Wachora ramani za nyumba mna shida gani?

Wachora ramani za nyumba mna shida gani?

Tutumieni wataalam kwenye ujenzi, ukitoka Kwa architect, unaenda Kwa Land surveyor, halafu unaenda civil engineer, halafu unamalizia Kwa mkadiaji majenzi
watu wanapenda bei rahisi hlf wanajengewa nyumba zina nyufa kibao.
 
Na mimi naomba msaada...nina kiwanja changu kipo Mbezi mwisho kina ukubwa wa 20 urefu na upana 26 je naweza kujenga nyumba ya ukubwa gani na gharama yake je kwa nyumba ya kawaida tu sio ya kifahari...maisha yenyewe ya kawaida so nyumba ambayo inasadifu hali halisi ya maisha

Hata kama maisha ya kawaida ila hicho unachokiomba na kuulizia hapa watu wamekaa darasni miaka 4 - 5 siyo rahisi kukipata bure,

Kuna architect yeye atakuchorea nyumba ya ndoto yako

Kuna engineer yeye ata design structure na ku detail

Kuna quantity surveyor huyu atakadiria gharama za nyumba yako kwa kutumia details na michoro ya architect na engineer...na ukitak kujenga sasa hivi hawa watu si rahisi kuwaepuka, watafute watakusaidia kulingana na hali ya maisha mkuu
 
Una maanisha nini ukisema structure ya jengo anafanya engineer wewe ukichora ramani huwa hujui structure yake?

Mkuu usione tuu majengo yanasimama kuna mahesabu makali, nyuma yake
 
Moja kwa Moja bila hata salamu.

Niko kwenye mchakato wa kuanza kujenga ka kibanda hapa downtown kwa Bashite.

Sasa kama mjuavyo lazima uwe na ramani ya unachotaka kujenga. Nikaamua niende instagram kucheki baadhi ya wadau wanaochora ramani.

Nikafanya utafiti wa gharama. Cha ajabu kwenye page hawaweki gharama za kuchora wala gharama roughly za kujenga nyumba.

Nikamtext mmoja kumuuliza gharama ya baadhi ya ramani ambazo amepost (ni zile za kawaida vyumba vitatu) ananiambia 600,000 pomoja na makadirio ya gharama 800,000. Ikumbukwe hii anayo na ameshaichora ni suala la kuiuza.

Nikaamua kusepa. Nikaenda kwa mwingine kasema 700,000/= nikamfuata mwingine kaniambia 550,000.

Swali: Hivi njie jamaa mnafikiri sisi tunaokota hela au hamuwezi hata soma status ya wateja wenu (purchasing Power).

Natambua kazi mnayoifanya ila jaribuni kuregeza bei. Mimi mshahara 250,000 take home. So mnataka nikusanye miezi mitatu bila kula nije kununua ramani kweli.

Nilitegemegea ukiwa na ramani mtu akiitaka unamsukumia hata kwa 50,000 maisha yanaendelea.

Anyway sina maneno mengi sana. Sasa nafikiri napita mtaani nikiona mtu ananyumba nzuri nitaenda kumuomba ramani nyie zenu kaeni nazo.

MREJESHO: Kuna mdau kanipa ramani full 2 (Nichague kama zitanifaa) ambazo yeye alijenga na amekubali kunipigia mihuri kwa 50 then nikafuatilie vibali Halmashauri. Actually ni ramani ziko very clear kuliko hata zile za malofa wa 700k.
Wanataja gharama bila kwenda site? Hizo ni ramani za mwendokasi
 
Ngoja nikuulize swali dogo Sana
Unajua ni kwanini leo nikiamua kwenda kusomea masters ya civil engineer ninaqualify Moja kwa moja na bachelor yangu ya architecture ,lakini wewe mwenye bachelor ya civil engineer huruhusiwi hata kidogo kwenda kuchukua masters ya architecture duniani kote hata ungekua na GPA ya Tano.
Pili kwanini architect ndio kiongozi kwenye ujenzi na sio Engineer Wala Qs

Ukijibu hayo tunaweza kwenda sawa
Aaah mjadala ulikuwa mtamu. Naona umehamisha magoli...
 
