Wabunge wapinga billlioni 6 kurejeshwa Serikalini

Wabunge wapinga billlioni 6 kurejeshwa Serikalini

Kwahiyo walitaka wasafiri waende nje WAKAANGALIE NYUMBA ZA UBALOZI??? Like serious? Unafunga safari unatumia pesa za walipa kodi kwenda KUANGALIA nyumba za ubalozi??
Aibu naona mimi wallah
_DSC8735.JPG
 
Wabunge wengine buana, watoto wa waliowapigia kura wanakaa chini wao wanataka kubaki na hela ili wale bata?, hii inauma sana kuwa na wabunge ambao sio wazarendo
 
pic+mps.jpg

WABUNGE wa upinzani na wa CCM, wamekosoa uamuzi uliofanywa na uongozi wa Bunge wa kurejesha Sh. bilioni sita serikalini ilhali baadhi ya shughuli za Bunge zimekwama kutokana na uhaba wa fedha.

Aidha, baadhi ya wabunge hao wamedai Rais Dk. John Magufuli, amekuwa akiingilia majukumu ya mihimili mingine, likiwamo Bunge.

Aprili 11, mwaka huu, uongozi wa Bunge ulimkabidhi Rais Magufuli hundi ya Sh. bilioni sita, ambazo ulieleza kuwa uliziokoa kutokana na kubana matumizi.

Rais Magufuli aliupongeza uongozi huo na kuagiza fedha hizo zitumike kutengeneza madawati, huku akizitaka ofisi na taasisi zingine za serikali kuiga mfano huo.

Katika kikao cha wabunge na uongozi wa Bunge hilo kilichofanyika mjini hapa juzi, kuanzia saa 11 jioni hadi saa 2:15 usiku, wabunge waliukosoa uongozi wa Bunge kwa uamuzi huo kwa vile "shughuli nyingi za Bunge zimekwama kutokana na uhaba wa fedha."

Katika mkutano huo, waandishi wa habari walizuiwa kushiriki kwa maelezo kuwa ulikuwa maalum kwa ajili ya maelekezo kwa wabunge.

Mchungaji Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini (CHADEMA), aliiambia Nipashe kwenye viunga vya Bunge jana kuwa wameshangazwa na uongozi wa Bunge kurejesha fedha serikalini wakati kuna mambo mengi ya msingi ya Bunge hayajafanyika, kutokana na ukosefu wa fedha.

"Kamati zingine zimezuiwa kusafiri wa maelezo kwamba hakuna fedha. Kamati ya Mambo ya Nje imezuiwa kusafiri kwa madai kuwa hakuna hela, walitarajia kwenda kuangalia nyumba za ubalozi huko nje, lakini wanaambiwa hakuna fedha, wakati pesa nyingi imerejeshwa serikalini," alisema.

Kadhalika, Mchungaji Msigwa alisema wabunge pia walihoji sababu za kuzuiwa kuonyeshwa moja kwa moja kwa shughuli za Bunge, jambo ambalo alidai limelenga kuminya uhuru wa vyombo vya habari nchini na "kuficha uovu ya serikali."
"Shughuli za Bunge hazionyeshwi moja kwa moja na vyombo vya habari, lakini anachokifanya Rais kinaonekana. Wabunge tulihoji uongozi wa Bunge kuhusu uamuzi huu," alisema.

Msigwa aliongeza kuwa katika mkutano huo, Mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA), Joseph Mbilinyi 'Sugu', alikwenda mbali zaidi akidai Rais Magufuli amekuwa akiingilia madaraka ya mihimili mingine.

Sugu alikumbushia 'kilio cha wapinzani' kuhusu uteuzi wa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Akson.

Rais Magufuli alimteua Dk.Tulia kuwa mbunge wa kwanza ikiwa ni siku mbili baada ya kuteuliwa na Kamati Kuu ya CCM kuingia kwenye ‘tatu bora’ ya kuwania Uspika, jambo ambalo Sugu alidai linatoa taswira Rais alitumia mamlaka yake kumweka kuwa Naibu Spika.

