Wabunge wapinga billlioni 6 kurejeshwa Serikalini

Wabunge wapinga billlioni 6 kurejeshwa Serikalini

Msigwa analalamika kuwa wabunge wameshindwa kusafiri nje ya nchi kwenda kuangalia balozi? Kila mwaka wamekuwa wanasafiri kuangalia kitu hicho hicho, nchi imepata faida gani? Na kwa 'akili kubwa' ya Msigwa bora wabunge wapande ndege kwenda kushangaa majengo Ulaya kuliko watoto kukaa kwenye madawati? Naomba kuuliza kwenye jimbo la huyo mchungaji shida kubwa waliyonayo wananchi ni wabunge kutokwenda Ulaya?

Bunge limekuwa ni chanzo cha umaskini nchi hii.
Mbona unamwongelea Msigwa tu? Kwani ni yeye peke yake anayelilia hizo Bil 6??



_DSC8735.JPG
 
Sijawah kumwamini huyu msigwa, jamaa ni mchumia tumbo kwa kwenda mbele
 
Kila fedha inayoonekana kukosa kazi inaambiwa iende kwenye madawati, kila siku madawati tu, au kuna shule zinazouza madawati?
Kila ukimwandikisha mtoto shule unaambiwa changia pesa ya madawati ila akimaliza shule hupewi hilo dawati
 
Hizi fedha zilitosha kabisa kugharamia shughuli nyingine muhimu za kibunge kama kurushwa matangazo ya bunge na chenji ingebaki.

Hili suala la madawati ya shule naona wanasiasa wanalishadadia kisiasa zaidi.
Kurusha matangazo ya bunge na dawa lipi la kichumi zaidi! Matangazo ya bunge wakati kuna mambo kibao ya muhimu hii nchi! Kurusha matangazo ya bunge wakati watu hawana dawa ni upuuzi.
 
pic+mps.jpg


WABUNGE wa upinzani na wa CCM, wamekosoa uamuzi uliofanywa na uongozi wa Bunge wa kurejesha Sh. bilioni sita serikalini ilhali baadhi ya shughuli za Bunge zimekwama kutokana na uhaba wa fedha.

Aidha, baadhi ya wabunge hao wamedai Rais Dk. John Magufuli, amekuwa akiingilia majukumu ya mihimili mingine, likiwamo Bunge.

Aprili 11, mwaka huu, uongozi wa Bunge ulimkabidhi Rais Magufuli hundi ya Sh. bilioni sita, ambazo ulieleza kuwa uliziokoa kutokana na kubana matumizi.

Rais Magufuli aliupongeza uongozi huo na kuagiza fedha hizo zitumike kutengeneza madawati, huku akizitaka ofisi na taasisi zingine za serikali kuiga mfano huo.

Katika kikao cha wabunge na uongozi wa Bunge hilo kilichofanyika mjini hapa juzi, kuanzia saa 11 jioni hadi saa 2:15 usiku, wabunge waliukosoa uongozi wa Bunge kwa uamuzi huo kwa vile "shughuli nyingi za Bunge zimekwama kutokana na uhaba wa fedha."

Katika mkutano huo, waandishi wa habari walizuiwa kushiriki kwa maelezo kuwa ulikuwa maalum kwa ajili ya maelekezo kwa wabunge.

Mchungaji Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini (CHADEMA), aliiambia Nipashe kwenye viunga vya Bunge jana kuwa wameshangazwa na uongozi wa Bunge kurejesha fedha serikalini wakati kuna mambo mengi ya msingi ya Bunge hayajafanyika, kutokana na ukosefu wa fedha.

"Kamati zingine zimezuiwa kusafiri wa maelezo kwamba hakuna fedha. Kamati ya Mambo ya Nje imezuiwa kusafiri kwa madai kuwa hakuna hela, walitarajia kwenda kuangalia nyumba za ubalozi huko nje, lakini wanaambiwa hakuna fedha, wakati pesa nyingi imerejeshwa serikalini," alisema.

