Bi nyakomba
JF-Expert Member
- Mar 23, 2012
- 385
- 104
Pole sana ndugu najua maumivu na sononi uliyonayo mpendwa ktk kipindi hili. Nakushuhudia,Mimi mwenyewe nilifiwa na Mwanangu wa miezi 8 ghafla alichomwa sindano ya maleria mchana akafariki usiku. hakua amezidiwa. nilibaki na maumivu yasioisha., nilikaribia kupata stroke kwa mawazo. nilishauriwa na Dr kupunguza mawazo ili nijiokoe. hakika ni maumivu yanayonitesa kila siku. niliamua kumkimbilia Mungu, maana yy ndo aliruhusu hilo litokeee. na angetaka mwanangu aishi Angeishi. hiyo ni mwezi wa 4.mpk Leo naona kama ni Jana tu. kila nikikumbuka naishiwa nguvu,moyo unaenda mbio. nalia machozi yasioisha.RIP my son. pole na wewe mdg yangu. Tumkimbilie Bwana Yesu tu. limeshatokea. Mungu akutie nguvu