Mchungaji Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini (CHADEMA), aliiambia Nipashe kwenye viunga vya Bunge jana kuwa wameshangazwa na uongozi wa Bunge kurejesha fedha serikalini wakati kuna mambo mengi ya msingi ya Bunge hayajafanyika, kutokana na ukosefu wa fedha.
"Kamati zingine zimezuiwa kusafiri wa maelezo kwamba hakuna fedha. Kamati ya Mambo ya Nje imezuiwa kusafiri kwa madai kuwa hakuna hela, walitarajia kwenda kuangalia nyumba za ubalozi huko nje, lakini wanaambiwa hakuna fedha, wakati pesa nyingi imerejeshwa serikalini," alisema.
Jamani kazi zingine za kamati zetu zinatia mashaka, kama hiyo hapo! Unatoka bongo na unakwea pipa kwenda kuangalia nyumba za ubalozi, wajemeni hivi kweli hivi kwelii?