Tatizo ni kubwa zaidi ya hapa. Tusiwaonee tu hawa akina dada. Wabunge wote wamefuja fedha za umma kwa safari nying zisizokuwa na tija. Kila mtu anajua hivyo.
ulichokiandika hakiendani na uhalisia,,anaeajiri walimu na kuwapangia vituo ni msigwa au huyo meya wa chadema
jiongeze,halafu alichokiongea msigwa ni kuhusu bunge kuzidiwa majukumu huku pesa ilotakiwa kufanya hayo haionekani so sidhani kama msigwa anakosa ama tatizo maana waliolalamika sio msigwa pekeake hata wabungr wa ccm wamelalamika.
kunamuingiliano wa kimamlaka kati ya rais na bunge,inaonekana kabisa bunge linakosa weledi wakufanya shughuli zake kwa uhuru maana kinachoonekana ni serekali kama imejivika madaraka ya kutoa maelekezo nini bunge wafanye na nini wasifanye
Ni muhimu watu wajue kinachoendelea na hawa watu naelewa unaweza ukawa una maslahi yako binafsi lakini maslahi ya wengi tunayasahau. Issue ni kwamba hawa wabunge wanadhani wamewekwa kwa ajili ya kusafiri wakati watoto wa shule zetu za kata wana kaa chini. Naweka picha ili wanaotaka kuona ukweli wenyewe ni kwamba wabunge wa CCM na UKAWA majority wako pale kwa ajili ya maslahi yao na familia zao na sio umma wa watanzania.Yes, tunataka safari za nje zikomeshwe. Na safari hizi zinawahusu wabunge wote. Hapa sioni umuhimu wa kuweka picha za Msigwa au Mwanjelwa kama vile hao ndio pekee wanaosafiri nje. Hili ni tatizo kubwa zaidi ya hapo. Tujiongeze zaidi wakati tunajadili suala hili badala ya kuchukua watu wawili/watatu na kuanza kuwasakama.
Ni muhimu watu wajue kinachoendelea na hawa watu naelewa unaweza ukawa una maslahi yako binafsi lakini maslahi ya wengi tunayasahau. Issue ni kwamba hawa wabunge wanadhani wamewekwa kwa ajili ya kusafiri wakati watoto wa shule zetu za kata wana kaa chini. Naweka picha ili wanaotaka kuona ukweli wenyewe ni kwamba wabunge wa CCM na UKAWA majority wako pale kwa ajili ya maslahi yao na familia zao na sio umma wa watanzania.
Siwaonee kitu chochote wanao onewa ni Watanzania ambao wanakula mlo mmoja na wana watoto wao wanaosoma shule za Kata na wana kaa chini. Probably hawa watoto wao wanasoma medium English school kama Feza. Hawa watu wanapeta na wanafanya matanuzi kiraini sana.Tatizo ni kubwa zaidi ya hapa. Tusiwaonee tu hawa akina dada. Wabunge wote wamefuja fedha za umma kwa safari nying zisizokuwa na tija. Kila mtu anajua hivyo.
Lakini Msigwa ndiye aliye toa kauli ya kwamba wanataka wakatembelea ofisi za Ubalozi. Kuzero kwa Msigwa ni fair kabisa.Nafikiri Mkuu una ajenda yako na Msigwa. Maana naona wewe ume-zero in kwa Msigwa kama vile yeye ndiye tatizo pekee katika suala hili. Mimi nilitaka tujadili tatizo kwa upana wake kwa sababu hii si issue ya mbunge mmoja. Lakini naona unajadili issue hii kisiasa zaidi.
Pole ila tu Mkuu hawa watu wanatakiwa waamke kutoka kwenya huo usingizi vinginevyo wataisoma namba.Maslahi niyatoe wapi tena mkuu, mimi si Mbunge!
Je hesabu za serikali nazo zinaongoza hivyo? Watu wamezoea kwamba mwaka wa serikali ukikaribia tamati basi fedha kama zimebaki au hazikutumiwa zinatafutiwa matumizi pamoja na kugawana.Kweli. Ki uhasibu pale fedha inapobaki kwenye mwaka mmoja wa fedha huwa carried forward kwenye mwaka mwingine wa pesa... Na sio kurudishwa ilipotoka...
Huu ndio unafiki na kujipendekeza kwa wanatanzania wengi, wanajinafikia hata nafsi zao, wanarudisha pesa lakini wanashindwa kurusha matangazo ya bunge, huyo mkubwa na mdogo wake wapunguziwe mishahara ili waone jinsi kazi inavyokua ngumu ikiwa hakuna pesa ya kutosha hio kazi.![]()
WABUNGE wa upinzani na wa CCM, wamekosoa uamuzi uliofanywa na uongozi wa Bunge wa kurejesha Sh. bilioni sita serikalini ilhali baadhi ya shughuli za Bunge zimekwama kutokana na uhaba wa fedha.
Aidha, baadhi ya wabunge hao wamedai Rais Dk. John Magufuli, amekuwa akiingilia majukumu ya mihimili mingine, likiwamo Bunge.
Aprili 11, mwaka huu, uongozi wa Bunge ulimkabidhi Rais Magufuli hundi ya Sh. bilioni sita, ambazo ulieleza kuwa uliziokoa kutokana na kubana matumizi.
Rais Magufuli aliupongeza uongozi huo na kuagiza fedha hizo zitumike kutengeneza madawati, huku akizitaka ofisi na taasisi zingine za serikali kuiga mfano huo.