Mbunge wa Igunga (CCM), Dk. Dalali Kafumu, alisema fedha za Bunge kutumika kununua madawati si jambo baya, lakini wabunge walipaswa kushirikishwa kabla ya kufanyika kwa uamuzi wa kurejesha fedha serikalini.

"Uamuzi wa kutengeneza madawati na kila Mbunge kupewa 600 apeleke jimboni kwake ni mzuri, tatizo wabunge hawakushirikishwa," Dk. Kafumu alisema.

Aliongeza kuwa: “Pia wabunge wa Muungano walihoji jana (juzi) kuhusu kutohusishwa kwao katika mpango huo wakati fedha zilizorejeshwa serikalini ni za Bunge la Muungano, wao hawapewi madawati maana Zanzibar ina Wizara ya Elimu inayojitegemea. Uongozi wa Bunge uliahidi utaangalia namna ya kushughulikia malalamiko yao."

Mbunge mwingine wa CCM ambaye hakuwa tayari jina lake litajwe gazetini, aliiambia Nipashe kuwa haungi mkono uamuzi wa kurejeshwa fedha serikalini kutokana na kusafiri kwa shida akiwa na moja ya kamati za Bunge hivi karibuni.

Chanzo: Nipashe
Mh hii ya kuwa mnasafiri nje ili kuona nyumba za mabalozi ndio nini sasa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kwani wao mafundi nyumba au wazibua vyoo???
Wabunge ikifika wakati wa posho hamna cha UKAWA wala CCM wote lao moja tu...... Mamaeeee
 
7d2c6825a326f50e8e783d12416ffee2.jpg

Hawana haya wamezoea kwenda kutumbua nje huko ndiyo kuisoma namba hakuna kutembelea majengo hii dunia ya leo do you need to travel all the team of more then 20 MP's kwenda kukagua hizo balozi? Mkimaliza wabunge team ya kwa CAG nayo inafuata!!!!
 
Hongera JPM kaza uzi zaidi hata safari za ndani watu wapande mabasi tu
 
Ila jf inatakiwa kuwa na ki sign cha dislike [emoji107] yaan kuna watu ninge wapigia leo hadi wakome, pesa hazijaliwa zinaenda kuchonga madawati, hasa apo wana lalamika nini!!!, probably watt wao wana soma seminaries na int. Schools ndo maana wana ona hazi wagusi.

Halafu hela ya posho, nayo wapunguze mapema sana

[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] ila prezidaa kwaweza, mazoea mabaya
 
Wabunge waianshi kimalaika kuliko wakurugenzi wa idara za serikali??

Umewahi kuulizia TANAPA na TPDC na UWERA na BoT na kweingineko wanaishije hao wakurugenzi??

After all budget ya bunge kwa mwaka ni ndogo sana, pamoja na kulipwa posho hizo, inapelekana tu na bajeti ya wizara moja ya serikali.
umeapaniki braza punguza jazba basi
 
Madawati 600 kwa kila MP hawataki eti kisa kuna shughuli za bunge zinakwama
af shughuli zenyewe eti baadhi ya kamati zimeshindwa kusafiri,zimeshindwa kufanya kazi zake kwa ufanisi n.k
kumbe kwao ni bora kamati isafiri ila watoto 600 katika majimbo yao wakae chini SHAME

Na hawa ndio wale wale ambao hurudi kwa wananchi wakijinasibu kwamba ni watetezi wao

kwa mtindo huu lets say tu
GO GO GO GO JPM
 
Yaani inatakiwa vyeo vyote vya kisiasa kuanzia mawaziri,wabunge na kushuka chini mishahara na marupurupu ishuke sana ili kwanza watu wasiache taaluma zao na kukimbilia siasa kwa tamaa ya pesa,ifike mahali mtu ajiulize anagombea ubunge wa nini kwanza hakuna maslahi lakini sasa hivi kama unavyo ona watu wapo kimaslai tu
Kuna kiongozi wa upinzani alikua anauza nafasi hadi milioni 100,wamemtumbua kimya kimya
 
