Kwako na kwa baadhi ya wana Jf pia.
...Mtoto anapozaliwa hususani hospitalini, kile chumba za kujifungua huwa kunakuwapo na wachawi wengi sana. Ni ngumu kuwaona ktk macho ya nyama ila ni wapo mule. Wakiwa mule ndani huwa wanakuja chukua vitu vifuatavyo
1. Damu inayotoka kwa mmama anayejifungua, damu ndio kinywaji cha majini na wachawi. Pia mda mwingine huwa wanabatiza kupitia damu za watu, hii ni stage ya juu ktk uchawi.
2. Vitovu vya watoto, vitovu vya watoto huwa vinatumika hususani ktk mauaji, ushawahi kusikia mtu anaumwa ghafla anakonda kama anaumwa UKIMWI kisha akafa, yaani hachukui hata wiki mbili? Basi hiyo ni moja ya shughuli za kitovu cha mtoto, ni KUUA. Kitovu pia kinaweza kutumika kuhifadhia uchawi, kitovu pamoja na malango ya uzazi. Kama wachawi wanataka kumpa mtoto mikoba na kumwandaa mapema huwa wanafanya hiki kitu.
3. Nyota ya mtoto, mtoto tangu akiwa tumboni mwa mamaye mchawi anaweza tambua nyota ya mtoto.
4. DAMU (Hii ndo MBAYA ZAIDI) Damu ni uhai wa mtu yaani ndio nafsi kamili ya mtu. Wanapochukua damu ya mtu ina maana Uhai kamili wa mtoto upo kwao, yule mtoto anaweza akalelewa kuzimu au na kituo cha wachawi na ninyi watu kwenye jamii msijue. Watoto wanaochukuliwa damu na wachawi tangu wakiwa wadogo wakifika miaka ya 16 na kuendelea huwa wanakuwa wachawi ktk kiwango cha hali ya juu sana, na kadri siku zinavyozidi kwenda ndo anavyozidi kupanda kiwango. Na kama mtoto huyo amechukuliwa damu akiwa anazaliwa na kulelewa kuzimu, akafika miaka flani hivi huwa wanapotea kabisa jamii au huwa wanakufa ktk hali isiyoleweka. Kinachotokea hapo ni kumchukua huyo mtoto moja kwa moja. Watoto hawa huitwa JINI JIWE (Yaani ameunganishwa na ufalme wa majini tangu akiwa tumboni mwa mama yake). Inawezekana mama yake akawa anajua au asijue.
Vipo vitu vingi sana watoto wetu wanapozaliwa kama hawana kinga ya Mungu mambo hayo hutokea.
TURUDI KWENYE MADA.
Ukiona kifo chochote cha ghafla, inawezakana ni kweli ni mapenzi ya Mungu ama ni ya Ibilisi. Wachawi huwa wanatumia mbinu flani ktk kuua na inawezakana kwa mtoto wako ikawa ni hivyo.
Huwa wanatuma Jini kwa huyo mtoto, lile jini likishamwingia huyo mlengwa wachawi wanakuja kumchukua yule mtoto halisi ambae ni wa kwako kisha wao wanaacha lile jini. Kwahiyo kwa macho ya kibinadamu unaona ni mtu ila sio mtu. Na Jini hilo sharti ni kuishi SIKU 7 TUU. Likiendeleza hapo mnaweza mkagundua mabadiliko ndani ya mtoto, anaweza akakataa vitu vya kawaida na hata maumbile yake yakabadilika. Ama hilo jini linaweza kuishi zaidi ili kuwadhoofisha na kuwanyanyasa ndugu wanaoishi na huyo mtu. Kwahiyo kama ni mipango ya Ibilisi basi tambua yule hakuwa mtoto ila lilikuwa ni hilo jini ambalo lilipaswa kukaa ndani ya siku 7 tuu ili kuonesha mauti kwa mtoto. Na kikawaida mtu ukishachukuliwa nafsi yako, akija Mtumishi wa Mungu kukuombea, anaweza kuirejesha nafsi ya huyo mtu. Hata kama madaktari wakisema huyo mtu kafa ila kama hajafa kwa mapenzi ya Mungu ila ni nafsi tu imechukuliwa basi uhai wa huyo mtu waweza kurudi.
Kwahiyo kama ni nguvu za zimemuondoa mwanao basi tambua mlichozika sio mtu, ndo maana unaambiwa hata mtu akichukuliwa msukule huwa hawaziki mtu.
***USHAURI WANGU KWAKO***
Mpe Yesu maisha yako, hakuna njia mbadala wa kupambana na mchawi mbali na YESU. Usiende kwa Mganga maana Mganga ndie mchawi mwenyewe. Sitaweza kueleza sana juu ya hili kwa Post ila amini nikuambiacho.
Sababu kubwa ya wewe hayo yote kukutokea ni kutokumpa Yesu maisha yako, Mkuu OKOKA na usimame kweli kweli kwenye wokovu. Shetani hajawahi kumshinda Mungu, hao waganga nao ni wafuasi wa shetani ndani ya dunia hii.
Karibu ndani ya Yesu, ukiingia ktk vita hii na wachawi pasipo Yesu utakuja kujijutia tuu.
Amina.