Wachawi wamemchukua mwanangu

Wachawi wamemchukua mwanangu

Unaweza ukaona ni rahisi sana kupambana na mchawi kupitia waganga, usipoangalia hata wewe unaweza ukaja ukawa mchawi.
Neno la Mungu ndio silaha pekee ya kupambana na mchawi. Vita ya kichawi ni mbaya saaaana. Inakuja kugharimu mpaka watoto wako na kizazi chako.

Unachosema kinaweza kuwa sahihi kwa kiwango fulani ila inategemea na mapokea na imani ya mwathirika hebu angalia biblia inavyosema juu ya uchawi
Kumbukumbu la TORATI inasema hivi: Usimawache mwanamke mchawi akaishi agizo hilo alipewa nani na nani kwa nini?
 
Agizo hili walipewa wana wa Israel kipindi kile cha sheria/torati, waliambiwa kuwa mwanamke asiichi pia kuna andiko linasema asionekane mchawi kwako/mbele yako. Swali la kwanza la kujiuliza, waliwatambuaje wachawi wakati wao walikuwa wakitembea sana kimwili na sio kiroho kama Kanisa la sasa lilivyo kupitia Roho Mtakatifu? Ukweli ni kwamba walikuwa wakiwatambua wachawi kupitia makuhani, kumbuka kipindi kile Roho hakuachiliwa kwa kila mshirika kama sasa hivi ilivyo. Roho alikuwa anapatikana kupitia makuhani na manabii. Na uchawi huwa unajulikana kwa jinsi ya rohoni (kwa wale ambao wanajua vita vya rohoni watakuwa wananielewa) sasa wale makuhani/manabii na waonaji wakishatambua watu flani ni wachawi walikuwa wanahukumiwa vifo maana ndivyo sheria ya Mussa ilivyoamuru, na sio Mussa ndo alipendekeza hivi, hapana ila ni Mungu.

Swali lingine la kujiuliza ni kwanini awe mwanamke na sio mwanamme mchawi?
Mwanamke ni chombo dhaifu kama maandiko yanavyotuelezea na hata ktk jamii inaonekana hivyo ila Mkuu labda nikwambie tu kuwa MWANAMKE AKISHAKUWA MCHAWI ANAKUWA NI MBAYA KULIKO HATA JAMBAZI. Mwanamke mchawi ni katili sana. Na Mwanamke anatumika sana kumdondosha mwanamme. Kumbuka Ajenda ya Shetani ni kunyanyasa binadamu, unaweza ukawa na ela ila ukawa ni mlevi au fisadi. Kupitia mwanamke mwanamke mchawi shetani anaweza akakuingiza ktk maagano/mikataba au akakuingizia maroho machafu sana na akakuharibia maisha yako ambayo hautakuja kuiona ile mbingu ambayo Mungu ameiandaa kwa ajili yetu wanadamu.
Niongezee kidogo tu kwa kusema kuwa, Mwanamke mchawi ni ngumu kuuacha uchawi au kuundoa ndo maana unaambiwa usimuache akaishi. Mwanamke mchawi yoyote yule huwa uchawi wake upo ktk malango ya uzazi wa mwanamke na kwa mwanaume yapo kichwani. Mwanaume ni mwepesi kuondoa uchawi wake sababu upo kichwani, wachawi wa kiume ni wepesi kuibiwa uchawi wao sababu upo kichwani ila mwanamke ni ngumu kuiba uchawi wake sababu upo ktk malango ya siri. Kwahiyo wanaume wengi hawatakiwi kukabidhiwa uchawi sababu hawadumu nao na raha ya uchawi ni kukaa nao kwa mda mrefu sana, na unapokabidhiwa huo uchawi unashauriwa uutunze na kuulinda. Kumbuka uchawi unapikwa na kuuzwa na mtu huwa anapewa uchawi kutoka kwa falme flani au falme husika na atakuwa anatumika kichawi ndani ya hiyo falme. Kwahiyo hizo falme zikimpa mtu mchawi na kisha kuibiwa wanaona wameingia hasara kubwa sana ndo maana wanawapenda zaidi wanawake sababu ni ngumu kuiba uchawi wao na kisha mwanamke ni katili sana na anaweza akamuangusha mwanamme.
******Naomba niishie hapa, nimechoka kutype mkuu, utansamehe ktk hili******
 
Mchawi hawez kugusa familia yako kama lazima mmoja wa famila yupo kwa kundi hilo likiwa

Uchawi uwezi kuutenganisha na familia ndugu.Mzazi au wazazi kwani familia za hivo huwa hakuna maendelea,watu hufa katika mazingira ya kutatanisha,umaskini nk nimefanya utafiti huwo kwenye kooo nyingi za kichaga utakuta wale wenye hayo mambo ni wahanga wa setback.Ndio maana sina hakika sana wamama au wababa walikuwa lazima wawe na mtoto nje ya ukoo ule ili laana za uchawi au mizimu zisiwamalize wote mmoja awe amesalimika
 
Pole sana!
ila hofu yangu ni moja! ku deal na mchawi lzm utumie uchawi pia vinginevyo butimba itakuhusu! nenda kiafrika zaidi anza na ramri ukimjua nawe mrushie kombora mgawane maumivu!