Tangu lini kazi ya bunge ikawa kutengeneza madawati? Tulishaambiwa hii nchi no tajiri sasa maigizo na kiki zinataka kuzidi kwanini serikali isitoe hizo pesa za madawati.
Hili nalo ni jipu
 
KASOME CHANZO CHA HII THREAD, NINAMUONGELEA MSIGWA KWA KUWA YEYE NDIYE ALIYEHOJIWA NA GAZETI LA NIPASHE NA KUSEMA ANAZIHITAJI HIZO HELA KWA AJILI YA KUTEMBELEA BALOZI NA KUONA MAJENGO. SASA HIYO PICHA KAMA INAVYO ONYESHA HAPO HIZO SIYO BALOZI ZA TANZANIA. HAPO MHESHIMIWA MCHUNGAJI MWA MSIGWA ANAJIRUSHA TU. SIWAPO WAWILI HAPO NA WOTE NI CHADEMA. LAKINI HUYU MSIGWA KWA KAULI ZAKE KWA VYOMBO VYA HABARI AMEONYESHA MARA NYINGI KWAMBA AMECOMPROMISE SANA POSITION YAKE AS A MEMBER OF PARLIAMENT AND AS A PASTOR. HANA KABISA HOFU YA MUNGU. KUMBUKA SIYO WOTE WASEMAO BWANA BWANA WATAUONA UFALME WA MUNGU.
 
ulichokiandika hakiendani na uhalisia,,anaeajiri walimu na kuwapangia vituo ni msigwa au huyo meya wa chadema

jiongeze,halafu alichokiongea msigwa ni kuhusu bunge kuzidiwa majukumu huku pesa ilotakiwa kufanya hayo haionekani so sidhani kama msigwa anakosa ama tatizo maana waliolalamika sio msigwa pekeake hata wabungr wa ccm wamelalamika.

kunamuingiliano wa kimamlaka kati ya rais na bunge,inaonekana kabisa bunge linakosa weledi wakufanya shughuli zake kwa uhuru maana kinachoonekana ni serekali kama imejivika madaraka ya kutoa maelekezo nini bunge wafanye na nini wasifanye

WEWE NI MSIGWA MWENYEWE AU UMETUMWA KUMDEFEND. JAMAA ANAJALI SANA MASLAHI YAKE BWANA MCHUNGUZE SANA HATA KAULI ZAKE ZA MARA KWA MARA. WATU WAKO MACHO ANGALIA SANA UNACHO KISEMA NA HOJA ZAKO UNAZO ZITOA. HUYU JAMAA ALIKUWA KUNA KIPINDI ANAFUATILIA SANA UWINDAJI HOLELA NA ALIKUWA MKALI SANA WAKATI LAZARO NYALANDU AKIWA WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII. GHAFLA ALIWEKA U - TURN HATA SIKUAMINI AKAANZA KUMTETEA LAZARO NYALANDU SINCE THAT DAY I KNEW YOU WERE GIVEN ????? AND YOU STARTED TRAVELLING WITH THE MINISTER AROUND THE WORLD, IN PLACES LIKE USA. IT IS VERY UNFORTUNATE. NINGESEMA MENGI LAKINI KWA SASA NAONA NI ISHIE HAPO UNTIL NEXT TIME.
 
Hizi fedha zilitosha kabisa kugharamia shughuli nyingine muhimu za kibunge kama kurushwa matangazo ya bunge na chenji ingebaki.

