Wachawi wamemchukua mwanangu

Wachawi wamemchukua mwanangu

Ndg yangu Zogwale sijui imani yako niipi ila kama una huyo ndg yako anataabishwa na wachawi or Mizimu sikushauri ushindane na mchawi Kichawi hutaweza.....Tambua kwamba wachawi hadi wanakufanyia majanga....huwa wanatoa makafara makubwa nailia ujinasue lazima ujue kafara aliyotumia ili ulipe hiyo Gharama then ndio ujue namna yakujinasua sio..Ishu ndogo km inavyofikiriwa kuna watu wamewekeza kwa shetani above 100% acha kabisa nakupa mfano wangu Mimi kuna MTU aliniharibia maisha Kafara aliyotumia alichukua.. sehemu za SIRI za wanawake wawili....ndio aliniapizi nazo sasa niambie utawezaje kulipa fidia ya Kafara kama hiyo ukienda kwa mganga japokuwa atajua kinachokutesa lkn hatakwambia namna yakujinasua ataishia kula Pesa yako tu....Ingawa sijui imani yako lkn....muamini MUNGU wakweli waganga ni Mawakala wa Shetani watakutesa sana
Mkuu dolevaby pole sana. Aise kisa chako kimenishtua. Ila hakika mchawi si mtu kabisa wa kukenulia meno. Ukimuweza ni kummaliza tu kiishe. Ninaamini umeshapona tatizo lako. Ila mimi nina fundo ni lazima nilipize kisasi, ila ninatafiti ili nimpate fundi haswa ambaye akitenga tu anamaliza. Niko tayari kusafiri hata kama ni mbali kiasi gani ili mradi tu nihakikishe atafanikisha tu. Siwezi kusema mengi ila kuna mateso sana wanafanyiwa hasa watoto ambao hawana hatia kabisa.
 
Last edited by a moderator:
Pole sana,muachie Mungu ndiye muweza wa yote!
 
Haya mambo ya kichawi namwachia mchawi LIKUD na MziziMkavu, mimi sijui uchawi.

Mimi ushauri wangu awe mcha Mungu sana, yeye na mkewe na wachawi hawatakuwa na nafasi kwao wala kwa watoto zao.

Sisi Waislam tunafundishwa kinga za uchawi, kwanza ni kuwa na udhu wakati wote, kusali kwa wakati, kusoma Qur'an sana, du'a mbali mbali za kujikinga na mambo hayo na shari zote za kidunia.

Ukiwa mcha Mungu mchawi hana chake kwako.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu dolevaby pole sana. Aise kisa chako kimenishtua. Ila hakika mchawi si mtu kabisa wa kukenulia meno. Ukimuweza ni kummaliza tu kiishe. Ninaamini umeshapona tatizo lako. Ila mimi nina fundo ni lazima nilipize kisasi, ila ninatafiti ili nimpate fundi haswa ambaye akitenga tu anamaliza. Niko tayari kusafiri hata kama ni mbali kiasi gani ili mradi tu nihakikishe atafanikisha tu. Siwezi kusema mengi ila kuna mateso sana wanafanyiwa hasa watoto ambao hawana hatia kabisa.

A see...namshukuru MUNGU angalau nimerudi kwenye mstari ila nilitaabika sana....Khs kulipiza kisasi kumng'oa ikibiti utumie manati ya mzungu au namna yyt lkn kwa uchawi utahangaika sana....Tatizo la wachawi wanaua watu lkn niwaoga sana wao kufa....so...wanatumia maKAFARA makubwa pia kijizibdika so hadi umpate kwa kwa uchawi utakuwa umesaga lami sana
 
Last edited by a moderator:
Pole sana.Ila kama hutamkamata Bwana Yesu sawa sawa, Shetani ataendelea kukuchezea,na hiyo haitakuwa mwisho.Dawa ya wachawi ni Yesu tu.Kumbuka kwamba adui yako sio mchawi,ni Shetani.Pambana na Shetani aliyemtumia huyo mchawi kumuua mwanao.Vita vyetu si juu ya damu na nyama,bali ni juu ya falme,mamlaka na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa giza.
Daaa.....ina huzunisha na kusikitisha sana
Pole sana mkuu kwa kupoteza uzao wako.
Naomba ufunge kwa wiki moja ukiongea na mungu
hakika utapata majibu ya duku duku lako.
 