Mkuu usimdanganye....Mchawi huwezi kushindana nae kichawi....Mkabidhi MUNGU ndo anamudu hayo manguvu ya GIZA sikiliza Mchawi mpaka anakuroga ujue kuna mlango ameupata...kumbuka pia mganga na mchawi wote ni sawa.....so utataabika sana...sisi wengine tumetaabishwa na wachawi kwa muda mrefu natulipambana kweli kweli kutumia waganga mwisho siku imebidi kumrudia MUNGU wa kweli na maisha yamekuwa Rahisi so acha kabisa kumshauri mtu aende kwa mganga ataharibikiwa kabisa
 
Pole sana mkuu @Counseller. Wachawi ni washenzi sana. Mkuu wangu ninakuomba kama ukimpata mganga wa kuweza kusitisha roho ya huyo mchawi basi tuwasiliane PM nimpate maana kuna ndugu yangu tatizo kubwa sana. Dawa ya moto ni moto si maji. Liwalo na liwe. Kama hayajakufika huwezi kuwaza kama mimi Zogwale hapa.

Ndg yangu Zogwale sijui imani yako niipi ila kama una huyo ndg yako anataabishwa na wachawi or Mizimu sikushauri ushindane na mchawi Kichawi hutaweza.....Tambua kwamba wachawi hadi wanakufanyia majanga....huwa wanatoa makafara makubwa nailia ujinasue lazima ujue kafara aliyotumia ili ulipe hiyo Gharama then ndio ujue namna yakujinasua sio..Ishu ndogo km inavyofikiriwa kuna watu wamewekeza kwa shetani above 100% acha kabisa nakupa mfano wangu Mimi kuna MTU aliniharibia maisha Kafara aliyotumia alichukua.. sehemu za SIRI za wanawake wawili....ndio aliniapizi nazo sasa niambie utawezaje kulipa fidia ya Kafara kama hiyo ukienda kwa mganga japokuwa atajua kinachokutesa lkn hatakwambia namna yakujinasua ataishia kula Pesa yako tu....Ingawa sijui imani yako lkn....muamini MUNGU wakweli waganga ni Mawakala wa Shetani watakutesa sana
 
Last edited by a moderator:
Unaweza ukaona ni rahisi sana kupambana na mchawi kupitia waganga, usipoangalia hata wewe unaweza ukaja ukawa mchawi.
Neno la Mungu ndio silaha pekee ya kupambana na mchawi. Vita ya kichawi ni mbaya saaaana. Inakuja kugharimu mpaka watoto wako na kizazi chako.

Kuna watu wanasikia tu habari za wachawi....Ile ndio kz yao wamewekeza kwenye hiyo sasa MTU anakurupuka anataka kumlipa kisasi mchawi sio Rahisi kwakweli km watu wanavyodhani
 
Asante....sana ndugu yangu A.Kunambi.....huo ndio ukweli tatizo watu hawapendi kutafuta maarifa kitu ambacho hawajui Ulimwengu wa Roho unanguvu kuliko huu ulimwengu wa Mwili tunaoishi sisi
 
Last edited by a moderator:
Mtukuze Mungu na kumuomba akulipie kwa huyo mtu ambaye amekufanyia ujinga huo, mkatili sana huyo
 
Uchawi uwezi kuutenganisha na familia ndugu.Mzazi au wazazi kwani familia za hivo huwa hakuna maendelea,watu hufa katika mazingira ya kutatanisha,umaskini nk nimefanya utafiti huwo kwenye kooo nyingi za kichaga utakuta wale wenye hayo mambo ni wahanga wa setback.Ndio maana sina hakika sana wamama au wababa walikuwa lazima wawe na mtoto nje ya ukoo ule ili laana za uchawi au mizimu zisiwamalize wote mmoja awe amesalimika

Ya kweli ayo umeona wachaga tu
 
Unasema hukuuliza mtoto kafa kwa ugonjwa gani halafu unadai karogwa?!! Acha fikra za kizamani Mkuu,

