from my list...damn!she is so bad ..will always always be on ur side my wifey...ayaaaaa! Yani usingizi wangu wote mtamu wa asubuhi umekata kwa jinsi navompenda Mangenitha wangu....
  reply • [h=3]Anonymous[/h] 18 July 2013 at 09:10 | #

  mwe!Mange naogopa kweli nahisi kama vitu vingine vinaweza kukuletea matatizo makubwa sana,maana hawa wauza sembe wengi wao ni watu wakubwa wa serikalini, yasije yakakukuta kama ya amina chifupa plis,bado tunataka kukuona hapa ukiblogua na kutuonyesha atleast picha za marekani sie ambao hatubahatika kufika.please achana na haya mambo wewe tupe mashauzi yako sie ndo tunayapenda.please stop this.

  reply • [h=3]Sir Amanthe[/h] 18 July 2013 at 09:12 | #

  MMhh Chief leo umeandika "daily news " haswaaaaaaaa,aaah mbona swaumu za watu leo zitakwazika??mana umechmbua kama karangaaaaaaaaaa,haya sisi wenye macho na masikio tumeelewa the whole concept of being "mudada wa mujini"!!!!weraaaaaa,aaah Mboni Masimba pole dada kwa kuchukuliwa kitumbua,kumbe wanakusemaga bureeeeee duh kweli "aliye msafi na aanze kurusha jiwe"!!!Mange Kimambi umeuaaaaaaaa aah ngoj ie nde blog za kucopy n paste najua leo hii ndo habar ya mujiniiiiiiiiiiiiiii na topic of the day!!
  reply • [h=3]neylicious[/h] 18 July 2013 at 09:12 | #

  Mange nazid kukupenda loh chezea shamim mtoto wa mji mpya moro town wewe uswaz uswaz tu asili ipo palepale hata angehamia osterbay
  Haya sasa mnaomsifiaga mama fashion8020 mpo wap tuwaone nyooo mwanamke mchonganishi na mwiz wa bwana wa mwenzke mujin inahusu loh Nazid kumchukia
  reply • [h=3]mbwiga[/h] 18 July 2013 at 09:13 | #

  SHAMIM KUMBE HUYO SI MUMEO. LOOO AIBUJE


 

Prisoner 46664

JF-Expert Member
Dec 18, 2010
1,948
2,000
I have never been able to understand these women or what they do,or those women who spend part of their quality day time to give a cheer to these fights without justified cause....i need a lesson,in this,i can not even a single bit understand women when what they do is this...anyways...ngoja nipite.
 

NancyM

JF-Expert Member
Mar 2, 2013
314
0
Lol very interesting jamani I took two days to read this umbeya chuki binafsi hazifai jamani aliyepewa kapewa tuu

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 

Aza

JF-Expert Member
Feb 23, 2010
1,700
1,250
Muke Ya Muzungu mambo,mie natafuta blogu ya yule mdada wa australia kama sikosei rosemary mama wawili sijui, ebu nifanzie mupango niipate blogu yaitweje :israel::israel:
 
Last edited by a moderator:

gwa myetu

JF-Expert Member
Aug 18, 2014
4,397
2,000
Mange leo kamlipua mume wa Shamim huko insta , kumbe mange yupo sawa jamaa huyo Kadinda anauza unga naameitwa na makonda .

Nasikia jamaa alitaka mtwanga mange na bastola
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom