mkonongo1938
JF-Expert Member
- Jan 22, 2016
- 1,990
- 2,403
Hizo nyumba za balozi hata wakiziangalia hawasaidii chochote.. Lakini Mh Magufuli please usiingilie muhimili wa bunge.. Acha kila muhimili ujitegemee
Kama msigwa analilia kusafiri kukagua nyumba za mabalozi kana kwamba yeye ni CAGHawa wabunge wengine ni majipu
Acha ujinga wewe!, unatumia miguu yaani watoto wakae chini wao waende kufanya tour kwenye ubalozi!Hizi fedha zilitosha kabisa kugharamia shughuli nyingine muhimu za kibunge kama kurushwa matangazo ya bunge na chenji ingebaki.
Hili suala la madawati ya shule naona wanasiasa wanalishadadia kisiasa zaidi.
walie tu,.. hawa wamekua wakifanya ubunge biashara kwamba wanatumia fedha kununua halafu wakiingia ndani ya mjengo ndio inaanza biashara ya kurudisha na kutengeneza faida. eti safari za nje wakati walisikia rais kapiga stop safari za nje. umma unaelewa kama bunge lilikua linaongoza kwa ubadhirifu. wakiwa bungeni posho ya makalio kwa kazi yenye mshahara kwa ajili ya kukaa. wakiwa nje ya bunge posho ya makalio kwa vikao vya kamati na safari sizizokua na mwisho nje ya nchi eti kujifunza. bunge gani inararua namna hii hela ya umma bila hata ya huruma!.. sasa sijui msigwa anafikiri bunge linaweza kuepuka madaraka ya rais? tunajua wamezoea ulaji na msuguano na rais hautaepukika lakini jpm atawashinda.![]()
WABUNGE wa upinzani na wa CCM, wamekosoa uamuzi uliofanywa na uongozi wa Bunge wa kurejesha Sh. bilioni sita serikalini ilhali baadhi ya shughuli za Bunge zimekwama kutokana na uhaba wa fedha.
Aidha, baadhi ya wabunge hao wamedai Rais Dk. John Magufuli, amekuwa akiingilia majukumu ya mihimili mingine, likiwamo Bunge.
Aprili 11, mwaka huu, uongozi wa Bunge ulimkabidhi Rais Magufuli hundi ya Sh. bilioni sita, ambazo ulieleza kuwa uliziokoa kutokana na kubana matumizi.
Rais Magufuli aliupongeza uongozi huo na kuagiza fedha hizo zitumike kutengeneza madawati, huku akizitaka ofisi na taasisi zingine za serikali kuiga mfano huo.
Katika kikao cha wabunge na uongozi wa Bunge hilo kilichofanyika mjini hapa juzi, kuanzia saa 11 jioni hadi saa 2:15 usiku, wabunge waliukosoa uongozi wa Bunge kwa uamuzi huo kwa vile "shughuli nyingi za Bunge zimekwama kutokana na uhaba wa fedha."
Katika mkutano huo, waandishi wa habari walizuiwa kushiriki kwa maelezo kuwa ulikuwa maalum kwa ajili ya maelekezo kwa wabunge.
Mchungaji Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini (CHADEMA), aliiambia Nipashe kwenye viunga vya Bunge jana kuwa wameshangazwa na uongozi wa Bunge kurejesha fedha serikalini wakati kuna mambo mengi ya msingi ya Bunge hayajafanyika, kutokana na ukosefu wa fedha.
"Kamati zingine zimezuiwa kusafiri wa maelezo kwamba hakuna fedha. Kamati ya Mambo ya Nje imezuiwa kusafiri kwa madai kuwa hakuna hela, walitarajia kwenda kuangalia nyumba za ubalozi huko nje, lakini wanaambiwa hakuna fedha, wakati pesa nyingi imerejeshwa serikalini," alisema.
