ashy da don
JF-Expert Member
- Jan 12, 2013
- 615
- 671
Mkuu unachoambiwa ni ukweli, fata utaratbu, wengi wenu mnakuja kuumia baadae mnakuja kulia lia tu baadae, utaratbu wa kujenga inabd upate ramani kwanza, na hyo ramani inabd iendane na matakwa yako yani iwe dream house yako, kumbuka nyumba ni uwekezaji hata kama utajenga kwa miaka 5 bado nyumba yako itakua na thamani kubwa, sasa si vzuri nyumba ya mill 40 umejenga alafu umekaa mwaka tu unaanza kuichukiaMkuu na jenga nyumba yangu sio ya serikali wala CCM wala katibu tarafa wala mahakama. Acheni kunipangia as if mnaleta material site.
. Mtafute Mchora ramani aende site, achukue vipimo kwenye site yako, umueleze kuwa unataka nyumba ya aina gani iweje hyo nyumba, pia iendane na budget yako.
Kumbuka kwenye kudesign nyumba kuna vtu vingi wanavyoangalia wataalamu mfano uelekeo wa upepo, mzunguko wa hewa ndani, usalama kwenye nyumba yako nk.
Mwambie uwezo wako na upatane naye kuhusu gharama ya michoro, akuchoree michoro ikiwa kamili akugongee muhuri, then uende manispaa ukapate kibali cha ujenzi. Usipjenga na kibali manispaa wakikuotea ukipigwa stop order na wew unakuta umefika kwenye kupaua nyumba watakupiga fine kubwa tu.. Hadi mili 5 mana hujafata sheria.
Mwisho acha kulalamika gharama za uchoraji huwa znaendana na gharama za nyumba wew unataka uchorew nyumba ya million 70 alafu unataka umlipe mchoraji elfu 50 hii sio fair.
Kumbuka kazi ya mchoraji ni kuandaa michoro pia kusimamai hatua zote za ujengaji ili jengo lililochorwa liendane na ramani. Hvo ukiambiwa gharama ya ramani ni 350k huwa znainclude vitu vingi sio tu yale makaratasi.