kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 16,247
- 16,169
Kuna uzoefu ambao wachezaji wetu wa ndani wangeweza kukutana nao kwa timu zetu kualika timu za kigeni au kushiriki mashindano ya CAF, lakini wachezaji wetu waishukuru TFF kuruhusu na timu zetu kusajili wachezaji wenye viwango vikubwa sana kama Pacome, Mpanzu, Diara, Camara, Aziz Ki, Sowah, Sila, Kipre, Mayele, nk kucheza nao kwenye timu au ligi moja. Hii ina maana kuwa wachezaji wetu ni kama vile wamepata mechi za kigeni karibu msimu mzima. Hivyo, wachezaji wetu hawana sababu ya kushindwa kutumia uzoefu wanaoupata kutoka kwachezaji wageni hawa kubeba kombe la mashindano ya CHAN mwaka huu.
Wenzetu wanacheza wachezaji wa ndani lakini sisi ni kama vile tunachezesha timu yenye hadi wachezaji wanaocheza mataifa ya kigeni. Hatutakuwa na kisingizio cha kushindwa kuubeba ubingwa wa CHAN.
Wenzetu wanacheza wachezaji wa ndani lakini sisi ni kama vile tunachezesha timu yenye hadi wachezaji wanaocheza mataifa ya kigeni. Hatutakuwa na kisingizio cha kushindwa kuubeba ubingwa wa CHAN.