Hili suala la madawati ya shule naona wanasiasa wanalishadadia kisiasa zaidi.
Inafika mahala hatuitaji kuwaona wala kuwasikia kwa mambo yao ya kipuuzi tutawasoma tu magazetini,mana jambo la maana wanaweka mbele matumbo yao nini maana kutuwakilisha?. Kipindi nipo huku miyuji Dodoma,wakiwa bungeni J'MOSI wanapishana magari tu kwenda mnada wa MSALATO kula nyama na kuhonga wanachuo kwa pesa za umma ,hawa watu wanakera sana.Kitu chenye manufaa kwa umma hata Rais kama kaingilia kati kuna ubaya gani sindo pa kumsupport mana anajenga habomoi.WALITAKA ZIONGEZE KWENYE POSHO ZAO?
 
Yaani umewapa za uso. Eti wanataka kwenda kuangalia nyumba za balozi zetu!!!! Kwa hali hiyo sioni faida ya bunge!!!!
Hivi Msigwa ana akili kweli? Na povu linamtoka kabisa madawati kwa students na kwenda kuangalia nyumba nje kipi bora? ? Duhh Tanzania nchi yangu
 
pic+mps.jpg

WABUNGE wa upinzani na wa CCM, wamekosoa uamuzi uliofanywa na uongozi wa Bunge wa kurejesha Sh. bilioni sita serikalini ilhali baadhi ya shughuli za Bunge zimekwama kutokana na uhaba wa fedha.

Aidha, baadhi ya wabunge hao wamedai Rais Dk. John Magufuli, amekuwa akiingilia majukumu ya mihimili mingine, likiwamo Bunge.

Aprili 11, mwaka huu, uongozi wa Bunge ulimkabidhi Rais Magufuli hundi ya Sh. bilioni sita, ambazo ulieleza kuwa uliziokoa kutokana na kubana matumizi.

Rais Magufuli aliupongeza uongozi huo na kuagiza fedha hizo zitumike kutengeneza madawati, huku akizitaka ofisi na taasisi zingine za serikali kuiga mfano huo.

Katika kikao cha wabunge na uongozi wa Bunge hilo kilichofanyika mjini hapa juzi, kuanzia saa 11 jioni hadi saa 2:15 usiku, wabunge waliukosoa uongozi wa Bunge kwa uamuzi huo kwa vile "shughuli nyingi za Bunge zimekwama kutokana na uhaba wa fedha."

Katika mkutano huo, waandishi wa habari walizuiwa kushiriki kwa maelezo kuwa ulikuwa maalum kwa ajili ya maelekezo kwa wabunge.

Mchungaji Peter Msigwa, Mbunge wa Iringa Mjini (CHADEMA), aliiambia Nipashe kwenye viunga vya Bunge jana kuwa wameshangazwa na uongozi wa Bunge kurejesha fedha serikalini wakati kuna mambo mengi ya msingi ya Bunge hayajafanyika, kutokana na ukosefu wa fedha.

"Kamati zingine zimezuiwa kusafiri wa maelezo kwamba hakuna fedha. Kamati ya Mambo ya Nje imezuiwa kusafiri kwa madai kuwa hakuna hela, walitarajia kwenda kuangalia nyumba za ubalozi huko nje, lakini wanaambiwa hakuna fedha, wakati pesa nyingi imerejeshwa serikalini," alisema.

Kadhalika, Mchungaji Msigwa alisema wabunge pia walihoji sababu za kuzuiwa kuonyeshwa moja kwa moja kwa shughuli za Bunge, jambo ambalo alidai limelenga kuminya uhuru wa vyombo vya habari nchini na "kuficha uovu ya serikali."
"Shughuli za Bunge hazionyeshwi moja kwa moja na vyombo vya habari, lakini anachokifanya Rais kinaonekana. Wabunge tulihoji uongozi wa Bunge kuhusu uamuzi huu," alisema.