Kadhalika, Mchungaji Msigwa alisema wabunge pia walihoji sababu za kuzuiwa kuonyeshwa moja kwa moja kwa shughuli za Bunge, jambo ambalo alidai limelenga kuminya uhuru wa vyombo vya habari nchini na "kuficha uovu ya serikali."
"Shughuli za Bunge hazionyeshwi moja kwa moja na vyombo vya habari, lakini anachokifanya Rais kinaonekana. Wabunge tulihoji uongozi wa Bunge kuhusu uamuzi huu," alisema.

Msigwa aliongeza kuwa katika mkutano huo, Mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA), Joseph Mbilinyi 'Sugu', alikwenda mbali zaidi akidai Rais Magufuli amekuwa akiingilia madaraka ya mihimili mingine.

Sugu alikumbushia 'kilio cha wapinzani' kuhusu uteuzi wa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Akson.

Rais Magufuli alimteua Dk.Tulia kuwa mbunge wa kwanza ikiwa ni siku mbili baada ya kuteuliwa na Kamati Kuu ya CCM kuingia kwenye ‘tatu bora’ ya kuwania Uspika, jambo ambalo Sugu alidai linatoa taswira Rais alitumia mamlaka yake kumweka kuwa Naibu Spika.

Mbunge wa Igunga (CCM), Dk. Dalali Kafumu, alisema fedha za Bunge kutumika kununua madawati si jambo baya, lakini wabunge walipaswa kushirikishwa kabla ya kufanyika kwa uamuzi wa kurejesha fedha serikalini.

"Uamuzi wa kutengeneza madawati na kila Mbunge kupewa 600 apeleke jimboni kwake ni mzuri, tatizo wabunge hawakushirikishwa," Dk. Kafumu alisema.

Aliongeza kuwa: “Pia wabunge wa Muungano walihoji jana (juzi) kuhusu kutohusishwa kwao katika mpango huo wakati fedha zilizorejeshwa serikalini ni za Bunge la Muungano, wao hawapewi madawati maana Zanzibar ina Wizara ya Elimu inayojitegemea. Uongozi wa Bunge uliahidi utaangalia namna ya kushughulikia malalamiko yao."

Mbunge mwingine wa CCM ambaye hakuwa tayari jina lake litajwe gazetini, aliiambia Nipashe kuwa haungi mkono uamuzi wa kurejeshwa fedha serikalini kutokana na kusafiri kwa shida akiwa na moja ya kamati za Bunge hivi karibuni.


Chanzo: Nipashe
Pato la Tzs.12m/- kwa mwezi linalalamikiwa kwa hoja ya kuingilia mihimili mingine. By the way, balozi zetu huko nchi za nje either zimepanga nyumba au serikali imejenga yenyewe kwa ajili ya shughuli na makazi yao. Dunia nzima inajua kama umekodi nyumba ni jukumu la mwenye nyumba aishughulikie mwenyewe kama kuna tatizo. Kama nyumba ni yako na inahitaji marekebisho huitaji mjomba aje aione kwanza kwa gharama zako. Ni juzi tu Bw. Msigwa ameandika uzi hapa JF kuhusu MCC akitoa hoja yeye "kama waziri wa mambo ya nje" (Not a shadow minister). This guy hana sura yoyote ya kuwatetea wananchi. Its all about "mimi".
 
Napendekeza kufuta posho zote kwa wabunge waimarishiwe mishahara tu
Pesa imepelekwa kutengeneza madawati,na kila mbunge atapewa madawati 600 wanalalamika
Walizoea kula nyama choma na wengine kususa kila wanapojisikia ilhali wamekomba posho
Yaani inatakiwa vyeo vyote vya kisiasa kuanzia mawaziri,wabunge na kushuka chini mishahara na marupurupu ishuke sana ili kwanza watu wasiache taaluma zao na kukimbilia siasa kwa tamaa ya pesa,ifike mahali mtu ajiulize anagombea ubunge wa nini kwanza hakuna maslahi lakini sasa hivi kama unavyo ona watu wapo kimaslai tu
 
Wamezoea kulala usngizii na kula bure ndo wakome, wafanye kazi au warudi kijijini wakalme


Wauza Sura ndiyo hawa wabunge wa viti maalumu sasa wapo DUBAI hapo. MAGU NA SAFARI ZA NJE MARUFUKU KABISA. TANZANIA ITAJENGWA NA WENYE MOYO.
photo6.JPG
 