Katika kikao cha wabunge na uongozi wa Bunge hilo kilichofanyika mjini hapa juzi, kuanzia saa 11 jioni hadi saa 2:15 usiku, wabunge waliukosoa uongozi wa Bunge kwa uamuzi huo kwa vile "shughuli nyingi za Bunge zimekwama kutokana na uhaba wa fedha."
Katika mkutano huo, waandishi wa habari walizuiwa kushiriki kwa maelezo kuwa ulikuwa maalum kwa ajili ya maelekezo kwa wabunge.
Mchungaji Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini (CHADEMA), aliiambia Nipashe kwenye viunga vya Bunge jana kuwa wameshangazwa na uongozi wa Bunge kurejesha fedha serikalini wakati kuna mambo mengi ya msingi ya Bunge hayajafanyika, kutokana na ukosefu wa fedha.
"Kamati zingine zimezuiwa kusafiri wa maelezo kwamba hakuna fedha. Kamati ya Mambo ya Nje imezuiwa kusafiri kwa madai kuwa hakuna hela, walitarajia kwenda kuangalia nyumba za ubalozi huko nje, lakini wanaambiwa hakuna fedha, wakati pesa nyingi imerejeshwa serikalini," alisema.
Kadhalika, Mchungaji Msigwa alisema wabunge pia walihoji sababu za kuzuiwa kuonyeshwa moja kwa moja kwa shughuli za Bunge, jambo ambalo alidai limelenga kuminya uhuru wa vyombo vya habari nchini na "kuficha uovu ya serikali."
"Shughuli za Bunge hazionyeshwi moja kwa moja na vyombo vya habari, lakini anachokifanya Rais kinaonekana. Wabunge tulihoji uongozi wa Bunge kuhusu uamuzi huu," alisema.
Msigwa aliongeza kuwa katika mkutano huo, Mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA), Joseph Mbilinyi 'Sugu', alikwenda mbali zaidi akidai Rais Magufuli amekuwa akiingilia madaraka ya mihimili mingine.
Sugu alikumbushia 'kilio cha wapinzani' kuhusu uteuzi wa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Akson.
Rais Magufuli alimteua Dk.Tulia kuwa mbunge wa kwanza ikiwa ni siku mbili baada ya kuteuliwa na Kamati Kuu ya CCM kuingia kwenye ‘tatu bora’ ya kuwania Uspika, jambo ambalo Sugu alidai linatoa taswira Rais alitumia mamlaka yake kumweka kuwa Naibu Spika.
Mbunge wa Igunga (CCM), Dk. Dalali Kafumu, alisema fedha za Bunge kutumika kununua madawati si jambo baya, lakini wabunge walipaswa kushirikishwa kabla ya kufanyika kwa uamuzi wa kurejesha fedha serikalini.
"Uamuzi wa kutengeneza madawati na kila Mbunge kupewa 600 apeleke jimboni kwake ni mzuri, tatizo wabunge hawakushirikishwa," Dk. Kafumu alisema.
Aliongeza kuwa: “Pia wabunge wa Muungano walihoji jana (juzi) kuhusu kutohusishwa kwao katika mpango huo wakati fedha zilizorejeshwa serikalini ni za Bunge la Muungano, wao hawapewi madawati maana Zanzibar ina Wizara ya Elimu inayojitegemea. Uongozi wa Bunge uliahidi utaangalia namna ya kushughulikia malalamiko yao."
Mbunge mwingine wa CCM ambaye hakuwa tayari jina lake litajwe gazetini, aliiambia Nipashe kuwa haungi mkono uamuzi wa kurejeshwa fedha serikalini kutokana na kusafiri kwa shida akiwa na moja ya kamati za Bunge hivi karibuni.
Chanzo: Nipashe
![]()

Tatizo kuna watu wanao jipendekeza kwania ya kujijenga zaidi,taabu kweli.Tulia katulizwa pale na muzee sasa ataacha kufuata maelekezo kutoka juu?
Lkn bunge ni muhimili unaojitegemea so ni vizuri wabunge wangeshirikishwa.
sina ajenda yoyote,,,kama kamati za bunge mafungu yake yanaondolewa kwa kigezo cha kubana matumizi unategemea utendaji wa kamati hizo zitakuaje???Nafikiri Mkuu una ajenda yako na Msigwa. Maana naona wewe ume-zero in kwa Msigwa kama vile yeye ndiye tatizo pekee katika suala hili. Mimi nilitaka tujadili tatizo kwa upana wake kwa sababu hii si issue ya mbunge mmoja. Lakini naona unajadili issue hii kisiasa zaidi.
Yaani watanzania Siku hizi ni kama vichaa, hata hamjui unataka Rais awafanyie nini wananchi.Hizi fedha zilitosha kabisa kugharamia shughuli nyingine muhimu za kibunge kama kurushwa matangazo ya bunge na chenji ingebaki.
Hili suala la madawati ya shule naona wanasiasa wanalishadadia kisiasa zaidi.
Aaaaah asigwa kumbe na ww huhitaji kule kwenu mara watoto wakalie madawatiMkuu unajua hayo madawati yanayohitajika hapa nchini hayafiki hata millioni 2??
Kwa mujibu wa wizara ya elimu madawati yanayohitajika ni Millioni 1.5 tu ambazo gharama zake hazifiki Billioni 150, serikali ikiamua hata leo tatizo la madawati linaisha ndani ya miezi mitatu tu.
Hili suala linafanywa kisiasa tu, watu wanatafuta kick.