Kadhalika, Mchungaji Msigwa alisema wabunge pia walihoji sababu za kuzuiwa kuonyeshwa moja kwa moja kwa shughuli za Bunge, jambo ambalo alidai limelenga kuminya uhuru wa vyombo vya habari nchini na "kuficha uovu ya serikali."
"Shughuli za Bunge hazionyeshwi moja kwa moja na vyombo vya habari, lakini anachokifanya Rais kinaonekana. Wabunge tulihoji uongozi wa Bunge kuhusu uamuzi huu," alisema.
Msigwa aliongeza kuwa katika mkutano huo, Mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA), Joseph Mbilinyi 'Sugu', alikwenda mbali zaidi akidai Rais Magufuli amekuwa akiingilia madaraka ya mihimili mingine.
Sugu alikumbushia 'kilio cha wapinzani' kuhusu uteuzi wa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Akson.
Rais Magufuli alimteua Dk.Tulia kuwa mbunge wa kwanza ikiwa ni siku mbili baada ya kuteuliwa na Kamati Kuu ya CCM kuingia kwenye ‘tatu bora’ ya kuwania Uspika, jambo ambalo Sugu alidai linatoa taswira Rais alitumia mamlaka yake kumweka kuwa Naibu Spika.
Mbunge wa Igunga (CCM), Dk. Dalali Kafumu, alisema fedha za Bunge kutumika kununua madawati si jambo baya, lakini wabunge walipaswa kushirikishwa kabla ya kufanyika kwa uamuzi wa kurejesha fedha serikalini.
"Uamuzi wa kutengeneza madawati na kila Mbunge kupewa 600 apeleke jimboni kwake ni mzuri, tatizo wabunge hawakushirikishwa," Dk. Kafumu alisema.
Aliongeza kuwa: “Pia wabunge wa Muungano walihoji jana (juzi) kuhusu kutohusishwa kwao katika mpango huo wakati fedha zilizorejeshwa serikalini ni za Bunge la Muungano, wao hawapewi madawati maana Zanzibar ina Wizara ya Elimu inayojitegemea. Uongozi wa Bunge uliahidi utaangalia namna ya kushughulikia malalamiko yao."
Mbunge mwingine wa CCM ambaye hakuwa tayari jina lake litajwe gazetini, aliiambia Nipashe kuwa haungi mkono uamuzi wa kurejeshwa fedha serikalini kutokana na kusafiri kwa shida akiwa na moja ya kamati za Bunge hiviavuna karibuni.
Source: Nipashe
Hata mimi pia ! Nimegundua hata wapinzani Wa nchi hii ni wachumia matumbo tu !!!Yaani umewapa za uso. Eti wanataka kwenda kuangalia nyumba za balozi zetu!!!! Kwa hali hiyo sioni faida ya bunge!!!!
Kwa hiyo kwako ,wewe fedha za wizara moja ni ndogo, kwako??,kwenda kwenye tour ni mhimu kwako ???Wabunge waianshi kimalaika kuliko wakurugenzi wa idara za serikali??
Umewahi kuulizia TANAPA na TPDC na UWERA na BoT na kweingineko wanaishije hao wakurugenzi??
After all budget ya bunge kwa mwaka ni ndogo sana, pamoja na kulipwa posho hizo, inapelekana tu na bajeti ya wizara moja ya serikali.
Wewe utakuwa ni Mhasibu wa SACCOS! Ha ha ha ha.....!Kweli. Ki uhasibu pale fedha inapobaki kwenye mwaka mmoja wa fedha huwa carried forward kwenye mwaka mwingine wa pesa... Na sio kurudishwa ilipotoka...
Kwa hiyo wewe na msingwa mnataka kwenda kuangalia nyumba za mabaloz teh teh teh akili ni nyweleNi kweli mkuu.
Hayo ndio matatizo ya vyeo vya kupewa, lazima utoe ushirikiano vinginevyo unapigwa pending tu...