Rais Samia achana na mambo ya ‘bahati haikuwa upande wetu’ Uwekezaji kwenye Soka ni muhimu kuliko Hamasa

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Ujenzi wa Mohammed VI football Complex umegharimu $65 milioni (TZS 163.45 bilioni). Hii ni tone tu katika pesa ambazo Ummy Mwalimu na Wizara ya Afya walitajwa kuzitafuna katika taarifa ya CAG.

Ukaguzi wa CAG (TANROADS) ulibaini TZS 136.69 bilioni zilitumika kununua mtambo wa sukari ambao hata hivyo mtambo wenyewe (ambao haujulikani kazi yake) miaka mitatu sasa, haujafika Tanzania

Mohammed VI football Complex. Youssef En-Nesyri (Sevilla Fútbol Club), Azzedine Ounahi (Olympique de Marseille), Nayef Aguerd (Westham) wametoka hapo. Ounahi na En-Nesyri wameitungua Tanzania AFCON.

Mohammed VI football Complex ni nyumbani kwa timu za taifa za nchi hiyo wakati wa maandalizi ya mashindano na pia timu za kigeni zinazotaka kufanya maandalizi yao nchini Morocco. Eneo hili linachukua mita za mraba 300,000.

Mohammed VI football Complex unabeba timu ya taifa (66 rooms and 4 suites), unabeba timu za U23 na U17 sehemu yao kuna vitanda 150 na vitanda 80 mtawalia na makipa wenye vyumba 54.

Pia ina sehemu za kulia chakula na maeneo ya kupumzika, ukumbi wa viti 221 ambao unaweza kuandaa matukio mbalimbali (mikutano, maonyesho ya filamu), na majengo ya utawala.

Ndani ya Mohammed VI football Complex kuna Jumba la kisasa kabisa, mojawapo kubwa zaidi duniani limesimikwa na kujengwa na vifaa vya kisasa vya hali ya juu, kulingana na viwango vya FIFA.

Kuna viwanja vinne vya mpira wa miguu vya nyasi asilia, viwanja vitatu vya mpira wa miguu vya nyasi bandia, uwanja wa mpira uliofunikwa, uwanja wa mpira wa mseto, chumba cha mazoezi

Tena ni kiwanja ambacho kinaweza kuandaa michezo ya kimataifa ya futsal. Pia kuna bwawa la nje la kuogelea lenye ukubwa wa michezo ya Olimpiki, viwanja viwili vya tenisi na Soka la Ufukweni.

Vifaa vingine vinavyopatikana Mohammed VI football Complex ni pamoja na kituo cha dawa za michezo na utendaji za kizazi kipya ambacho kinakidhi viwango vya FIFA katika uwanja huo kikijumuisha;

physiotherapy, stress testing, dentistry, ophthalmology, trauma, psychology, podiatry, nutritional medicine, radiology, ultrasound, electrotherapy, bone densitometry, cryotherapy, an emergency mobile medical unit.

Hii ni sehemu ya programu ya kitaifa ya uboreshaji wa miundombinu ya soka katika taifa la Morocco. Programu hii imewalipa. Miaka minne baadae wamefika nusu fainali kombe la Dunia, Qatar.

Chini ya mpango huo, pia ni kwa ajili ya kuendeleza mazoezi ya soka, viwanja 138 vya mpira wa miguu vilivyotengenezwa kwa nyasi bandia vimekarabatiwa na viwanja 13 vya nyasi asilia vimeanzishwa.

Morocco waliamua kuwekeza katika miundombinu ya michezo. Real Madrid CF na Fußball-Club Bayern München wametembelea Mohammed VI football Complex na kuweka kambi ya timu zao.

Morocco wamewekeza katika soka la vijana na miundombinu. Limewalipa. Leo Morocco wapo nafasi ya 13 katika viwango vya FIFA juu ya German (14) na Denmark (19) kwa viwango vya 21 Dec 2023

Morocco ndiyo mabingwa wa Futsal Duniani kwa sasa. Morocco ndiyo mabingwa wa AFCON U23. World Cup U17 Morocco wamefika 16 bora. World Cup Morocco wamefika nusu fainali. UWEKEZAJI unalipa siyo HAMASA.