Msigwa aliongeza kuwa katika mkutano huo, Mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA), Joseph Mbilinyi 'Sugu', alikwenda mbali zaidi akidai Rais Magufuli amekuwa akiingilia madaraka ya mihimili mingine.

Sugu alikumbushia 'kilio cha wapinzani' kuhusu uteuzi wa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Akson.

Rais Magufuli alimteua Dk.Tulia kuwa mbunge wa kwanza ikiwa ni siku mbili baada ya kuteuliwa na Kamati Kuu ya CCM kuingia kwenye ‘tatu bora’ ya kuwania Uspika, jambo ambalo Sugu alidai linatoa taswira Rais alitumia mamlaka yake kumweka kuwa Naibu Spika.

Mbunge wa Igunga (CCM), Dk. Dalali Kafumu, alisema fedha za Bunge kutumika kununua madawati si jambo baya, lakini wabunge walipaswa kushirikishwa kabla ya kufanyika kwa uamuzi wa kurejesha fedha serikalini.

"Uamuzi wa kutengeneza madawati na kila Mbunge kupewa 600 apeleke jimboni kwake ni mzuri, tatizo wabunge hawakushirikishwa," Dk. Kafumu alisema.

Aliongeza kuwa: “Pia wabunge wa Muungano walihoji jana (juzi) kuhusu kutohusishwa kwao katika mpango huo wakati fedha zilizorejeshwa serikalini ni za Bunge la Muungano, wao hawapewi madawati maana Zanzibar ina Wizara ya Elimu inayojitegemea. Uongozi wa Bunge uliahidi utaangalia namna ya kushughulikia malalamiko yao."

Mbunge mwingine wa CCM ambaye hakuwa tayari jina lake litajwe gazetini, aliiambia Nipashe kuwa haungi mkono uamuzi wa kurejeshwa fedha serikalini kutokana na kusafiri kwa shida akiwa na moja ya kamati za Bunge hivi karibuni.

Chanzo: Nipashe

" Kamati ya Mambo ya Nje walitegemea kwenda kuangalia nyumba za ubalozi huko nje wakaambiwa hakuna fedha"- Sijui kwenda tu kuangalia nyumba za ubalozi nje au kuwatengenezea madawati wanafunzi ni kipi muhimu? Afterall, maelezo wakati wa kukabithi hundi hiyo yalikuwa ni kwamba " ni fedha zilizopatikana baada ya kubana matumizi"- kubana matumizi ni pamoja na safari za kwenda kushangaa majengo ya ubalozi nje. Kama kamati ilitaka kweli kujua hali ya majengo hayo ziponjia nyingi tu za kufanya hivyo, wangeweza kutumia picha n.k
Huu utaratibu wa kamati za bunge kuzunguka duniani kwa kisingizio cha kujifunza sijui umesaidia nini tangu uaanze? Ni eneo la kutumia fedha za walipa kodi wa nchi hii vibaya tu
 
Kuna baadhi ya wabunge waliwekeza mapesa mengi sana ili wapate ubunge yakiwa na nia ya kupiga mapesa kutokana na rushwa kutoka kwenye mashirika ya umma pamoja na Maposho ya kufa mtu. Sasa Hali si shwali maana Mashirika ya umma JPM kashikiria account zote kila senti anachungulia. Kapiga chini watumishi hewa na matumizi yasiyo ya lazima katika taasisi za umma na serikalini.Sasa Njaa kuu imeingia bungeni Ndio maana Baadhi wasiyo na soni wanajitokeza na kulalamika kuhusu mtonyo huu wa bil.6. Poleni Ndugu zangu sisi tupo tuanahitaji hizo nafasi kama maona hazilipi mtuachie maana tunahasira za kumuonyesha JPM majembe yapo mtaani.

Ni wazo tu.
 
si umeona mpaka akina msigwa MBOWE wameanza kutafuta huruma
. sipati picha tutakapoanza kuondoa ruzuku ya vyama , na posho ya makalio
 
Back
Top Bottom