Wachora ramani za nyumba mna shida gani?

Wachora ramani za nyumba mna shida gani?

guzman_

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2016
Posts
1,277
Reaction score
2,443
Moja kwa Moja bila hata salamu.

Niko kwenye mchakato wa kuanza kujenga ka kibanda hapa downtown kwa Bashite.

Sasa kama mjuavyo lazima uwe na ramani ya unachotaka kujenga. Nikaamua niende instagram kucheki baadhi ya wadau wanaochora ramani.

Nikafanya utafiti wa gharama. Cha ajabu kwenye page hawaweki gharama za kuchora wala gharama roughly za kujenga nyumba.

Nikamtext mmoja kumuuliza gharama ya baadhi ya ramani ambazo amepost (ni zile za kawaida vyumba vitatu) ananiambia 600,000 pomoja na makadirio ya gharama 800,000. Ikumbukwe hii anayo na ameshaichora ni suala la kuiuza.

Nikaamua kusepa. Nikaenda kwa mwingine kasema 700,000/= nikamfuata mwingine kaniambia 550,000.

Swali: Hivi njie jamaa mnafikiri sisi tunaokota hela au hamuwezi hata soma status ya wateja wenu (purchasing Power).

Natambua kazi mnayoifanya ila jaribuni kuregeza bei. Mimi mshahara 250,000 take home. So mnataka nikusanye miezi mitatu bila kula nije kununua ramani kweli.

Nilitegemegea ukiwa na ramani mtu akiitaka unamsukumia hata kwa 50,000 maisha yanaendelea.

Anyway sina maneno mengi sana. Sasa nafikiri napita mtaani nikiona mtu ananyumba nzuri nitaenda kumuomba ramani nyie zenu kaeni nazo.

MREJESHO: Kuna mdau kanipa ramani full 2 (Nichague kama zitanifaa) ambazo yeye alijenga na amekubali kunipigia mihuri kwa 50 then nikafuatilie vibali Halmashauri. Actually ni ramani ziko very clear kuliko hata zile za malofa wa 700k.
 
Bure Hapana mkuu. Nataka mtu mwenye reasonable price. Hii ya kutajiana bei kama nataka kujenga mansion ni ufara kabisa
Niambie aina ya nyumba unayotaka kujenga. Unataka ghorofa au nyumba ya chini? Kiwanja chako kina ukubwa gani?
 
Mtaani Utapata Nyingi Sana
Wakati Mwingine Fundi Utakayempata Anaweza Kukupatia Ushauri Mzuri Kuhusu Nyumba Uitajayo

Kupewa Utapewa Maana Ramani Nyingi Sana
Nimefikiria hivo pia. Mana hawa jamaa hawana utashi wa kujiongeza. Mimi wakati naanza kufanya hizi shughuli zangu nilikuwa napewa hata ishu ya 100,000. Nikiwa home nimepumzika naifanya napata hela ya vocha.
 
Waulize hizo gharama zinahusisha na mihuri toka kwa Architectural firms ambazo ziko registered na AQRB..? Kama jibu ni ndio basi price uliopewa ndo ya mtaani hiyo.. Ukumbuke kujenga siku hizi unatakiwa uwe na kibali toka Manispaa.. Na ili upate kibali toka Manispaa unatakiwa uwe na michoro iliyopitishwa na Manispaa.. Na ili Manispaa wapitishe michoro, wanahitaji michoro yenye mihuri ya firms ambazo mchoro umechorwa huko..
 
Duuh hiyo ni ramani ya architecture bado kuna structural drawings, resonable price njoo nikupatie zote mbili kwa laki 6, architect nampa 3 na engineer analamba 3,

Kwanini bei inakuwa juu?wengi wanaochora mtaani hawana ofisi wala mihuri, hivyo lazima wakienda kugonga mihuri kwenye ramani waache 100,000 - 200,000, na kwa architects na wahandisi wanaojitambua lazima wakague kwanza kazi kabla hawajagonga
 
Mimi ni msanii mkuu. Mimi nataka ramani hizo habari za Manispaa sizielewi na sifanyagi kabisa.
 
Waulize hizo gharama zinahusisha na mihuri toka kwa Architectural firms ambazo ziko registered na AQRB..? Kama jibu ni ndio basi price uliopewa ndo ya mtaani hiyo.. Ukumbuke kujenga siku hizi unatakiwa uwe na kibali toka Manispaa.. Na ili upate kibali toka Manispaa unatakiwa uwe na michoro iliyopitishwa na Manispaa.. Na ili Manispaa wapitishe michoro, wanahitaji michoro yenye mihuri ya firms ambazo mchoro umechorwa huko..
Hizo blah blah zoote hazijustify gharama ya Tshs 350k
 
Duuh hiyo ni ramani ya architecture bado kuna structural drawings, resonable price njoo nikupatie zote mbili kwa laki 6, architect nampa 3 na engineer analamba 3,

Kwanini bei inakuwa juu?wengi wanaochora mtaani hawana ofisi wala mihuri, hivyo lazima wakienda kugonga mihuri kwenye ramani waache 100,000 - 200,000, na kwa architects na wahandisi wanaojitambua lazima wakague kwanza kazi kabla hawajagonga
600,000 ramani? Aisee sio mimi mkuu. Never sifanyi huo ulofa
 
Back
Top Bottom