Mmeibia Nchi Hii Kwa Muda Mrefu Na Sasa Ni Lazima Muisome number kama Wakazi wa Mabondeni.
Wizi hauna kabila .
Uhalifu hauna kabila na wale wanovunja sheria wanatakiwa kuadhibiwa.
Pia ukichunguza wizi uliotikisa hii nchi hapakua na wachaga.
EPA.
MEREMETA
RICHMOND
ESCROW
Uuzwaji wa kupeana wa Nyumba za Serikali
Uuzwaji wa mashirika ya umma kwa bei za rushwa.
Kuvunjwa kwa azimio la Arusha ili kuweka mazingira mazuri ya kuiibia serikali.
Mtumishi mmoja wa serikali kumiliki Majumba 73 kwenye eneo moja.
Uuzwaji wa Loliondo.
Mikataba ya gesi yenye harufu ya rushwa.
Sakata la uuzwaji wa UDA.
Ununuzi wa feri chakavu kwa bei ya kuruka.
Mabehewa feki.
Kiwira
Uuzwaji wa bei poa wa kilimanjaro hotel.
Uchafu wa majiji na miji kutokana na kushindwa kwa wakurugenzi.
Kuvunjika kwa maadili ya vijana na wazee kila kona ya nchi kutokana na tamaa ya fedha pia hufanywi na wachaga peke yao.
Tafakari kabla ya kubagua watu kwa misingi ya ukabila.
Wizi wa kura.
Mashule yanayotoa elimu kimagendo yaliyojaa nchi nzima pia hayamilikiwi na wachaga.
Biashara za madawa ya kulevia .
Ununuzi wa rada.
N.k.
Yote niliyotaja hapo juu ni ufisadi mkubwa uliolitia hasara taifa letu.
Na hapakua na uchaga kwenye huo ufisadi lakini linapokuja suala la madaraka ndipo watu wanawabagua wachaga.
Nadhani hii ni promotion na propaganda zinazofadhiliwa na mafisadi waliojichimbia kwenye uongozi wa nchi ili waendelee kuihujumu nchi.
Mfano tu uko wazi Bazili Mramba alikua waziri wa fedha kipindi cha Mkapa na akakuza sana uchumi wa nchi na kudhibiti thamani ya fedha yetu lakini utawala uliofuata uliingia kwa majungu na kumpeleka gerezani kwa sababu tu alikua mchaga ili wapate nafasi ya kuiba fedha za umma.
Mkulo alivuruga alituhumiwa sana lakini hakupelekwa gerezani kama Mramba.
Mrema alikataa ufisadi uliofanywa kwenye sakata la Chavda na akafukuzwa kwa sababu ya uchaga wake ili waroho wa mali za umma wapate nafasi ya kuiibia nchi.
Agrey Mwanry alikuatendaji bora kuliko waziri wake lakini uchaga wake ukamponza.
Mbowe ndiye mwenyekiti bora wa chama kuliko wenyeviti wa vyama vyote nchini lakini kwa sababu ya uchaga wake anaambiwa hajafanya kitu.
Fikiri sawa sawa kwa kutumia akili yako mwenyewe.