Yaah ni kweli architecture wanasoma structure ndio maana structural engineer anaweza kuwa aliyesoma architecture au civil engineering japokuwa sio kweli architect ni boss wa civil engineer hii nakataaa mi site zote nilizowahi kufanya kazi hakuna architect yoyote ambae amewahi kuwa boss wangu coz project ni ya client na client ndio boss
Client
Architect
Clerk of works
Consultant
Qs
Main contractors
Sub contractors and Specialists
 
Yaani kweli ramani ya nyumba laki?huo no uboya nyumba nachora mwenyewe
 
Yaani kweli ramani ya nyumba laki?huo no uboya nyumba nachora mwenyewe
laki??? labda nikuchoree choo .6% ya gharama za mradi ndio ujira wangu kama consultant. ok chora mwenyewe the ukimaliza uchukue michoro yako upeleke manispaa wakakupe permit na michoro yote uchore ikamilike kama vile floor plans,foundation plan,elevation zote ,sectons,roof plan,site layout,details za staircase,parapetwalls,roof trusses,landscapping,waste water(septic and soak pits? system mpaka 3d's.
 
Nimesoma comments zote 210[emoji16]! Nahitaji ramani pia, vyumba 3, ; Master room 1, bedroom 2 , jiko, stoo, public toilet, dining na sebul.. ila sebul natak iwe kwenye kona (dirisha kubwaaa 2) ..halafu ili ufike seblen inatakiwa upite korido kadhaa hiv, sio ile unafungua mlango unakutana na sofa! (Hii ni kwaajil ya usalama [emoji3])

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesoma comments zote 210[emoji16]! Nahitaji ramani pia, vyumba 3, ; Master room 1, bedroom 2 , jiko, stoo, public toilet, dining na sebul.. ila sebul natak iwe kwenye kona (dirisha kubwaaa 2) ..halafu ili ufike seblen inatakiwa upite korido kadhaa hiv, sio ile unafungua mlango unakutana na sofa! (Hii ni kwaajil ya usalama [emoji3])

Sent using Jamii Forums mobile app
Nakutumia moja uone kama itakufaa mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni kwamba mna ushamba mwingi au ni utoto mwingi?hamjui umuhimu wa ramani ya nyumba kweli?
Nyumba ambayo utaishi wewe mwenyewe inakuaje mtu mwingine akuchoree ramani? Anajuaje mahitaji yako?
Watu wa mijini mna tabu sana. Sasa ramani ya nini? Kwetu village unachora kwa kidole gumba cha mguu huku ukimwelekeza Fundi 'nyumba itapita humuuuuuu'. Yàani bure kabisa bila hata kutoa senti na nyuma inadumu, unakufa wanairithi hata vitukuu!!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Client ni owner hajui lolote kuhusu ujenzi.tukija kwenye building industry ,ujenzi wowote ule Architect ndio bosi wa proffesionals wote kwenye ujenzi.
Mimi nakubali wewe ni architect mana nimesoma na ma archtect huo ubishi wa kupenda kuwa maboss kwenye industry mnaupenda sana[emoji3][emoji3], Kusema kua eti architect ni boss wa civil sio kweli Mimi naona inategemea mana hiyo ni kama client ataamua kutafuta consultant kwaajili ya kazi yake Basi huyo atamsimamia contractor ambaye ni mjenzi. Na consultancy hawezi kua mtu moja et uamue tu kua nilivyofanya ndio hivi baass Hapana inakua ni team yenye architect,civil,Q's na akina watu wa umeme ili kila mtu acheki upande wake hivyo wewe kama wewe et ukachora mawazo yako yasiyohitaji ushauri labda liwe jengo lako[emoji28].

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mleta mada achana na wenye mawazo ya kifisadi kama huyu, kwangu utapata kwa 100000 tu na pengine mtaani hata kwa hiyo 50k ukapata. Laki 8 ramani wakati hiyo ni gharama ya chumba kabisa!! Ukitaka kujenga nyumba hakikisha unaepuka gharama zisizo za lazima na hivyo minimize gharama to the lowest. Nakupongeza kwa kushtuka mapema.
Upo wapi ndugu
 
Back
Top Bottom