Last edited by a moderator:
A see...namshukuru MUNGU angalau nimerudi kwenye mstari ila nilitaabika sana....Khs kulipiza kisasi kumng'oa ikibiti utumie manati ya mzungu au namna yyt lkn kwa uchawi utahangaika sana....Tatizo la wachawi wanaua watu lkn niwaoga sana wao kufa....so...wanatumia maKAFARA makubwa pia kijizibdika so hadi umpate kwa kwa uchawi utakuwa umesaga lami sana

Ni kweli wao ni waogoa ndo maana nikasema huko juu ktk post zangu kwamba kile kinachowafanya waue ni ile roho/jini la uchawi lililo ndani yake. Jini hili humtoa mtu kabisa huruma na kuwa mkatili kama alivyoibilisi. Mchawi baada ya kuua na ile roho ya uchawi ikamtenga kwa muda huwa anaishi kama binadamu wa kawaida. Anakuwa na uoga ule ule na hofu ile ile ila akiwa ktk ulozi/uchawi kama hauna Mungu ndo utamkoma.
 
Mkuu kanambi,, wewe noma Hiyo store ya kutunzia uchawi kwa watoto wa kike imenifanya nichoke hapa nipo hoi.

Kama ushawahi kusikia wachawi huwa wanaendesha ndege zao kama ungo kupitia manii za wanaume basi tambua ni kweli kabisa, wanawake wana faida kubwa sana ktk uchawi.
Mwanamke mchawi anawekewa pando ndani ya uke wake, kazi ya hilo pando ni kushikilia shahawa za mwnaume ambae atafanya mapenzi na huyo mchawi. Pia wachawi wanaweza wakaweka hilo pando hata kwa mwanamke ambae sio mchawi ili kwamba wakati akilala na mwanaume basi zile mbegu wao wazichukue na kuzitumia.
 
Daaa.....ina huzunisha na kusikitisha sana
Pole sana mkuu kwa kupoteza uzao wako.
Naomba ufunge kwa wiki moja ukiongea na mungu
hakika utapata majibu ya duku duku lako.

Sio mungu ni Mungu
 
Last edited by a moderator:
Niite nam nitakuitikia na kukuonyesh mamb makuu na yaajab usiyo yajua. Nakushaur hakun jamb linalo mshnd mung mlilie yey nd mtoa hukum wa mwish na kumbuk malipo ni hap hap so mwchie yy anawez
 
Wanajamvi ndugu yenu nimefiwa,

Nina majonzi sana na hasira kali moyoni mwangu, mke wangu alijifungua juzi saa 2 usiku katika hospitali ya wilaya ya Maswa, mtoto alikuwa wa kike na mwenye afya njema, mzuri wa sura na mchangamfu sana.

Jana mida ya saa 4 usiku tukashangaa kumkuta mtoto kalegea na anatokwa damu masikioni na mdomoni na hakuwa akihema, ikabidi tumkimbize hospitali haraka sana, kufika hospitali tukaambiwa ameshafariki dunia, sikumuuliza Dr ni nini kimemuua mwanangu nilikuwa nimechanganyikiwa, kufika nyumbani mwanangu sura yake ilikuwa imebadilika kabisa na siyo yake.

Mchana wa leo wakati maiti inaandaliwa kuvikwa sanda tumeona mambo yasiyo ya kawaida katika mwili wa mwanangu, mwili wake katika sehemu za mbavu umetobolewa tobolewa na kubadilika rangi ikawa kahawia, kucha zake zote zimekuwa nyeusi kama aliyevilia damu, mwili wake ni wa moto kama vile yu hai.

Wakati alikufa tangu jana usiku, amebadilika na kuwa mweupe kupindukia, nimemzika mwanangu kwa majonzi sana, naapa lazima nitalipa kisasi, roho inaniuma sana ndugu zangu, sina niliyemkosea.
Pole sana kwa maelezo yako hayo unayo yasema ni kweli wachawiwatakuwa wamemchukuwa mtoto wako. Usingemzika ulipo kwenda nae hospitali ulipoambiwa na Dakatari kuw amtoto wako amefariki ulikuwa umpeleke kwenye kanisa la ufufuo wakamuombee huenda huyo mtoto uliye mbeba alikuwa sio mtoto wako wachawi wamekuwekea mtoto mwengine mtoto wako wamemchukuwa lakini pia hujachelewa mtafute Mchungaji Gwajima wa Kanisa la Ufufuo anaweza kukusaidia kumrudisha mtoto wako.