2021/2022; Wydad Athletic Club Casablanca ni mabingwa wa klabu bingwa Afrika. Renaissance Sportive de Berkane ni mabingwa shirikisho Afrika. Association sportive des Forces armées royales (ASFAR) ni mabingwa wa klabu bingwa Afrika - wanawake.

Timu zote za Morocco. Hazikufika hapo kwa bahati mbaya. Uwekezaji wao ni mabilioni ya fedha. Wamejenga viwanja vyao michezo na shule za michezo kwa ajili ya kuibua vipaji kutoka kwa vijana wadogo ndani na nje ya Morocco. Timu ya Taifa inapata faida.

Walid Regragui ndiye kocha wa Morocco. Mzaliwa wa France raia wa Morocco. Amefundisha Wydad Athletic Club michezo 48, akadumu siku 353. Alipoondoka Wydad Athletic Club akateuliwa kuwa Mwalimu timu ya taifa ya Morocco.

Amewafikisha Morocco nusu fainali World Cup. CCM mtu wa aina hii yupo? Tunaanda watu wetu kuwa walimu wa timu kubwa ndani na nje ya nchi? Nani kwa mfano? Simba na Yanga zinachukua walimu wao kutoka nchi za America na Ulaya. Ndani hapa hawapo.

Wachezaji wengi wa timu ya taifa ya Morocco wamezaliwa nje ya Morocco, na hadi sasa wengi wanao uraia pacha. Timu ya Taifa ya Morocco ambayo imefika nusu fainali World Cup kule Qatar 2022 98% ya wachezaji wake wamezaliwa nje ya Morocco na wanacheza ULAYA.

Romain Saïss (🇫🇷), Yassine Bounou (🍁), Achraf Hakimi (🇪🇸), Noussair Mazraoui (🇳🇱), Sofyan Amrabat (🇳🇱), Hakim Ziyech (🇳🇱), Ilias Chair (🇧🇪), Selim Amallah (🇧🇪), Walid Cheddira (🇮🇹), Sofiane Boufal (🇫🇷), Zakaria Aboukhlal (🇳🇱), M'barek Boussoufa (🇳🇱), Mehdi Carcela-Gonzalez (🇧🇪)

Wachezaji wa kikosi cha Morocco kilichofika nusu fainali ya World Cup, ni mchezaji mmoja tu alitoka Wydad Athletic Club Casablanca (walikuwa mabingwa wa klabu bingwa Afrika), wachezaji wengine wote wanacheza vilabu vya Ulaya, ikiwepo Manchester United.

Sera za Tanzania haziruhusu uraia pacha, hii inafanya vipaji vingi kupotelea ughaibuni au kukosa huduma za wanaopenda kutumikia Tanzania lakini wabaki na uraia wao. Watu timamu tungeweka mjadala katika eneo hili, tupate muafaka wa pamoja.

CCM mmejiandaa vipi? Mpira wa miguu haudanganyi, mpira hauhitaji siasa za kuacha VX pembeni na kupanda punda. Mpira wa miguu unahitaji uwekezaji, mikakati ya muda mrefu na utekelezaji. Huwezi kutumia intelejensia ya polisi kufuzu kombe la Dunia 2030 au kushinda AFCON.

Serikali ya CCM, wekezeni katika ujenzi wa miundombinu ya michezo. Msiwekeze katika kununua magari ya kifahari na ufisadi wa kutisha. Acheni UFISADI. Acheni maandalizi ya zimamoto.

Achana na habari za ‘bahati haikuwa upande wetu’, hakikisha serikali inawekeza kwa nguvu katika mpira wa miguu, jengeni viwanja vya kisasa vya michezo, jengeni academies, watafutie soko la nje wachezaji.

Baada ya miaka 10 tukae chini kujadiliana tukiwa tumeacha mambo ya “mama anaupiga mwingi” na tumeachan na porojo za hamasa. Mpira wa miguu una njia zake za mafanikio, kwanza uwekezaji. Nakutaki utekelezaji mwema.

Martin Maranja Masese, MMM.
 
Back
Top Bottom