Sasa unasema utalipa kisasi,utamlipia kisasi nani? Ni nani aliyemroga mwanao? Na kulipa kwako kisasi kutakusaidia nini? Sana sana utaingia gharama tu za kwenda kwa Waganga nao watafune Fedha zako!! Rudi Hospitali uliza mwanao alikufa kwa Ugonjwa gani? Achana na mambo ya kishirikina na weka matumaini kwa Mungu ambae ndiye mlinzi wetu wa kweli,

Kumbuka kila binadamu atakufa kwa siku aliyopangiwa na Mungu tu,hakuna kuwahi kufa wala kuchelewa ni maamuzi ya Mungu tu.
 
Agizo hili walipewa wana wa Israel kipindi kile cha sheria/torati, waliambiwa kuwa mwanamke asiichi pia kuna andiko linasema asionekane mchawi kwako/mbele yako. Swali la kwanza la kujiuliza, waliwatambuaje wachawi wakati wao walikuwa wakitembea sana kimwili na sio kiroho kama Kanisa la sasa lilivyo kupitia Roho Mtakatifu? Ukweli ni kwamba walikuwa wakiwatambua wachawi kupitia makuhani, kumbuka kipindi kile Roho hakuachiliwa kwa kila mshirika kama sasa hivi ilivyo. Roho alikuwa anapatikana kupitia makuhani na manabii. Na uchawi huwa unajulikana kwa jinsi ya rohoni (kwa wale ambao wanajua vita vya rohoni watakuwa wananielewa) sasa wale makuhani/manabii na waonaji wakishatambua watu flani ni wachawi walikuwa wanahukumiwa vifo maana ndivyo sheria ya Mussa ilivyoamuru, na sio Mussa ndo alipendekeza hivi, hapana ila ni Mungu.

Swali lingine la kujiuliza ni kwanini awe mwanamke na sio mwanamme mchawi?
Mwanamke ni chombo dhaifu kama maandiko yanavyotuelezea na hata ktk jamii inaonekana hivyo ila Mkuu labda nikwambie tu kuwa MWANAMKE AKISHAKUWA MCHAWI ANAKUWA NI MBAYA KULIKO HATA JAMBAZI. Mwanamke mchawi ni katili sana. Na Mwanamke anatumika sana kumdondosha mwanamme. Kumbuka Ajenda ya Shetani ni kunyanyasa binadamu, unaweza ukawa na ela ila ukawa ni mlevi au fisadi. Kupitia mwanamke mwanamke mchawi shetani anaweza akakuingiza ktk maagano/mikataba au akakuingizia maroho machafu sana na akakuharibia maisha yako ambayo hautakuja kuiona ile mbingu ambayo Mungu ameiandaa kwa ajili yetu wanadamu.
Niongezee kidogo tu kwa kusema kuwa, Mwanamke mchawi ni ngumu kuuacha uchawi au kuundoa ndo maana unaambiwa usimuache akaishi. Mwanamke mchawi yoyote yule huwa uchawi wake upo ktk malango ya uzazi wa mwanamke na kwa mwanaume yapo kichwani. Mwanaume ni mwepesi kuondoa uchawi wake sababu upo kichwani, wachawi wa kiume ni wepesi kuibiwa uchawi wao sababu upo kichwani ila mwanamke ni ngumu kuiba uchawi wake sababu upo ktk malango ya siri. Kwahiyo wanaume wengi hawatakiwi kukabidhiwa uchawi sababu hawadumu nao na raha ya uchawi ni kukaa nao kwa mda mrefu sana, na unapokabidhiwa huo uchawi unashauriwa uutunze na kuulinda. Kumbuka uchawi unapikwa na kuuzwa na mtu huwa anapewa uchawi kutoka kwa falme flani au falme husika na atakuwa anatumika kichawi ndani ya hiyo falme. Kwahiyo hizo falme zikimpa mtu mchawi na kisha kuibiwa wanaona wameingia hasara kubwa sana ndo maana wanawapenda zaidi wanawake sababu ni ngumu kuiba uchawi wao na kisha mwanamke ni katili sana na anaweza akamuangusha mwanamme.
******Naomba niishie hapa, nimechoka kutype mkuu, utansamehe ktk hili******

Natamani nikuone uniongezee ELIMU SIJUI UTANISAIDIAJE!!!!??? Maana ulivyofunguka hadi naona mwanga mweupe mbele yangu
 