Yaani inatakiwa vyeo vyote vya kisiasa kuanzia mawaziri,wabunge na kushuka chini mishahara na marupurupu ishuke sana ili kwanza watu wasiache taaluma zao na kukimbilia siasa kwa tamaa ya pesa,ifike mahali mtu ajiulize anagombea ubunge wa nini kwanza hakuna maslahi lakini sasa hivi kama unavyo ona watu wapo kimaslai tu
AMEN AMEN AMEN WATANZANIA WAMEAMKA NA ASANTE SANA JAMII FORUM KWA KUTUPA HII FORUM.
 
MBONA MADAKTARI WANAJIHUSISHA NA SIASA!!!!!!!!.

CHA AJABU NINI UILICHOONA WEWE!!!!!!!!!!
FUATILIA SANA SIYO KAWAIDA SANA KWA WACHUNGAJI WALA MADAKTARI KUJIHUSISHA NA SIASA ILA WAPO WACHACHE. LABDA NI WALE AMBAO WALIINGIA UCHUNGAJI AU UDAKTARI LAKINI HAWAKUWA NA WITO NA KAZI HIZO.
 
Kurusha matangazo ya bunge na dawa lipi la kichumi zaidi! Matangazo ya bunge wakati kuna mambo kibao ya muhimu hii nchi! Kurusha matangazo ya bunge wakati watu hawana dawa ni upuuzi.
KASHUGHULUKIENI MAENDELEO YA WANANCHI MTAONEKANA KWENYE MTANDAO KAMA MAGU, SIYO KWA DRAMA WANAZOZIFANYAGA AKINA SUGU BUNGENI.
 

Yes, tunataka safari za nje zikomeshwe. Na safari hizi zinawahusu wabunge wote. Hapa sioni umuhimu wa kuweka picha za Msigwa au Mwanjelwa kama vile hao ndio pekee wanaosafiri nje. Hili ni tatizo kubwa zaidi ya hapo. Tujiongeze zaidi wakati tunajadili suala hili badala ya kuchukua watu wawili/watatu na kuanza kuwasakama.
 
Huyo Msigwa jimboni kwake ana shule ina walimu wanne tu, Aibu kubwa sana ndani ya manispaa unakua na shule yenye walimu wanne wakati shule zingine ndani ya manispaa hiyo hiyo zina walimu mpaka 50 ameshindwa hata kuongea na afisa elimu au kumbana mkurugenzi ahamishe walimu kutoka shule zingine na kuwapeleka huko. Meya chadema, diwani chadema mbunge chadema wao wanaangalia matumbo yao. ni Aibu sana kutaka fedha wakazitumbue badala ya kwenda kuwasaidia wananchi
ulichokiandika hakiendani na uhalisia,,anaeajiri walimu na kuwapangia vituo ni msigwa au huyo meya wa chadema


jiongeze,halafu alichokiongea msigwa ni kuhusu bunge kuzidiwa majukumu huku pesa ilotakiwa kufanya hayo haionekani so sidhani kama msigwa anakosa ama tatizo maana waliolalamika sio msigwa pekeake hata wabungr wa ccm wamelalamika.



kunamuingiliano wa kimamlaka kati ya rais na bunge,inaonekana kabisa bunge linakosa weledi wakufanya shughuli zake kwa uhuru maana kinachoonekana ni serekali kama imejivika madaraka ya kutoa maelekezo nini bunge wafanye na nini wasifanye
 
Wabunge wanataka kwenda nje kukagua nyumba?

6.JPG

UJUMBE wa Tanzania ukiongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, wakiwa kwenye picha ya pamoja na zawadi waliyopewa na Mwana Mfalme Prince Bandar bin Saud bin Mohammad Al-Saud, ambaye pia ni Rais wa Mamlaka ya Wanyamapori ya Saudi Arabia. Wengine kutoka kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dk. Adelhem Meru; Balozi wa Tanzania Saudi Arabia, Profesa Abdillah Omari; Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli; Waziri Kivuli wa Maliasili na Utalii, Peter Msigwa; Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan Kijazi na Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Herman Keraryo.
 
Back
Top Bottom