MCHUNGAJI JOSEPHAT GWAJIMA_DALILI ZA MTU ALIYECHUKULIWA MSUKULE PART 1

Last edited by a moderator:
nasikia kuna mtu anauwezo mkubwa sana.atuma watu wake yanamvua makolokolo ya uchawi yote anakuwa mweupe
 
hv mkuu NDUKI kapita hapa? hebu tupe chochote mkuu katika hili
 
Last edited by a moderator:
Pole Sana Mr, Usihangaike Kutafuta Bunduki Au Kumjua Ninani Ili Umlipie, Siku Zote Haijawai Kutokea Ubaya Ukaushinda Wema. Mwenyezi Mungu Ndie Alie Asili Ya Uhai Atakulipia Mwanao. Ungecho Kifanya Kwa Wakati Huu Ni Kurudi Kwa Mungu Kwa Moyo Wako Wote Kwa Imani Yako Nae Atakutetea. Mungu Amekazia Sana Ya Kua Yupo Karibu Nao Walio Vunjika Moyo,na Waliopondeka Moyo Huwaokoa.
Tafuta Kuwa Na Haki Na Mungu Maana Mungu Humtetea Mwenye Haki Hata Makuchani Mwa Simba, Kila La Heri Ndugu.
 
Wanajamvi ndugu yenu nimefiwa,

Nina majonzi sana na hasira kali moyoni mwangu, mke wangu alijifungua juzi saa 2 usiku katika hospitali ya wilaya ya Maswa, mtoto alikuwa wa kike na mwenye afya njema, mzuri wa sura na mchangamfu sana.

Jana mida ya saa 4 usiku tukashangaa kumkuta mtoto kalegea na anatokwa damu masikioni na mdomoni na hakuwa akihema, ikabidi tumkimbize hospitali haraka sana, kufika hospitali tukaambiwa ameshafariki dunia, sikumuuliza Dr ni nini kimemuua mwanangu nilikuwa nimechanganyikiwa, kufika nyumbani mwanangu sura yake ilikuwa imebadilika kabisa na siyo yake.

Mchana wa leo wakati maiti inaandaliwa kuvikwa sanda tumeona mambo yasiyo ya kawaida katika mwili wa mwanangu, mwili wake katika sehemu za mbavu umetobolewa tobolewa na kubadilika rangi ikawa kahawia, kucha zake zote zimekuwa nyeusi kama aliyevilia damu, mwili wake ni wa moto kama vile yu hai.

Wakati alikufa tangu jana usiku, amebadilika na kuwa mweupe kupindukia, nimemzika mwanangu kwa majonzi sana, naapa lazima nitalipa kisasi, roho inaniuma sana ndugu zangu, sina niliyemkosea.

Hili ni pigo lenye maumivu makali mno...si kwasababu Mtoto kafa hapana bali kafa kifo cha aina gani!!!
Kwenye hali kama hii ya ghadhabu na sononi unaweza kufanya lolote bila kutafakari ili kujiponya na maumivu ya kulipa kisasi
Ushauri wangu : chukua muda wa kutosha ukipumzisha akili na kutafakari kwa kina yote yaliyotokea na kwa nini iwe kwako na si kwa mwingine, kuna mengi yatafuata ukiwa mtulivu ambayo yatakupa Ufunuo na hata ufumbuzi usiotegemea...ni jambo linalohitaji muda wa kutosha na niamini ninachokuambia wabaya wako wataumbuka
 
Toyota Sienta, taa ya check engine imewaka takriban wiki tatu sasa, pia gari ukianza kuondoka inajivuta kama ina sense obstacle mbele, yaani ukikamyaha mafuta inasita kisha inafumguka hata ukiachia, fundi amecheck na kubaini fuel filter imeziba kwa uchafu. Inakuwaje wakati ameisafisha ikawa sawa kwa wiki moja tu tatizo limejirudia, au nimelenga asiye adui?
 
Hivi humu ndani bado watu wanaamini uchawi, hii nchi ya maajabu sana
 
Toyota Sienta, taa ya check engine imewaka takriban wiki tatu sasa, pia gari ukianza kuondoka inajivuta kama ina sense obstacle mbele, yaani ukikamyaha mafuta inasita kisha inafumguka hata ukiachia, fundi amecheck na kubaini fuel filter imeziba kwa uchafu. Inakuwaje wakati ameisafisha ikawa sawa kwa wiki moja tu tatizo limejirudia, au nimelenga asiye adui?

Umeisoma mada mkuu? Hapa utakuwa umepotea njia
 
Back
Top Bottom