Unasema hukuuliza mtoto kafa kwa ugonjwa gani halafu unadai karogwa?!! Acha fikra za kizamani Mkuu,

Sasa unasema utalipa kisasi,utamlipia kisasi nani? Ni nani aliyemroga mwanao? Na kulipa kwako kisasi kutakusaidia nini? Sana sana utaingia gharama tu za kwenda kwa Waganga nao watafune Fedha zako!! Rudi Hospitali uliza mwanao alikufa kwa Ugonjwa gani? Achana na mambo ya kishirikina na weka matumaini kwa Mungu ambae ndiye mlinzi wetu wa kweli,

Kumbuka kila binadamu atakufa kwa siku aliyopangiwa na Mungu tu,hakuna kuwahi kufa wala kuchelewa ni maamuzi ya Mungu tu.
Sio kila kifo ni mpango wa Mungu Mkuu.
 
Katika maisha lazima kujipanga sana ila uwe salama wewe na familia yako kwa lile unaloliamini. Kwa kifupi kama wewe ni mtu wa dini sali sana na kama husali sana basi jiwekee ulinzi wa kutosha. Wachawi wanapenda sana kuloga watoto wadogo au kina mama wajawazito kwa sababu ni rahisi kwao kufanya hivyo. Pole sana ndugu usilipize kisasi ila jipange lililotokea lisitokee tena.

Naomba kujua kwa nn ni rahisi kwa mama mjamzito na mtoto? nahitaji ufahamu tu..
 
Mchawi hawez kugusa familia yako kama lazima mmoja wa famila yupo kwa kundi hilo likiwa
Mchawi ambae anatumika na anajitambua kuwa anaroga ni lazima aue. Kuna mchawi ambae hajitambui kama anatumika kuroga, hii ni hususani wale ambao wanakaribia kupewa uchawi, huwa usiku wanaota ndoto za ajabu ajabu. Mara yupo makaburini, Baharini, yupo sehemu ambayo kuna watu wapo nae na kila atakayemuangalia hawezi kumtambua. Watu wa namna hii huwa wanachukulia na kufanyishwa uchawi bila wao kujua ila NI LAZIMA KWENYE NDOTO AONE VITU FLANI.
Pia kuna hawa wanaotumika na wao wenyewe kujijua, Mchawi lazima aue. Na huwa inafika kipindi anapokosa kafara za nje au akatamani/ikambidi apande ngazi flani ya huwa kafara ya mtu wake wa karibu inahusika sana.
Kinachowasumbua hawa wachawi wadogo ni ile roho ya kichawi ndani yao, asikwambie mtu. Binadamu wa kawaida anaweza asifanye mambo ambayo mchawi anafanya kama kuua ndugu wa karibu au mtu yoyote yule, kunywa damu za watu, kukaa na wachawi wengine n.k kwa hali ya kibinadamu ni ngumu sana ndo maana wanawapandikizia hiyo roho ya uchawi.
Mchawi anapomtoa ndugu yake kafara au anamroga ili aje kufa, akiwa ktk hali ya kibinadamu huwa anaumia vile vile kama ndugu zake wa kawaida wanavyoumia na kulia anaweza kulia, ila akivaa ile roho ya uchawi wakati anaenda kumroga ili aumwe huyo mtu huwa anatamani afe hata apo apo. Anakuwa na ukatili wa kutisha. Na unapoona ktk ukoo wenu kuna jambo baya linatokea basi tambua chanzo kipo ndani ya huohuo ukoo. Na kama ni familia mnateseka basi kuna anayewajua vema ndo anawachezea, tena inawezekana kabisa akawa anashirikiana na ndugu zenu.
 
Easymutant sio kweli kwamba ni kwa mama na watoto tuu. Na wala sipingi moja kwa moja ila nitakujibu kama ifuatavyo.
Kwa Wamama wajawazito huwa wanamtaka huyu mtoto tuu. Yawezekana wanataka kumuua mtoto, kumteka mtoto, kuchukua baadhi ya viungo vya mtoto n.k hii yote ni kwa ajili ya ulozi/uchawi.
Wamama Wajawazito wanafatiliwa na mauti ya watoto zao na wao wenyewe pindi wakiwa wajawazito. Na ktk ulimwengu wa roho yawekana kuna vitu anavihisi ama kuviota. Hivyo vitu kwa asilimia kubwa huwa ni kweli kabisa.
Wachawi wanaenda mahospitalini kwenye chumba za kujifungulia ili kuchukua damu za wamama pindi wajifunguapo. Ama kwenda kuchukua baadhi ya viungo vya mtoto, kama kitovu, nyota, damu n.k
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom